KIJANA KATIKA KUELEKEA NDOA TAKATIFU.

BWANA YESU asifiwe.
karibu tujifunze
Waebrania 13:4 ''  Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.''

Ndugu Una Jambo La Kufanya Kwa Ajili Ya Kutimiza Hatima Ya Maisha Yako. Tatizo Wala Haliko Kwa MUNGU, tatizo liko kwako . Kwa Kila Msichana Au Mvulana Hapa Chini Ya Jua, MUNGU Amemwekea Mwanaume/mwanamke Wa Kufunga Nae Ndoa. shetani Anaweza Kutumia Kigezo Cha Ubaya Wa Sura Kwa Njia Ya Muonekano Lakini Habari Njema Ni Kwamba MUNGU Amekupa Nguvu Na Mamlaka Ya Kumfunga shetani Na Malaika Zake Na Kumtupilia Mbali Na Maisha Yako Kupitia Jina La YESU KRISTO. 
 ''Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali Mwanamke amchaye BWANA , Ndiye atakayesifiwa.'' Mithali 31:30.

Hata Hivyo Kigezo Cha Uzuri Au Urembo Hakiangaliwi Sana Siku Hizi Kuna Mifano Halisi Inaonyesha Wanaume Zaidi Ya 2 Wakimgombea Msichana Ambaye Wala Sura Yake Haivutii, Pia Siku Hizi Wasichana Wengi Warembo Kupindukia Wanajikuta Umri Unasonga Pasipo Kuolewa. Unaweza Ukavutia Kwa Nje Lakini Vijana Wengi Wa Kike Na Wa Kiume Huangalia Uzuri Wa Rohoni Na Tabia. 

Ushauri Wangu Ndugu Ambaye Ni Msichana Hakikisha Unamkanyaga shetani Ili Asikufanye Wakaka Wakuone Wewe Sio Mwanamke Wa Kuoa Bali Kuchezea Na Pia Kijana Wa Kiume Mpinge Shetani Ili Wadada Wasidhani Wewe Wa Kuwaoa Bali wa Kuchunwa tu.

 Sauti Inayokuijia Ili Kukushinikiza Kufanya Mabaya Ni Sauti Ya shetani Na Sio Sauti Ya MUNGU. Ikitokea Tu Sauti Hiyo Ikemee Ife Kwa Jina La YESU KRISTO. Muombe BWANA Ili Akupe Nguvu Ili Usije Ukaitii Sauti Ya shetani Maisha Yako Yote.

 Kijana Unaweza Ukajiaanda Ili Uoe Au Kuolewa Kwa Wakati Muafaka. Tatizo Likawa Chaguo Maana Kila Atakayetaka Kukuchumbia Wewe Unamkataa Kwa Kigezo Cha Kidunia Kabisa Kwamba Huyu Ana Mambo Ya Kizamani, Sio Kama Vijana Wa Kisasa Ambao Tunaweza Kutoka Out. Wengine Wameokoka Na Wamemuomba MUNGU Awape Mme Au Mke Mwema, Na MUNGU Amewapa Lakini Wao Wanamkataa Yule Ambaye Ni Chaguo La MUNGU. Hiyo Itapelekea Kuoa Au Kuolewa Na Mtu Ambaye Ana Ucha MUNGU Wa Muda Na Baadae Anaweza Kugeuka Tanzi Kwako Hata Uzima Wamilele Ukawa Mtihani Kwako Kuingia. 

Lakini Ndugu Unaweza Kumsimamisha shetani Sasa Ili Asiendelee Kuchelewesha Ndoa Yako. Unaweza Pia Kumilki Milki Yako Huku Ukipangua Vikwazo Na Kuomba Ili Ukutanishwe Na Mume/mke Wako Mtarajiwa. MUNGU Hatakua Na Njia Nyingine Zaidi Ya Kukuongoza Kuelekea Mahali Mke/mme Wako Alipo. Sasa Ni Wakati Wa Kupata Baraka Za Ndoa Kwa Jina La YESU KRISTO. 
 1 Kor 6:18 '' Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.''
Kataa Dhambi Ya Uasherati, Ikimbie Dhambi Hii, Ogopa Dhambi Hii Na Ikemee Dhambi Hii Ya Uasherati. Ni Heri Kuoa Kuliko Kuwaka Tamaa
 Kutoka 20:14 ''Usizini.''
 Kama Kuna Jambo Baya Sana Ambalo Anajifanyia Mwenyewe Kijana Wa Kiume Au Kijana Wa Kike Ni Kuishi Katika Tamaa Za Mwili Huku Akidai Ameokoka Huku Pia Akitarajia Kuoa Au Kuolewa Na Kijana Aliyezaliwa Mara Ya Pili.

Ewe Msichana Uliyempokea YESU Kuwa BWANA Na MWOKOZI Wa Maisha Yako, Sikia Siri Hii; 

 Mke Mwema siku zote anatoka kwa BWANA na mme mwema siku zotye hutoka kwa BWANA tu.

Kujituma Kwako Katika Kazi Ya Kanisa Pamoja Na Mipango Ya Kanisa, Kutatoa Fursa Nzuri Kwa Waoaji Kukuona. Kila Kijana Akitaka Kuoa Atazingatia Kwanza Na Kuwaza Msichana Bora Wa Kanisani Kabla Ya Kuwafikiria Wengine Wa Kutoka Nje. 

Maisha Yako Ya Kikristo Yana Nguvu Sana Na Hatimaye Kufanyika Msaada Kwako Kama Kivutio Kwa Mmeo Mtarajiwa. 
1 Kor 5:9 '' msichangamane na wazinzi.''
MATATIZO 16 Ambayo Nayaona Kwa Mabinti Makanisani, Na Matatizo Kuwachelewesha Kuolewa Ni 
-Wivu Kwa Wasichana Wenzao Wanaopata Wachumba, 
-Umbea Nao Ni Kikwazo, 
-Masengenyo Ni Kizuizi Cha Kuolewa, 
-Kukaa Barazani Pa Wenye Mizaha, 
-Tamaa Ya Pesa, 
-Kujitenga Na Mabinti Wenzao Kanisani, 
-Kujiinua Na Kuwadharau Wasichana Wenzao Kanisani Kisa Tu Wao Wanasifiwa Wakiimba, 
-Kujifanya Matawi Ya Juu, 
-Kuwa Na Urafiki Na Watu Wabaya, 
-Kutokuwa Na Ukarimu Kwa Wageni Kanisani,
- Kuvaa Mawigi, 
-Kutokuwa Wanamaombi, 
-Kutojitunza, 
-Kutokuwa Wasiri, 
-Kuvaa Nguo Fupi 
-Na Dhambi.

 MUNGU Awasaidie Mabinti Na Kuwafanikisha Kuolewa.

''Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani'' Mithali 31:10

 Kila Kijana Aliye Ndani Ya KRISTO Anapenda Kumuoa Binti Ambaye Anathibitisha Imani Yake Kwa Dhati Kimatendo Na Kumridhisha. Hakuna Mtu Anayetaka Kuishi Kama Kuzimu Na Kila Mmoja Anatarajia Maisha Yenye Furaha Katika Ndoa Anayoiendea. Ngoja Nikupe Siri Hii; Kuna Ndoa Nyingi Sana Zisizohesabika Ambazo Zimetokana Na Ushauri Au Ushawishi Wa Wachungaji Au Ndugu Wa Kiroho. Na Jambo Hilo Linaweza Kufanikiwa Endapo Msichana Husika Atakuwa Ni Mtu Wa Kujituma Kwenye Mambo Ya MUNGU Na Ni Mwaminifu, Biblia Inasema Katika Mathayo 5:14 Kwamba " Ninyi Ni Nuru Ya Ulimwengu. Mji Hauwezi Kusitirika Ukiwa Juu Ya Mlima"

Hivyo Kuna Baadhi Ya Wachungaji Wakiombwa Ushauri Hupendekeza Fulani Aolewe Na Mmoja Wa Vijana Aliyefika Kwake Kuomba Ushauri, Ni Kwa Sababu Ya Tabia Njema Ya Msichana. Binti Weka Wazi Imani Yako, Amua Kuwa Muumini Moto Na Sio Baridi. Hii Ni Hatua Ya Nzuri Itakayokuwezesha Kupata Kibali Na Mvuto Kutoka Kwa Akina Kaka Ambao Wataongozwa Na Sifa Zako Kuleta Posa Kwako. YESU Anawapenda Sana Wasichana. Ubarikiwe.
 
 ''Rafiki hupenda siku zote'' Mithali 17:17a
Kwa Wadada:MAOMBI KWA AJILI YA KUTAFUTA MATAKWA YA MUNGU KWENYE NDOA YAKO IJAYO.

Mwongozo Wako Wa Maombi, ni Mithali 18:2, Isaya 55:6, Yeremia 33:3 Na Zaburi 25:14.

JEHOVAH MUNGU, Muumba Wa Mbingu Na Nchi, Ninasema Asante Kwa Uzima Ulionipa, Utukuze Milele BWANA. BABA, Ninaleta Ombi La Kuchumbiwa Na Kijana Huyu(mtaje) Kwa Ajili Ya Ndoa, Mbele Ya Kiti Chako Cha Rehema Nikiomba Usema Nami BWANA. Naamini Kuwa Utatimiza Mapenzi Yako Kuhusu Ndoa Yangu, Nakuomba BWANA Usiruhusu Nifanye Makosa Katika Ndoa Yangu kwa Jina La YESU. Nifunulie Jambo Hili Kwa Ndoto, Maono, Ufunuo Au Kwa Namna Yeyote Ile, Mimi Niko Tayari Kukutii. Kama Sio Mapenzi Yako Kwa Mimi Kuolewa Na Kijana Huyu, Nikoseshe Amani Nikimuona Mahali Popote, Kama Ni Mpango Wako, Ruhusu Amani Na Furaha Yako, Nakuomba Pia BWANA Unisaidie Kutofautisha Kati Ya Upendo Na Tamaa Ya Mwili. Asante MUNGU Kwa Kunijibu Maombi Yangu. Ni katika jina la YESU KRISTO Nimeomba AMEN AMEN.
  Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments