Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) linaloongozwa
na Askofu Mkuu, Zachary Kakobe limesherekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwake
mwaka 1989 leo kwa maandamano.
Sherehe hizo zilihudhuriwa
na waumini zaidi ya 5,000 kutoka mikoa na
wilaya mbalimbali za Tanzania na maandamano hayo yalianzia Viwanja vya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mpaka makao makuu ya kanisa hilo Barabara
ya Sam Nujoma.
Kwaya ya FGBF Mwika Moshi na pozi la picha
Askofu Kakobe na baadhi ya wachungaji wakiwasili kanisani
Askofu Kakobe akizungumza na waandishi wa habari
Comments