![]() |
Na Alex Emmanuel Bubelwa. |
Wote tuliomwamini Mwokozi tunajua ukweli ya kuwa , ipo siku moja Itakayokuwa ni ya kuushangaza Ulimwengu wote. Ni siku ambayo dharau na kebehi kwa watakatifu wa Mungu zitakoma,

Ninazungumzia siku ambayo Mfalme Yesu atarudi kwa ajili ya kulinyakua Kanisa lake ili kuliepusha na Saa ya kuharibiwa itakayoupata ulimwengu wote.
YESU ATARUDI LINI?

Amin, nawaambia, kizazi hiki (kizazi kimoja ni miaka 100 Kibiblia kwa mujibu wa Mwanzo 15:13,16. Hivyo alisema kizazi kilichopo tangu Wasraeli waliporudi kwenye nchi yao mwaka 1948 ) hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia. (Math 24:32-34)
Ni miaka takribani minane imepita tangu mwaka 2006, tangu gazeti la Nyakati lilipoandika habari ya mtu mmoja aliyetoa unabii akisema Yesu amemdhibitishia ya kuwa atarudi na kulinyakua Kanisa mwaka 2014, ambao ni mwaka huu!
Simuiti Nabii wa uwongo kwa kuwa mwaka huu haujaisha!
MAISHA YAKO UNAYAJUA MWENYEWE, JIULIZE IWAPO PARAPANDA LINAPULIZWA MUDA HUU UTAKUWA KATIKA HALI GANI?
MARAN ATHA!
MUNGU akubariki sana.
By Alex Emmanuel Bubelwa.
Comments