KWA WADADA: OMBA MAOMBI HAYA YA KUMFANYA MMEO ATOKEE



BWANA YESU Asifiwe,

Kila Eva Ana Adamu Wake, Hata Wewe Mmeo Yupo Tu Na Ni Haki Yako Kutoka Kwa MUNGU. MUNGU Akupe Mme Wako Baada Ya Maombi Haya, Tubu Kwanza Kisha Anza Kuomba. Muongozo Ni Isaya 45:1-3, Zaburi 37:23 Na Wafilipi 1:6.

Twende.

BWANA Wangu Na MUNGU Wangu, Naja Kwako Kama Nilivyo. Pokea Utukufu Wote Na Heshima Katika Jina La YESU. BWANA Nayaleta Maisha Yangu Yote Mikononi Mwako, Naomba Uje Ufanye Sawasawa Na Mapenzi Yako Katika Jina La YESU. Naileta Ndoa Yangu Ijayo Katika Mkono Wako Wa Uweza, BWANA Nakuomba Na Ninaamini Kuwa, Utasababisha Mume Wangu Kujidhihirisha Na Kutokea Mbele Yangu Kwa Jina La YESU KRISTO. Popote Alipo, Nakuomba Na Kuamini Kuwa Atakuja Na Kuleta Posa Kwangu Kwa Jina La YESU KRISTO. Mahali Popote Alipo Mume Wangu, Nakuomba BWANA Umlinde, Na Umpe Ustawi Na Umfanye Ajidhihirishe Kwangu Kwa Jina La YESU KRISTO. Namfungua Mume Wangu Kutoka Kutoka Katika Nguvu Za Giza.
Namfungua Mume Wangu Kutoka Katika Nguvu Za Giza Zinazomzuilia Kuambatana Na Mimi Na Kushindwa Kunitamkia, Katika Jila La YESU. BWANA, Nakuomba Unipe Taraja La Moyo Wangu Sawasawa Na Mithali 10:24, Na Unipe Mume Atakayenipenda Na Kunitunza Katika Jina La YESU KRISTO. Katika Jina La YESU KRISTO, Namfungua Mume Wangu Kutoka Pande Zote Nne Za Dunia. Dhihirisha Ahadi Hii Kwa Muda Muafaka Katika Jina La YESU. Naamuru Kufunguliwa Kutoka Katika Kifungo Cha Kukosa Pesa Au Matatizo Mengine Yanayomzuilia, Katika Jina La YESU KRISTO. BWANA, Nakuomba Na Kuamini Kuwa Utanifunulia Mwenzi Wangu Wa Maisha Na Kumfanya Anitafute Kwa Nguvu Zote Katika Jina La YESU KRISTO. BWANA, Waruhusu Malaika Wako Waniletee Mume Wangu Popote Alipo Katika Jina La YESU KRISTO. Amen. Na Kila Nguvu Ya Giza Inayosababisha Kuchelewesha Ndoa Naiharibu Na Ninaidhoofisha Na Kuivuma Mamlaka Kwa Jina La YESU KRISTO. Asante BABA Wa Mbinguni Kwa Kuwa Yametimia Katika Jina La YESU KRISTO, 

 AMEN. 

Ubarikiwe Sana Na BWANA YESU Aliye Hai.

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292

mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments