LIANGALIE TATIZO LAKO KWA JICHO LA KIMUNGU.



1Samwel 17:40-47.
Na MP Paul Ufufuo na Uzima Moshi,

“..... akajichagulia mawe laini matano katika kijito cha maji, akayatia katika mfuko wa kichungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake, na kombeo lake alikuwa nalo mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti. Huyo Mfilisti naye akamsogelea Daudi na kumkaribia; na mtu yule aliyemchukulia ngao yake akamtangulia. Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri. Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake. Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni. Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli. Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.”

Kulikuwa na vita kati ya Wafilisti na Israel na wafilisti wakataka mtu mmoja atakayeweza kupigana na shujaa wao Goliath badala ya kuingia vitani na kuwauwa watu wasio na hatia. Israel wakiongonzwa na Sauli mfalme wao waliogopa na hawakutoa mtu wa kupigana na Goliath. Siku moja Mzee Yese akamtuma mwanawe Daudi kuwapelekea wanawe wakubwa waliokuwepo vitani na Sauli na Daudi aliposikia Mfilisti Goliath tena asiyetahiriwa anayatukana majeshi ya Bwana hakupendezwa na akaamua kuchukua hatua za kujua kwani majeshi ya Bwana kutukanwa na hata walipomwambia kuna Goliath mtu wa vita tangu ujana wake hakuogopa, akamwangalia goliath kwa jicho la Ki-Mungu akamwona mdogo akaenda kwa Mfalme Sauli, akampa CV yake iliyojaa habari za ushujaa na ushindi uliotokana na kuangalia matatizo kwa jicho la kiungu.
Hatimaye sauli alipomruhusu akapigane, alipokuwa akienda aliokota mawe laini matatu yaaani alimwona Goliath kama tatizo dogo na akamwambia wewe wanijia kwa upanga, na fumo, na mkuki lakini mimi ninakujia kwa jina la Bwana wa majeshi uliyoyatukana.
Watu wakisikiliza ujumbe

Haijalishi una tatizo lenye jina kubwa kiasi gani, limrkuwepo kwa mda gani, ugonjwa ulionao una jina kubwa kiasi gani, wanaokuonea wana cheo gani wewe waendee kwa jina la Bwana Yesu akaaye ndani yako nawe upoke ushindi wako.

Daudi hakuangalia ukubwa wa goliath na vitisho vyake, nawe leo tumia jina la Yesu kuondoa kila tatizo linalokusumbua iwe ni kansa, ukimwi, kufirisika na kila kitu kinachokutatiza.
Baada ya majibizano ya muda Goliati akaanza kumfuata Daudi naye Daudi akamfuata akizungusha kombeo lake kumwelekea Goliath na ndivyo ilivyo kwako ufanyaye bidii kwenda kanisani kwamwabudu Mungu, bidii yako katika kuomba, kusoma neno na kumtumikia Mungu kwa namna mbalimbali.

Unahitaji jambo moja tuu tumia jina la Yesu uliyenaye, kwa kupigwa kwake tumepona, Goliath alibeba upanga na daudi aliutumia huohuo kumkata kichwa.

Yageuze mabaya waliyokunuwizia yawapate wenyewe, silaha zao walizoziandaa kutuharibu na zirudi kwao wenyewe, mashimo waliyoyachimba watumbukie wenyewe, na mitego yao iwanase wenyewe katika jina la Yesu Kristo wan a Nazareth.


Yesu anasema “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” yaani haijalishi ni mzigo mgubwa kiasi gani Yesu ni jina kuu lipitalo majina Yote, na chukulia kwa mfano tuu wewe ni Tingatinga na mbele yako kuna tatizo bajaji je utaogopa kwamba usalama wako uko hatarini au bajaji ndo yenye kuogopa? Mfano mwingine ni chukulia wewe ni Train na mbele yako kuna umbwa utaogopa kwamba umbwa atakuharibu au kwamba wewe ndiye mwenye kumdhuru kwa kuondoa kabisa uhai wake?

Umembeba Yesu ambaye ni zaidi ya Tingatinga na Train kwa ulinganifu wa tatizo kama mnyama umbwa, leo angusha tatizo lako kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth na ubaki huru na aliyebarikiwa. Amen

Comments