HAKIKISHA UKO NDANI YA SAFINA

BWANA YESU asifiwe!
Karibu.
BWANA MUNGU Alimwambia Nuhu Atengeneze Safina Maana Mwisho Wa Viumbe Vyote Umekaribia(Mwanzo 6:13-14 , MUNGU akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia. Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami. )

Sababu Ya Mwisho Wa Viumbe Vyote Kukaribia Ni Kwa Sababu -Mwanadamu Amemsahau MUUMBA, 
-Mwanadamu Anawaza Ngono Tu Masaa 24, 
-Mwanadamu Anamwabudu Shetani Na Sanamu Zake, -Mwanadamu Anatoa Mimba Kila Mara Kama Tu Anapenga Kamasi, Yaani Kila Zikija Kamasi Anazitoa, 
-Mwanadamu Akiamka Tu Anakwenda Bar kulewa Wala Sio Kumwabudu MUNGU, 
-Mwanadamu Anawaona Watumishi Wa MUNGU Kama Waliokosa Kazi. 
Mwisho Ulifika Na Wote Wakafa. 
Watu wote duniani nzima walikufa wote kwa sababu tu hawakuwa ndani ya Safina.
Kwenye Safina ya Nuhu walipona watu 8 tu yaani Nuhu na mkewe, Yafehi na mkewe, Hamu na mkewe pamoja na Shemu na mkewe.
Safina ilikuwa ni muhimu sana kwa Nuhu na wanae. wanadamu wote hawakuamini kwamba inawezekana watu wote dunia nzima kufa siku moja? Hawakuamini lakini ndivyo ilivyokuwa, walikufa wote isipokuwa watu 8 walikua ndani ya Safina. Hata leo kuna mamilioni ya watu hawaamini kama kuna jehanamu ya moto. Watu hawaamini kama kuna moto wa milele, shetani amewapumbaza na wanajiona wako salama kumbe sio salama.
Hata leo kuna Safina ndugu yangu.

Mathayo 24:37-44 ''Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja BWANA wenu. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja. ''
Ndugu yagngu, BWANA YESU siku moja atarudi je atakukuta wapi? BWANA YESU atakukuta unafanya nini? Yeye kama safina ya mwisho; siku ya mwisho ikifika je utakutwa ndani ya safina hata usiende jehanamu? Siku ya kufa kwako ikifika; Je utakuwa ndani ya safina ili uende mbinguni?
 

Luka 17:26-27 ''Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu. Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote. ''

Ndugu yangu, MUNGU Ameamua Kuleta Safina Ya Mwisho, Safina Hii Wala Haitabeba Wanyama Na Ndege Bali Wanadamu. Safina Yetu Ni BWANA YESU (Yohana 1:12-13, Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. ). 

BWANA YESU Alikufa Msalabani Ili Atuokoe. Ukitaka Leo Kuingia Kwenye Safina Hii Jikane Mwenyewe Luka 9:23-24 '' Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. ''. 

Ukimpokea YESU, Yeye Atakupa Uzima Na Siku Ya Mwisho Atakufufua (Yohana 6:40 , Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana(YESU) na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. )


YESU Anaandaa Makazi Ya Watakatifu Mbinguni (Yohana 14:2-3, Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Nami niendako mwaijua njia. )

-Ndugu Kimbilia Kwenye Safina Hii Pekee Ya Kukupa Uzima Wa Milele.
 -Ndugu Mkimbilie KRISTO Mwenye Uzima Wako Wa Milele.
Safina yetu ni BWANA YESU hivyo kila mmoja ahakikishe ameingia kwenye safina hii ya kutupeleka uzima wa milele.

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292

mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

 

Comments