KUNA UHURU SAHIHI NDANI YA YESU KRISTO.

BWANA YESU asifiwe!
Karibu tujifunze jinsi ya kuwa huru na kuulinda uhuru .

Mataifa karibu yote ya kiafrika yalitawaliwa na wakoloni. Ni Ethiopia na Liberia tu ndizo hazikutawaliwa baada ya mkutano mkuu wa Berlin wa mwaka 1884, Hata Misri ilitawaliwa japokuwa kwa  muda mfupi. Mataifa mengine yote yalikuwa wanatawaliwa na wakoloni lakini ulifika muda wa kuwa huru baada ya utumwa na mateso ya miaka mingi. Uhuru huu ni uhuru kamili lakini baada ya uhuru huo kuna ukoloni mamboleo unafuata. ujumbe wangu leo unazungumzia uhuru au kuwa huru na uhuru huu ninaouzungumzia hauna ukoloni mamboleo bali ni uhuru kabisa. Uhuru sahihi unatolewa na MUNGU katika KRISTO YESU pekee.

Yohana 8:36 ''Basi Mwana(YESU) akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.''

YESU Akikuweka Huru, Unakuwa Huru Kabisa. 

Ndugu Yangu nina swali kwako.
-Kwanini Kwenye Baadhi Ya Maeneo hujawa Huru? 
- Kwanini Uteswe Na Mapepo? 
-Kwanini Usumbuliwe Na Wachawi Na Mizimu? 
-Kwanini Tamaa Mbaya Ikuzonge?. 

Jibu ni kwamba Kuna Kitu Unapungukiwa.
 - Kama Hupungukiwi Maombi Basi Unapungukiwa Neno.
- Kama Hupungukiwi Mafunuo Basi Unapungukiwa Nguvu Za MUNGU Kwa Sababu Ya Matendo Yako. 
-Kama Hupungukiwi Nguvu Za ROHO MTAKATIFU Unapungukiwa Imani. 
-Kama Hupungukiwi Utakatifu Basi Unapungukiwa Kusoma Neno. 

  ''Lakini sasa mkiisha kuwekwa HURU, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa MUNGU, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA  wetu-Warumi 6:22'' 

Ndugu Angalia Ni Wapi Unapungukiwa Ili Utengeneza Na Uwe Huru Kwa Jina La YESU KRISTO. 
-Na Ukiwa Huru Wachawi Wakija Watakuta Malaika Wasio Na Idadi Kwako, 
-Kama Wakija Mapepo Watakuta Kuna Ukuta Wa Moto Ambao Hauna Mlango Wala Dirisha, 
-Wakija Mizimu Watakutana Na Viboko Vya Moto Visivyo Na Idadi. 
  ''Na mlipokwisha kuwekwa HURU mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.-Warumi 6:18''
Hakika YESU Akikuweka Huru Unakuwa Huru Kabisa. BWANA YESU Anakupenda Sana Na Muda Huu Anakuandalia Makao Mbinguni Yohana 14:1-18- YESU anasema ''Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini MUNGU, niaminini na mimi.  Nyumbani mwa BABA yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.  Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.  Nami niendako mwaijua njia.  Tomaso akamwambia, BWANA, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi.  Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. Filipo akamwambia, BWANA, utuonyeshe BABA, yatutosha. YESU akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona BABA; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe BABA? Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya BABA, na BABA yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini BABA akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya BABA, na BABA yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa BABA. Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba BABA, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye ROHO wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. )

Ukipendwa Na YESU ni bora kuliko vyote. BWANA YESU akukumbuke na kukupa uzima wake.

Ndugu unatakiwa uwe huru mbali na uonevu wa shetani. na uhuru huu MUNGU amekupa kupitia YESU KRISTO jambo la kufanya wewe ni kuitumia mamlaka ya KRISTO ambayo iko ndani yako kujiweka huru kwa maombi. Kama YESU hajaingia kwako basi mpe maisha yako leo na uhuru kamili utaupata tena uhuru wa milele.

 Mwenye Nyumba Hapigi Hodi.
 Mwanadamu Ni Nyumba, Inaweza Kuwa Nyumba Ya MUNGU Au Nyumba Ya shetani.  ukitaka kuwa huru basi shikamana na MUNGU wako katika KRISTO YESU.

Kama Wewe Umemruhusu shetani Akufanye Kuwa Nyumba Yake; Nakuhakikishia Muda Wowote shetani akitaka kuingia ataingia tu maana wewe ni nyumba yake, na shetani ni Mbaya Sana Na Aliowageuza Nyumba Yake Lazima Wakabwe Na Majinamizi Usiku, Lazima Waote Wanazikwa, Lazima Waamke Asubuhi Wakiwa Wamechoka Maana Wachawi Walikua Wakilia Nyama Za Watu Juu Ya Migongo Yao Usiku Wakiwa Wamelala. 

Ndugu Yangu YESU Akikuweka Huru, Utakuwa Huru Kabisa . 

Kuna Dada Mmoja Zamani Tukiwa Shule ya msingi  Ambaye Kwao Walikuwa Wachawi kabisa Maana Hata wao Walikuwa Wanajitangaza, Dada huyu Alituuliza Swali Kwamba " Nani Ambaye Baadhi Ya Siku Huamka Asubuhi Mdomo Wake Ukiwa Mchungu Sana?"  
Wengi Walinyoosha Mikono; Akasema "Ukiamka mdomo mchungu sana  Ujue Usiku Wachawi Walijisaidia haja ndogo kinywani mwako " Akasema Hata Yeye Amewahi kuwawekea  Mikojo Wengi, Siku Akienda Na Mama Yake Kuroga.
 Ndugu yangu ona ubaya huu wa shetani kwa wale ambao hawajawekwa huru na YESU, ona ubaya huu wa shetani kwa watu ambao shetani anawamiliki, ona ubaya huu wa shetani kwa watu ambao yeye shetani ni mkoloni kwao. YESU kwa upendo wake wa ajabu akaamua kuja ulimwenguni ili tu mimi na wewe tusiteswe tena na wachawi. na wachawi ni wabaya sana maana kama wanauwezo wa kula nyama za watu watashindwaje kujisaidia kinywani mwako? wana roho ya shetani, roho ambayo haina huruma na mwanadamu yeyote. Lakini BWANA YESU akasema kwenye kikao kule mbinguni kwamba ''Mimi hii sivumilii, Lazima niende nikawaokoe wanadamu na dhambi zao, lazima nikahakikishe wote watakaonifuata watakuwa huru tena huru kwelikweli''
 Ndugu Ndio Maana BWANA YESU Alikuja Ili Tusiwe Nyumba Ya shetani tena. Biblia inasema hivi katika 2 Kor 5:17 '' Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. ''

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292

mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments