KANISA LA UFUFUO NA UZIMA LEO KUIZINDUA HELIKOPTA YA KUHUBILIA INJILI .


Kila jambo ukipanga na ukafuatilia matokeo yake mara nyingi huwa chanya. helikopta - imewasili rasmi katika kanisa la Gwajima baada ya kujibiwa maombi yao na juhudi zao zimeleta matunda. Helikopta hiyo ambayo inasemekana itatumika kama chombo cha angani katika kuhubiri Injili ya Yesu Kristo na kufika sehemu zisizofikika. Na kufuatia hilo sasa kanisa la Utukufu wa Yesu, Glory of Christ Church Tanzania, ama kwa jina maarufu Ufufuo na Uzima chini ya Mchungaji Kiongozi, Askofu Josephat Gwajima, watakuwa na ibada ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya kuwafanikisha kwenye jambo hilo.
Mungu awabariki wote walioshiriki kubeba maono ya Mtumishi wa Mungu Gwajima

Comments