BWANA  YESU asifiwe ndugu.
Karibu tuzibomoe ngome za shetani ambazo hutenda kazi ndotoni hadi hadharani.
Ndugu mmoja aliniuliza swali ambalo ndilo lilipelekea MUNGU kunipa ujumbe huu, ndugu huyo aliuliza kwamba '' Naota mara kwa mara nafanya mapenzi na watu tofauti tofauti ndotoni, watu hao wengine nawafahamu na wengine siwafahamu naomba unisaidie kujua maana yake na jinsi ya kuzuia jambo hili ambalo hunifanya nijichafue kila siku, na wakati mwingine nikiamka nakuta dalili zote za kwamba nilifanya mapenzi muda mfupi uliopita, na hata uchovu nakuwa nao. UBARIKIWE''
BWANA YESU asifiwe.
Ngoja nikufundishe jambo hili kuhusu ndoto hizo chafu.
Ukiota unafanya 
mapenzi ndotoni maana yake una jini mahaba au jini maimuna. Yaani kama 
wewe ni mwanamke basi una mme wa rohoni ambaye ni jini na kama wewe ni 
mwanamume basi tambua kwamba una mke wa rohoni wa kipepo ambaye siku 
akitaka kuja huja na wewe unaona ni ndoto kumbe alikuja na kufanya ngono na wewe  na haya yanatokea kwa mtu ambaye hana ulinzi wa damu ya YESU 
KRISTO. 
Kuna aina 3 za mashetani.
1. shetani mwenyewe.
2. wakuu wa idara za kipepo.
3. watenda kazi.
maimuna ni mmoja wa wakuu wa vitengo wa shetani, na kitengo chake ni 
kuleta ukahaba kwa wanadamu. Watenda kazi ni majini hawa wa kawaida 
ambao hutumwa na maimuna kuja kufanya ukahaba na wanadamu ambao hawana 
ulinzi wa damu ya YESU KRISTO. maimuna anaweza kutuma jini la kike kwa 
ajili ya kwenda kufanya mapenzi na wanadamu wanaume na  na kama 
mwanadamu aliyekusudiwa ni mwanamke basi hutumwa jini la kike. na majini 
yote ya ukahaba yanaitwa maimuna na wakati mwingine kwa sababu majini 
haya ni viumbe wa kiroho huweza kuwaingia watu kabisa na kuwatumikisha 
kipepo. Ndio maana wengi tumewaombea na mapepo yakiwa yanatoka husema 
wao ni maimuna, ukisikia hivyo wewe mtumishi wa MUNGU tambua kwamba 
unayemuombea alikuwa anateswa na jini mahaba au jini maimuna. maimuna ni
 ukoo wa majini mahaba yote ndio maana nimewahi kumwombea mtu nikiwa 
Zanzibar akiwa anateswa na jini mahaba au maimuna na hata hapa Dar 
nimewahi kumwombea Dada mmoja ambaye naye alikuwa na jini mahaba, hivyo 
unaweza kushangaa kwamba jini mahaba wa Zanzibar kafikaje Dar kumbe jina
 hilo maimuna ni jina la ukoo wa majini yote ya ukahaba. 
mapepo haya 
yakimwingia mtu mtu huyo hubadilika mara moja. Kama mme au mke alikuwa 
mwaminifu kwenye ndoa yake basi yakimwingia haya majini mahaba huanza 
kutokuridhika na mwanandoa mwenzake na kuanza kutoka nje ya ndoa, ni 
hatari sana . 
Wapo wadada wengi hujiuza miili yao, chanzo ni jini mahaba
 aliyewaingia.Ndugu yangu ukiota ndoto za kufanya mapenzi mara kwa mara 
kemea sana jambo hilo kwa maombi ya vita kupitia jina la YESU KRISTO. 
Yohana 8:36 Biblia inasema ''BWANA YESU akikuweka huru , utakuwa huru 
kwelikweli.''
-Atakuwa ameingia agano na mashetani.
-hakikisha unampokea BWANA YESU kuwa BWANA na MWOKOZI wa 
maisha yako na baada ya hapo 
-uwe mtu wa vita yaani mwana maombi  na tena 
-hakikisha kila siku kabla ya kulala unaomba maombi kwamba damu ya YESU 
KRISTO ikuzingire pande zote maana Tunamshinda shetani kwa damu ya 
Mwana kondoo YESU KRISTO-uFUNUO 12:11.
 Na kwa sababu ya uonevu wa shetani
 na majini yake kuzidi sana duniani '' Kwa kusudi hili BWANA YESU 
alidhihilishwa ili azivunje kazi zote za shetani- 1 Yohana 3:8b.
 JIFUNIKE KWA DAMU YA YESU SIKU ZOTE KWA MAOMBI HAYA.
 
BWANA MUNGU Ninakushukuru Kwa Kunilinda, Asante Kwa Damu Ya Mwanao YESU KRISTO Inenayo Mema Siku Zote. Najifunika Kwa Damu Ya YESU KRISTO, Ninawafunika Ndugu Zangu Wote Kwa Damu Ya YESU KRISTO, Nafunika Familia Yangu, Ndugu Zangu, Nyumba Yangu, Biashara Yangu, Ofisi Yangu, Chakula Changu, Fedha Zangu, Kiwanja Changu, Rafiki Zangu, Majirani Zangu Huduma Yangu Na Kila Kinachonihusu Kwa Damu Yenye Nguvu Ya YESU KRISTO Wa Nazareth. Ninalifunika Anga Lote, Nchi Yote Na Bahari Yote Kwa Damu Ya YESU KRISTO. Imeandikwa Katika Ufunuo 12:11 " Nao Wakamshinda(shetani) Kwa Damu Ya Mwana Kondoo(YESU) Na Kwa Neno La Ushuhuda Wao" Ewe shetani, Nimeitumia Damu Ya YESU KRISTO Kukushinda Sasa Na Hata Milele Katika Jina La YESU KRISTO, jini mahaba nakutetekeza kwa jina la YESU KRISTO maana Neno la MUNGU katika Yeremia 1:10 kwamba MUNGU ameniweka juu ya falme zote za mashetani ili kuwang'oa mashetani, na kuwabomoa na kuwaharibu na kuwaangamiza kwa jina la YESU KRISTO. Sasa nawaangamiza majini wote waliotumwa kwangu kutoka kuzimu kwa jina la YESU KRISTO Amen.

 Kwa
 sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku 
nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio 
kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na 
utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi 
kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko 
KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
   
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
Comments