KIZUNGUZUNGU YA ENOCK JONAS YAITIKISA IRINGA.


 
Mwimbaji Enock Jonas katika picha

 
Ni ujio mpya wa mwimbaji wa nyimbo za injili tanzania Enock Jonas  umewabariki  wakazi wa nyanda za juu kusini baaada ya kuja na albamu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wakazi hao.
 
Akizungumza nasi mmoja kati ya wakazi wa Iringa aliyenaswa  akinunua nakala ya albamu hiyo ya KIZUNGUZUNGU amesema amevutiwa sana na uimbaji wa mwimbaji huyo huku akimsifia kuwa anatazama wakati tulio nao maana watu wengi  hawaamini kuwa YESU KRISTO  ni mtaji anaweza kuwatajirisha.
 
 Ndani ya albamu hiyo utakutana na nyimbo kali kama vile YESU ni mtaji ,nipe mdundo, kizunguzungu na wimbo ambao watu wengi wapendezewa sana nao unaitwa ninafuta maneno yenu

Comments