
Kuwa
Rohoni ni kuwa na Daiolojia na Mungu. Daiolojia ni mazungumzo baina ya
pande mbili, nikimaanisha Mungu na Mwanadamu. Tuangalie daiolojia Agano
la Kale na Jipya.
A. AGANO LA KALE
Agano
la Kale Mungu alizungumza na Wanadamu kwa njia mbalimbali, Mgawanyo
wangu wa daiolojia na Mungu nimeugawanya kwa kuzingatia idadi ya
wahusika.
1. Moja kwa moja na mtu binafsi (wachache)
a. Ndoto – Danieli 2:19
b. Maono – Ezekieli 1:1
c.Ana kwa ana – Kutoka 33:11, Hesabu 12:7-8
2. Kupitia Mtu mwingine(wengi)
a. Kuhani (Urim, Thumimu na Naivera) – Kutoka 28:30-31,1 Samweli 28:6
b. Unabii – Kumbu Torati 18:18
3. Kupitia Kitu(Kiumbe) kingine
a. Punda – Hesabu 22:28
b. Samaki – Yona 2:10
c.Kiganja – Danieli 5:5-6
d. Malaika – Kutoka 33:2a
B. AGANO JIPYA
Agano
Jipya Mungu ameboresha Daiolojia, ni kinyume cha Agano la Kale. Lakini
bahati mbay wahusika wa Agano Jipya hawapo makini ukilinganisha na wale
wa Agano la Kale.
1. Moja kwa moja na Mtu binafsi (wengi)
a. Yesu – Ebrania 1:1-2
b. Roho Mtakatifu – Ufunuo 2:7, Matendo 13:2
c. Kuwa Rohoni – Ufunuo 1:10
2. Kupitia Mtu mwingine(wachache)
a. Nabii – Matendo 11:27-28
b. Malaika – Matendo 10:3-4
C. KIZAZI KIPYA -- Zaburi 24:6
-Pamoja
na njia zote nilizozitaja hapo juu,bado Mungu anaweza akazungumza na
Mwanadamu kwa njia yoyoyte na kaktumia chochote. Mungu hana mipaka, vitu
vyote ni watumishi wake.
Njia
zote za Mwanadamu kuongea na Mungu au Mungu kuongea na Mwanadamu ni
nzuri lakini iliyo bora kuliko zote ni kuongea kwa kupitia Yesu kwa njia
ya Roho Mtakatifu, wewe utatakiwa kuwa rohoni ili uwe na Daiolojia.
Ungependa kuwa rohoni?
Comments