JINSI YA KUFUTA LAANA ULIYONAYO NA KUHARIBU MIZIMU YA UKOO WENU.

BWANA YESU asifiwe.
Karibu nikupe siri hizi ambazo zitasababisha uzima kwako na kuishi kwa raha. Neno la kutuongoza ni Yohana 8:36 inayosema ''Basi Mwana(YESU) akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. ''

Watu Wengi Wanateswa Na Laana Mbalimbali Zikiwemo Laana Kutoka Kwa Wazazi, Ndugu, Walimu, Majirani, Wachawi, Waganga Wa Kienyeji, Majini, Mizimu Nk. Laana Hizi Ni Mbaya Sana Na Wakati Mwingine Walio Kulaani Kama Ni Wanadamu Walishakufa Tayari, Huna Jinsi Ya Kuwaomba Msamaha Ili Laana Ifutwe, Wakati Mwingine Laana Zingine Ni Sahihi Kabisa Maana Ulifanya Jambo Baya Ukalaaniwa, Umeshindwa Kulivua Hilo Vazi La Laana Ulilovalishwa,

Na Fomular Ya Laana Ni Kwamba Mkubwa Anamlaani Mdogo, Mdogo Hawezi Kumlaani Mkubwa, Na Kama Mkubwa Ndiye Anayemlaani Mdogo Hivyo Kunahitajika Nguvu Kubwa Kuliko Mtoa Laana Ndipo Laana Inaondoka.

 Isipokuwa Laana Ya MUNGU, Hiyo Haina Dawa Zaidi Ya Kutubu Na Kumwomba MUNGU Yeye Atakusamehe Na Laana Itaondoka Kwako.
Lakini Laana Zingine Zote Zitaondoka Kwako Kwa BWANA YESU Kukuondolea. Jina La YESU Lina Nguvu Zaidi Ya Laana Zote,Yeye Alikuja Ili Azivunje Kazi Zote Za Shetani 1 Yohana 3:8b ''
Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. ''.

Kimbilia Kwake Wewe Unayeteswa Na Mzigo Wa Laana na utawekwa huru sawasawa na Mathayo 11:28 ambapo BWANA YESU anasema  ''Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. ''. 
MUNGU Akubariki

 SIRI YA MIZIMU NA ROHO ZA UKOO PIA MADHARA MIZIMU NA ROHO ZA UKOO.

Kila Ukoo Una Mizimu Yake Na Maroho Yake Ya Ukoo.
Mizimu Hii Na Maroho Haya Ya Ukoo Ni Watenda Kazi Wa Shetani, Mizimu Huwa Haifi Maana Ni Kundi La Malaika Waasi Waliofukuzwa Mbinguni Pamoja Na lucifer(shetani).

Mizimu Kwenye Ukoo Wenu Zina Kazi 3.

-Kwanza Mizimu Huhakikisha Kila Jambo Baya La Ukoo Wako Lililowapata Babu Zako Tangu Vizazi Vingi Nyuma linakupata na wewe , Kama Kuna Magonjwa Yaliwasumbua Babu Zako Lazima Yakupate Na Wewe, Kama Ukoo Wenu Huwa Hawafungi Ndoa Takatifu Na Wewe Itakua Hivyo Hivyo, Na Kila Lolote La Kishetani La Kiukoo Lazima Likupate Na Wewe.

-Kazi Ya Pili Ya 2 Ya Hizi Roho Za Shetani Kwenye Ukoo Wako, Mizimu Ni Walinzi, Sio Walinzi Wa Uzima Wako Bali Wanakulinda Na Kuhakikisha Hufanyi Lolote Ambalo shetani Hajakupangia. Na Kumbuka Kwamba shetani Hajawahi Kukupangia Jambo Jema Hata Siku Moja. Kuna watu leo akishika tu Biblia na kuanza kusoma usingizi unampata hiyo ni mizimu inakuzuia, kuna watu leo ukiwaambia twende kanisani anakuambia mwili umekua mzito ghafla hivyo labda siku nyingine mizimu hapo inamzuia.

-Na Kazi Ya 3 Ya Mizimu Kwako Ni Watoaji Taarifa kuzimu Na Wapeleka Taarifa Zako Kuzimu. Ukipanga jambo lolote jema na la kimungu lazima utaona ugumu maana kabala hujaanza kutenda taarifa zako zimeshafika kuzimu na zinatendewa kazi kinyume na mipango yako. Dawa Ya Kuwaondoa Mizimu Na Roho Za Ukoo Ni Kumpa YESU KRISTO Maisha Yako, Yohana 8:36 Inasema ''Mwana wa MUNGU akikuweka huru , utakuwa huru kweli kweli,'' Na uzuri wa MUNGU ni kwamba ametoa jina la YESU KRISTO ili kila aombaye awekwe huru kama inavyosema Yohana 14:13 ''
Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. ''

Ndugu jitenge leo na roho hizi za ukoo na mizimu ya ukoo kwa maombi ya vita kupitia jina la YESU KRISTO. Usikubali kuongozwa na mizimu na mapepo ya ukoo maana ukiongozwa na mizimu lazima utaishia tu kuzimu. Mizimu ni kiza kimbilia leo kwenye nuru ambayo ni BWANA YESU.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments