JINSI UNAVYOWEZA KUMTAFUTA MUNGU NAYE AKATENDA MAKUU JUU YAKO.

Bwana YESU asifiwe. 
Mtumishi Alex
MUNGU wetu ni Mungu wa utaratibu na ili MUNGU atende makuu katika maisha yako lazima ufanye yafuatayo:- LAZIMA UWE SAFI MBELE ZA MUNGU, LAZIMA UMTAFUTE MUNGU KWA BIDII, LAZIMA UWE MWELEKEVU. Hebu tuangalie neno linasemaje "AYUBU 8:5-7 Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii na kumsihi huyo Mwenyezi, ukiwa wewe u safi na mwelekevu, hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako na kuyafanya makazi yako kufanikiwa, tena ajapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa mdogo lakin mwisho wako ungeongezeka". Baada ya kufanya hayo Mungu anaahidi MAFANIKIO katika maisha yako!!

. "2NYAKATI 7:14" Pia Mungu anaeleza mambo mhimu katika fungu hili, mambo hayo ni UNYENYEKEVU, KUACHA NJIA MBAYA, KUOMBA na KUTAFUTA USO WA BWANA. Kwa hiyo ili Mungu atende mambo makuu katika maisha yako lazima uzingatie hayo. baada ya hayo Mungu anaahidi kwamba ATASIKIA KUTOKA MBINGUNI, ATATUSAMEHE DHAMBI, ATAIPONYA NCHI. Mungu atusaidie kuyatenda hayo. 

 UTUMISHI KTK MAZINGIRA YANAYOTUZUNGUKA. 

 MTUMISHI KATIKA MAZINGIRA YANAYOMZUNGUKA ANAKUTANA/ANAKUMBANA NA VITU GANI!. 

Mtumish katika kazi yake ya kumtumikia MUNGU anakutana na mambo mengi, yafuatayo ni baadhi ya mambo hayo:-

 (1)Lazima akutane na imani za kishirikina za kuabudu miungu. "DANIEL 3:8-18" Biblia inaeleza jinsi watumishi hawa wa MUNGU yaani Shadraka, Meshaki na Abednego walivyojikuta katika huduma yao wakipambana na ibada za miungu. 

 (2)Lazima huduma yake au imani yake ipingwe. "Mdo 5:26-33". Wakat mitume walipokuwa wakifanya hudama yao wapo watu walioinuka na kupinga huduma hiyo, unaweza kusoma fungu hilo hapo juu. 

(3)Lazima utakumbana na majaribu pamoja na vishawish vingi, unaweza kusoma habar za YUSUFU katika MWANZO 39:6-20. Mwisho wa somo hili. Ninajua MUNGU ana mpango na maisha yako, hivyo tamani sana kumtumikia MUNGU katika  maisha yako.

 MUNGU HUKUMBUKA NA HUSIKILIZA KILIO CHA WATU WAKE!.

 Kile unachomwomba MUNGU huwa anakumbuka na hawezi kukusahau hata siku moja. "KUTOKA 2:23-25 HATA BAADA YA SIKU ZILE NYINGI MFALME WA MISRI AKAFA, WANAWAISRAEL WAKAUGUA KWA SABABU YA ULE UTUMWA, WAKALIA KILIO CHAO KIKAFIKA JUU KWA MUNGU KWA SABABU YA ULE UTUMWA, MUNGU AKASIKIA KUUGUA KWAO MUNGU AKAKUMBUKA AGANO LAKE ALILOLIFANYA NA IBRAHIMU NA ISAKA NA YAKOBO, MUNGU AKAWAONA WANAWAISRAEL NA MUNGU AKAWAANGALIA".
 Kumbe yale magumu unayopitia Mungu anayaona na wala hajakusahau. Biblia inasema Wanawaisraeli wakamlilia MUNGU na MUNGU akasikia kilio chao na kuyaona mateso yao jinsi walivyokuwa wametumikishwa na Wamisri. Ni kwel Mungu aliwaokoa na mateso yao, ndio maana anasema katika KUTOKA 3:8 kwamba atashuka ili awaokoe na mikono ya wamisri na kuwapandisha kutoka nchi ile hata nchi njema. Nataka nikutie moyo kuwa usiangalia tatizo ulilonalo bali mtazame YESU KRISTO ili akuokoe na tatizo lako. 

  Imani ya mtu ambaye ameamua kumwamini YESU kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake imani yake huanza kukua kama vile mtoto anavyokuwa, Mkristo ambaye amemwamini YESU ili akuwe kiimani lazima apewe chakula na chakula hicho ni "Neno la MUNGU"(WAIBRANIA 5:13-14). "MTU AKIKUWA KIIMANI ANAPOKEA MAMBO MAKUU SABA":- 
(1)Anapokea roho ya hekima->YAKOBO 3:17, 
 (2)Anapokea roho ya maarifa->2TIMOTHEO 2:23,
 (3)Anapokea roho ya uweza->Mdo 16:16-18, 
(4)Anapokea roho ya ufahamu->1FALME 13:11-26, 
(5)Anapokea roho ya shauri->YAKOBO 5:19-20, 
 (6)Anapokea roho ya kumcha MUNGU->Mdo 10:1-4, (7)Anapokea roho ya furaha->WAFILIPI 4:4-7. 

HEKIMA YA KIMUNGU ITOKAYO JUU INA MAMBO YAFUATAYO:- (YAKOBO 3:17) Ni safi, Ni ya amani, Ni ya upole, Imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, Haina unafiki, Iko tiyali kusikiliza maneno ya watu. Barikiwa sana na KRISTO YESU. By Alex wa YESU.

Comments