KUKATAA UAGUZI, UGANGA WA KIENYEJI NA UCHAWI.

BWANA YESU asifiwe ndugu.
Karibu tujifunze.
Walawi 19:26-28 ''Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi. Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu. Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA. ''
 MUNGU anaagiza mambo haya kwa wote wampendao unajua ni kwanini? ni kwa sababu hawa waganga wa kienyeji, wachawi ni mawakala wa shetani.
Najua katika jamii nyingi za kiafrika ni nadra sana kukuta mtu hana chale kwenye mwili wake. nakumbuka mwaka 1992 tulichanjwa chale familia nzima na kisha kuoga maji yaliyochemshwa kwa majani fulani ya miti katikati ya uwanja wa nyumbani kabla jua halijachomoza, nilikuwa nina miaka 6 na sikuweza kuhoji zaidi tu ya kuumia kwa sababu ya chale za mganga  aliyekuja nyumbani kufanya jambo hilo, tuliambiwa kwamba dawa ya huyo mganga itafanya kazi kwa miaka 10 hivyo mwaka 2002 ilikuwa ni awamu ya pili kuchanjwa ndipo nilipokataa maana kwa miaka 10 iliyopita kama ni kukabwa na majinamizi nilikabwa, kama ni kuumwa niliumwa, kama ni kutishwa na wachawi nilitishwa sana. Nikagundua aliyekuwa ananilinda kwa miaka hiyo 10 ni MUNGU wa mbinguni na sio mungu wa dunia hii maana hata mganga yule aliyetuchanja chale mwanzo alikuwa amekufa, na hata waganga maarufu ambao hata waliitwa mungu wa pili walikuwa na wao wamekufa. Namshukuru MUNGU siku moja nikiwa nimeshaokoka, nilipata ufunuo kwamba nifute maagano yote ya kipepo kupitia zile chale, nifute kazi zote za zile chale kwa damu ya YESU KRISTO na hakika zilifutika maana hadi niliona ishara ya kufutika kwa ushetani huo. Ndugu zangu mlinzi wetu ni MUNGU tu na sio vinginevyo.

Kwa yule uliyeokoka na katika ukoo wenu una waganga wa kienyeji wengi naamini utakuwa unanielewa vizuri sana jinsi ambavyo ugumu unaokuwa unauona katika maombi na mambo mengine ya kiroho.Neno hapo juu linasema
-Msiroge.
-Achana na utambuzi wa mapepo.
-Msichanjwe chale.
-Msichanje chale.
-Msifanye mazindiko yeyote kwa ajili ya watu.
-Msijiwekee alama yeyote katika miili yenu.
Ndugu yangu kama MUNGU amekukataza jambo mtii yeye na kama amekataa uganga na wewe ukatae vilevile maana uganga huo ni kazi ya shetani.
Kataa Aina Zote Za Uaguzi, Kataa Uganga Wa Kienyeji, Kataa Unajimu, Kataa Usoma Bao, Kataa Usoma Nyota, Kataa Usangoma, Kataa Usihiri Na Kila Aina Ya Uaguzi Maana Ni Machukizo Kwa BWANA MUNGU Wako. Biblia Katika Isaya 8:19 Inasema " Na Wakati Watakapokuambia, Tafuta Habari Kwa Watu Wenye Pepo Na Kwa Wachawi; Waliao Kama Ndege Na Kunong'ona; Je! Haiwapasi Watu Kutafuta Habari Kwa MUNGU Wao?. 
Je Haitupasi Mimi Na Wewe Unayesoma Ujumbe Huu Kutafuta Habari Ya Jambo Lolote Kwa BWANA MUNGU Wetu? 
Kwanini Kutafuta Msaada Kwa Wafanyakazi Wa shetani? Ndugu Zangu shetani Ni shetani Tu Hata Kama Atakuja Kwa Wema Lakini Ni shetani Na Atakalolifanya Ni La Kishetani Tu Hata Kama Litakua Jema Machoni Pako. Dada Mmoja Alikua Hazai, Na Kwa Hofu Ya Kuachwa Na Mmewe Akaona Aende Kwa Mganga Ili Kupata Mtoto, Mganga Akamchukua Na Kumpeleka Makaburini, Walipofika Mganga Akaita Mara Kaburi 1 Likafumuka Likatokea Li Mzimu Ndani Ya Kaburi Na Kumwingilia Kingono Yule Dada Hadi Kuzimia. ni mambo ya aibu na fedheha kubwa sana. Ndugu Zangu MUNGU Akikataa Jambo Heri Kuacha maana ni madhara kwako ukiling'ang'ania jambo hilo na hasara kubwa zaidi ya kulifuata jambo hilo ambalo MUNGU kupitia Biblia amelikataza ni jehanamu ya moto.

 Juzi Juzi Tumesikia Kwenye Vyombo Vya Habari Jinsi Waganga Wa Kienyeji Dar Es Salaam Walivyokuwa Wakifanya Mapenzi Na Wateja Wao Ili Tu Wapate Uwezo Wa Kutunga Mimba. Jiulize wamama kama hao zaidi ya ishirini wanaamua kuuza utu wao na kufuta thamani za ndoa zao kwa kudanganywa na waganga wa kienyeji. Ndugu zangu waganga na wachawi ni jamii moja, mganga lazima awe mchawi vilevile na wote wanatumia mizimu na majini katika utendaji wao wa kazi.

Ndugu Zangu Ni Heri Kumtii MUNGU Na Sio shetani. Wafanyakazi Wakubwa Wa shetani Ni Waganga Wa Kienyeji, Wachawi, Mizimu Na Majini Lakini Wanadamu Wengi Bado Wanaenda Kwa Waganga Wa Kienyeji. 
 Katika Ezekieli 21:21 Biblia Inasema Juu Ya Mfalme Mjinga Kwamba " Maana Mfalme Wa Babeli Alisimama Penye Njia Panda, Penye Kichwa Cha Njia Hizo Mbili, Ili Atumie Uganga; Aliitikisa Mishale Huko Na Huko, Akaziuliza Terafi, Akayatazama Maini." 
 Ndugu Yangu Kataa Kwa Namna Yeyote Kwenda Kwa Waganga Wa Kienyeji. Kataa Kuagua. Teketeza Roho Za Uaguzi Kwa Jina La YESU KRISTO. Mfalme Huyu Wa Babeli Alitumia Viungo Vya Binadamu, Mishale Na Sanamu Katika Uganga. Wapo Watu Wengi Kwa Sababu Ndugu Zao Au Wazazi Wao Ni Waganga Wa Kienyeji Na Hiyo Imepelekea Na Wao Kuingia Maagano Na Mashetani. Ndugu Yangu YESU KRISTO Anatosha, shetani Wa Nini?.Mkatae shetani Na Kazi Zake.

 Ndugu Zangu Tuache Dhambi, Tuogope Dhambi Na Tukimbie Dhambi. Mambo Hayo 3 Inatakiwa Kila Mtu Ayaweke Moyoni Mwake.
 ''Na Hao Waonaji Watatahayarika, Na Wenye Kubashiri Watafadhaika;... Kwa Maana Hapana Jawabu La MUNGU-3:7.
 Ndugu Zangu MUNGU Atupe Neema Ili Tuendelee Kukaa Kwenye Uwepo Wake Siku Zote Za Maisha Yetu. Kataa Kila Kazi Za Shetani Zikiwemo, Uganga Wa Kienyeji Na Uchawi.

 Ndugu Endelea Kulishika Tumaini Maana Aliyeahidi Ambaye Ni BWANA YESU Ni Mwaminifu Milele Yote. achana na msaada feki wa wafanga wa kienyeji.


Kujihusisha Na Uganga Wa Kienyeji Na Uchawi Ni Mbaya Sana. Mfalme Sauli Akufa Kwa Sababu Ya Kutaka Msaada Kwa Waganga Wa Kienyeji. Biblia Inasema Hivi Katika 1 Nyakati 10:13-14 " Basi Sauli Alikufa Kwa Sababu Ya Kosa Lake Alilomkosa BWANA, Kwa Sababu Ya Neno La BWANA, Asilolishika; Na Tena Kwa Kutaka Shauri Kwa Wenye Pepo Wa Utambuzi, Aulize Kwake, Asiulize Kwa BWANA."  


Sauli Alikuwa Mtumishi Wa MUNGU Kama Wewe Ulivyo Lakini shetani Alimteka Na Kusababisha Kumwasi MUNGU Kwa Kwenda Kwa Waganga Wa Kienyeji Au Kwa Jina Jingine Kwa Wenye Mapepo Ya Utambuzi. Ndugu Yangu Hata Kama Una Shida Kubwa Kiasi Gani Usikubali Shida Hiyo Ikupeleke Kwa Mganga, Hata Kama Unahitaji Jambo Muhimu Kiasi Gani Usikubali Kutaka Msaada Kwa Waganga Wa Kienyeji. Mtake BWANA YESU Na Nguvu Zake Naye Atakuponya Na Atakuokoa Na Kila Aina Ya Kusudi La Shetani. 1 Yohana 3:8b Biblia Inasema " Kwa Kusudi Hili Mwana Wa MUNGU Alidhihilishwa Ili Azivunje Kazi Zote Za Shetani.''  Matatizo Yako Yatavunjika, Magonjwa Yako Yatavunjika Na Utakuwa Huru kwa jina la YESU KRISTO aliye hai..

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292 

                     mabula1986@gmail.com
                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
 MUNGU Akubariki.

Comments