BAADHI YA DALILI ZA MTU ALIYEKUFA KIROHO

Na Nyandula Mwaijande.

i. Mtu kuishi maisha yake ya kale
ii. Kutoona thamani ya maisha ya kiroho
iii. Kutoogopa kutenda dhambi
iv. Kutoona utamu wa kuishi na Yesu
v. Kutokupenda kufanya toba
vi. Kutokupenda kuomba au kutoa msamaha
vii. Kutojisikia hamu ya kusali
viii. Kutokuwa na shauku ya kusoma na kutafakari Neno la Mungu
ix. Kutokuwa na hamu ya kushiriki sala pamoja na wengine. Hata akifanya hivyo ni kwa sababu ya kutimiza wajibu tu.
x. Kuwa mkali hata kwa kwa kitu kidogo na kujawa na hasira.
xi. Kupoteza ile roho ya wito na kuanza kufikiri mno mambo ya ulimwengu.
xii. Kunung’unika kwa kila analotendewa na wala haoni jema kwa wenzake.
xiii. Ni vigumu kwake kujitoa kwa muda, mali hata kwa ajili ya kanisa na wahitaji.
xiv. Kuwa na tabia ya kupiga mayowe ya fujo na kuwa kero kwa wengine.
xv. Mara nyingi hasikii na wala hapendi kupokea ushauri.
xvi. Kujihisi kutopendwa.
xvii. Kuhisi kutendewa vibaya tu na kila mmoja.
xviii. Kukosa amani, furaha na utulivu.
xix. Kuwa msiri, kutoshirikisha wengine mambo yake lakini anapenda sana kujua mambo yaw engine na kuyaeleza kwa wengine.
xx. Kuwa na hofu/wasiwasi.
xxi. Kupoteza ari ya kueneza injili (kushuhudia).
xxii. Kuwa mtu wa sababu nyingi kwa kila jambo.
xxiii. Kupoteza uaminifu na utii kwa Mungu pamoja na kujawa na kiburi.
Ndugu yangu nimeona nikukumbushe ili ukiona baadhi ya dalili hizo kwako ujue unahitaji kutengeneza na Mungu haraka ili udumu katika maisha ya kiroho pia ni vema kusimama kwenye zamu yako kwa njia ya maombi pamoja na kusoma sana Neno la Mungu maana huko ndiko utagundua mistari ya kutiwa moyo, kuimarishwa, kufundishwa na hata kukemewa unapofanya tofauti na mapenzi ya Mungu. Kusoma Neno la Mungu ni njia nzuri katika safari ya maisha ya kiroho kwa sababu Neno la Mungu linaokoa, linaponya, linabariki, linabadilisha na kuneemesha maisha yetu ya kiroho.


MUNGU AKUBARIKI SANA .

By Nyandula Mwaijande.

Comments