FAHAMU JINSI MUNGU ALIVYOJIFUNUA ZAMANI, NA JINSI ALIVYOJIFUNUA KATIKA NYAKATI HIZI TULIZONAZO.

Bwana Yesu asifiwe wapendwa!. 

Mungu wetu ni Mungu ambaye amejifunua kwetu kwa nyakati mbili tofauti, wakati wa agano la kale na wakati wa agano jipya. Lakini pamoja na kujifunua kwa nyakati mbili na kwa njia tofauti bado Mungu wetu hajabadilika, ni yule yule jana, leo, na hata milele.

Na Mtumishi Alex
 Katika AGANO LA KALE, MUNGU alisema na watu wake kwa njia ya manabii katika sehemu kubwa, lakini katika AGANO JIPYA, MUNGU anasema na watu wake kupitia KRISTO YESU, hii ndiyo njia pekee ambayo Mungu amejifunua katika nyakati hizi tulizonazo. 
Hebu tuangalie Biblia inasemaje
Waebrania 1:1-4  ''Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,  mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.  Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;  amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.


Ndugu mpendwa katika KRISTO YESU, tamani sana kusema na Bwana YESU katika maisha yako kuliko kitu kingine chochote. 
Barikiwa sana. 
By ALEX wa YESU.

Comments