MAPITO

Na Frank Philip


"Basi BWANA aliwapa Israeli nchi hiyo yote, ambayo aliapa kwamba atawapa baba zao; nao wakaimiliki, na kukaa mumo. Kisha BWANA akawapa raha pande zote, sawasawa na hayo yote aliyokuwa amewaapia baba zao; wala katika adui zao wote hakusimama hata mtu mmoja miongoni mwao mbele zao; yeye BWANA akawatia adui zao wote mikononi mwao. Halikuanguka neno lo lote katika jambo lo lote lililokuwa ni jema ambalo BWANA alikuwa amelinena katika habari ya nyumba ya Israeli; yalitimia mambo yote" (Yoshua 21: 43-45).

Uzuri wa kujua Neno la Mungu alilosema kwa familia yako, nchi yako, watoto wako au wewe mwenyewe, nk. ni kwamba UKILING'ANG'ANIA na kusimama nalo kwa uaminifu, haijalishi MAPITO utakayopitia, MWISHONI, kila jambo Alilosema BWANA hutokea. Tatizo ni pale ambapo hujui NJIA wala UNAKOKWENDA.

Mungu atupe NURU tujue njia zetu na MIISHO yetu ili tupate hekima ya kutembea Naye, na kujua kutenda au kunena kama itupasavyo; lakini pia tupate FARAJA tupitiapo magumu ya maisha.

Frank Philip.

Comments