JIFUNIKE KWA DAMU YA YESU NA MWOMBE ROHO MTAKATIFU AKUONGOZE KWENYE MAOMBI.

 

 BWANA YESU asifiwe.
Haya ni maombi ambayo yanaweza kukusaidia kuomba muda mrefu.
Watu wengi wameniambia kwamba hawawezi kuomba muda mrefu hivyo ninachosema ni kwamba tubu dhambi kwanza na hakikisha uko safi mbele za BWANA na baada ya kutubu omba maombi yafuatayo hapo chini kisha sema hitaji lako lolote. Ubarikiwe sana.

JIFUNIKE KWA DAMU YA YESU SIKU ZOTE KWA MAOMBI HAYA.

BWANA MUNGU Ninakushukuru Kwa Kunilinda, Asante Kwa Damu Ya Mwanao YESU KRISTO Inenayo Mema Siku Zote. Najifunika Kwa Damu Ya YESU KRISTO, Ninawafunika Ndugu Zangu Wote Kwa Damu Ya YESU KRISTO, Nafunika Familia Yangu, Ndugu Zangu, Nyumba Yangu, Biashara Yangu, Ofisi Yangu, Chakula Changu, Fedha Zangu, Kiwanja Changu, Rafiki Zangu, Majirani Zangu Huduma Yangu Na Kila Kinachonihusu Kwa Damu Yenye Nguvu Ya YESU KRISTO Wa Nazareth. Ninalifunika Anga Lote, Nchi Yote Na Bahari Yote Kwa Damu Ya YESU KRISTO. Imeandikwa Katika Ufunuo 12:11 " Nao Wakamshinda(shetani) Kwa Damu Ya Mwana Kondoo(YESU) Na Kwa Neno La Ushuhuda Wao" Ewe shetani, Nimeitumia Damu Ya YESU KRISTO Kukushinda Sasa Na Hata Milele Katika Jina La YESU KRISTO. Amen.




MAOMBI YA KUMWOMBA ROHO MTAKATIFU AKUONGOZE KWENYE MAOMBI.

BABA Katika Jina La YESU KRISTO Nakushukuru Kwa Uzima Ulionipa. ROHO MTAKATIFU Ninaomba Uwe Pamoja Nami Katika Vita Dhidi Ya shetani Na Wajumbe Wake. ROHO MTAKATIFU, Wewe Ni Mfariji Wangu, Pigana Vita Hivi Kwa Ajili Yangu Na Unifariji Katika Jina La YESU. Siwezi Kuomba Kama Vile Uombavyo Wewe. Nakusihi Sema Nami Sasa Ukikitumia Kinywa Changu Katika Jina La YESU KRISTO. Nakuomba Unilinde Na Kuniongoza, Unifundishe Jinsi Ya Kuomba, Nitumie Kama Shoka Lako Katika Vita Dhidi Ya Adui. Uje Katika Nguvu Na Uweza Wako Na Ukaonyeshe Ukuu Wako Dhidi Ya shetani Na Wajumbe Wake Katika Jina La YESU KRISTO. Amen.



  Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292

mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments