IMANI ITENDAYO KAZI

Na SNP MWANGASA (Ufufuo na Uzima, Moshi)

i) UTANGULIZI
Luka 17:11, hii na habari ya watu 10 waliokuwa na ukoma ambao walimwendea Yesu ili awaponye, na Yesu akawaambia nendeni mkajinyeshe kwa makuhani. Na wakati wakiwa njia kwenda huko wakakutana na uponyaji wao na wote wakatakaswa.
Tunaweza kujifunza mambo kadhaa kuhusu hii habari, kwa kipindi kile wakoma ni watu waliohesabika kama wamepigwa na Mungu. Na kwa namna hiyo watu wengi walikuwa wanawatenga .. katika hali ya kawaida ni watu waliokuwa wakidharauliwa na kukosa heshima miongoni mwa watu. kwa wakati huo ndipo walipoamua kukaa mahali ambapo Yesu anapita.. na baada ya Yesu kuwakuta akawaambia wakajionyeshe kwa makuhani. 
 
1. CHANZO CHA IMANI

Tunajifunza imani kuu iliowaponya hawa wakoma .. baada ya kusikia lile neo wakaamua kutenda sawasawa na lile neno. TUTAONA HILI katika kitabu cha warumi 10:17, “Imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la kristo.” Mambo ya kujifunza ni kuwa imani chanzo chake ni kusikia, tukiishia hapo tunajifunza kitu hapa, tukiangalia kwenye biblia utagundua baada ya neno kusikia kuna alama ya mkato ikimaanisha imani chanzo chake ni kusikia. Kumbe imani yoyote ya kushindwa au ya kushindwa yanatokana na kile unachosikia.
 
2. NGUVU YA KUSIKIA

Kama tulivyoona kwenye andiko hapo juu, kuwa imani inaandia kwenye kusikia. “masikio yetu yanaweza kutupelekea katika kuanguka au kuinuka” ni muhimu kujua kila unachosikia kinaleta IMANI ndani ya mtu, ambayo yaweza kuwa nzuri au mbaya kutegemea kile ulichosikia. Na ndio maana , shetani hutumia sana masikio kuwafanya watu wamtumikie yeye.

2.1 Uzuri wa kusikia.
Unapohabari za Mungu, na neno la kristo basi imani na nguvu ya Mungu itaingia kwenye maisha yako. Kwa maana hata wale wakoma walisikia neno kutoka kwa kristo. Na hapo wakapata imani ya kuchukua hatua na baada ya kuchukua hatua ya kuamua kwenda kujionyesha hapo wakapokea utakaso wao.. lakini la kujifunza hapa ni kwamba imani yao imepatikana baada ya kusikia NENO kutoka kwa kristo.
 
2.2 Hatari ya mambo tunayoyasikia.
Ni muhimu kujua kile unachosikia kina leta kesho yako, “maisha unayoishi leo ni matokeo yayale uliyowahi kusikia” na ndio maana shetani anatumia hiyo kukamata na anataka usikie mambo mabaya ili utende mabaya. Na ndio maana ukifuatilia kwenye maisha yako huwezi kukumbuka kama kuna mtu aliyewahi kukufundisha dhambi, lakini unajikuta unatenda kwa kuwa habari za dhambi zimeenea zaidi kuliko taarifa za nuru.
 
3. MAPENZI YA MUNGU
 
2 Timotheo 4:7 “nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda”. Yohana 10:10 “mwivi haji ili aharibubu,kuua na kuchinya lakini mimi nilikuja ili muwe na uzima tele” kumbe kazi ya Yesu duniani ni bayana nay a shetani ni bayana.. Paulo alisema amemaliza kazi ya kristo. Na ndiomaana neno imani linaingia pale, kwasababu huwezi kutenda kazi ya kristo bila kuwa na imani ya YESU ndani yako. Na imani chanzo chake ni kusikia kumbe unaposikia habari za kristo unajikuta unatenda kazi ya kristo. Na unaposikia habari za upande wa shetani utajikuta unatenda kazi za shetani.
Unalolisikia laweza kukuingiza kwenye laana nau Baraka. Jifunze kusikia neno la Mungu. Nandio maana biblia inasema kwenye kitabu cha 2 wakorintho 10:3-5 “tukiteka nyara kila fikra” kumbe fikri zetu na mawazo yetu ni muhimu yawe katika kumtii Mungu , lakini ili fikra iweze kumtii Mungu ni lazima isikie neno la Mungu. (warumi 10:17)

Comments