NA MCHUNGAJI KIONGOZI: JOSEPHAT GWAJIMA,Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe |
I.
UTANGULIZI
Asante Mungu kwa ajili ya uwepo wako mahali hapa, Mungu
katika jina la Yesu uinuliwe Mungu wetu katika dunia yote kwa maana wewe ni mkuu
kuliko miungu yote, na leo utaenda kujitukuza
katikati yetu na kutufunulia yale yote ambayo shetani ameyatenda katika maisha yetu, leo bwana utaenda kutufunulia
uzao wa mashetani ulioko katikati ya
wanadamu na Mungu wetu kwa jina la Yesu utaenda kutufungua na kutuweka huru na
uzao wa mashetani.
II.
SOMO
Mwanzo 3:15,
15 nami nitaweka uadui kati yako na
huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na
wewe utamponda kisigino.
Mungu anatuonyesha kuwa kuna uzao wa aina
mbili:-
1.Uzao wa mwanamke – ni wale waliozaliwa na mwanamke kama wewe na
mimi, maana yake wale wanaomfuata Yesu
maana Yesu naye ni uzao wa mwanamke.
2.Uzao wa nyoka- wazao
wa nyoka ni wale wanaomfuata shetani,
Mathayo 23:29-33,
33 Enyi nyoka, wana wa majoka,
mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?
Utaona Yesu alipokuwa anaongea na watu
wabishi wa neno lake aliwaita nyoka wana wa majoka, Yesu aliwaona kwa ndani
kwamba siyo watu ingawa kwa jinsi ya mwili wanaonekana wanadamu kumbe siyo
wanadamu ila wamejichanganya katikati ya wanadamu. Leo kwa jina la Yesu
tunaenda kuyachambua majoka yote yaliyojichanganya kwa wanadamu , yale
yaliyoingia na kuchuchukua nafasi mbalimbali katika tawala za serikali, yale
yaliyooa na kuolewa na wanadamu katika jina la Yesu.
Mathayo 3:7, Luka 3:17,Utaona
bwana Yesu anawaambia nani aliyewaambia kuikimbia hukumu ya bwana, Yesu alijua kuwa ni mashetani ingawa wamevaa miili hivyo hawaitaji kuokoka kwa maana walishahukumiwa.
Leo nakutangazia uzao wa nyoka uliokuletea matatizo katika familia yako, katika
biashara yako katika kazi yako leo watang’olewa katika jina la Yesu.
Mathayo 12:34,
34 Enyi
wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu
huyanena yaujazayo moyo wake.
Bwana Yesu anawaambia nyie majoka mwawezaje kunena mema kumbe ni waovu, majoka(mashetani)
waliovaa miili wanaweza kutenda au kunena mema
ili usiwatambue kusudi wakuvute na kukupata siyo kwamba
wanatenda mema kwako kwa uzuri maana asili ya shetani hawezi kutenda mema.
Mambo matatu muhimu yatakayotokea tunapoekelea katika ulimwengu huu ni :
1.
Shetani anahama kutoka katika ulimwengu wa roho
na kuhamia mwilini kwa kadiri ya Wakristo wanaotumia nguvu za Mungu wanapoongezeka,
watu wanaolitumia jina la Yesu wanapoongezeka, ndipo ufalme wa giza unapopigwa
sana katika ulimwengu wa roho unabomolewa, hivyo shetani anahamia mwilini ili kukwepa makombora ya walokole rohoni yasimpate. Nyakati hizi shetani
anaingia katika ulimwengu wa mwili na kufanya biashara , kuoa au kuolewa na
wanadamu, lakini leo kwa jina la Yesu tunawafuata mashetani huko huko mwilini walipo na kuwang’oa.
2.
Shetani anang’ang’ania ashikilie tawala za dunia, yaaani wanavaa
miili na kuwa viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali duniani kote ili
kumtengenezea mpinga kristo njia ili atakapokuja kutawala akute tayari tawala
zote zipo chini ya shetani. Katika jina la
Yesu lazima tuwarudishe kuzima walikotoka ili kwanza Tanzania na dunia nzima
waokolewe walio wake Yesu ili watu wa
Mungu watakapo kuwa tayari wamenyakuliwa wakati huo mpinga kristo atakapokuja
kutawala.Watu wa Mungu nawatangazia kujiingiza kwenye siasa ili wakati wa
uchaguzi angalau watu wamchague mwanadamu mwenzao kuliko kuchagua majoka ya
aina ya cobra na chatu yaliyovaa miili na kuomba kuchaguliwa katika nafasi
mbalimbali.
3.
Wakati mashetani wanahamia mwilini na kuwa
binadamu ili wachukue tawala za wanadamu . Mungu naye anafanya mpango wa
kuwaleta watu wa mbinguni katika ulimmwengu wa mwili. Malaika wanavaa miili ili
kupambana na uovu wa shetani , utaona uamsho usio wa kawaida maana watu wengi
wa mbinguni wamevaa miili na kupeleka injili ya Yesu kristo kwa kasi duniani
kote. Imeandikwa alitokea mtu ametumwa kutoka kwa Mungu,kumbe Mungu anaweza
kumtuma mtu wake na kuitenda kazi ya Mungu, utashangaa unamwona mtu ananena kwa lugha mpaka cheche zinatoka
anafungua watu walioonewa na ibilisi kwa
mamlaka ya jina la Yesu ujue huyo ni
mjumbe wa Mungu katikati ya wanadamu.
Yohana 8:44-45,
44 Ninyi
ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye
alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo
kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye
ni mwongo, na baba wa huo.
45 Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki.
Katika nyakati zinazokuja utaona mapambano
makali sana kati ya wale waliovaa miili kutoka kuzimu (mashetani)
wakitunishiana misuli na wale waliovaa miili
kutoka mbinguni (wajumbe wa Mungu) ili kwamba dunia nzima waokolewa
kabla ya unyakuo wa mwanakondoo Yesu Kristo.1Yohana3:10, wana wa Mungu ni dhahiri na wana wa ibilisi ni dhahiri
pia , wakati huo utaona na kutambua kuwa huyo ni mwakilishi wa Mungu au wa
shetani.
Waebrania 2:14, Ibilisi ana nguvu ya mauti, hivyo shetani anapovaa
mwili lazima awe wakala wa mauti mbalimbali, mfano mauti ya biashara, mauti ya
kazi, mauti ya ndoa . Ndiyo maana utamwona mtu analalamika kuwa biashara yangu
iliporomoka nilipoanza kushirikiana na Fulani au ndoa yangu ilivunjika nilipomkaribisha
mtu Fulani kwenye nyumba yangu, hii inaonyesha kuwa yule alikuwa wakala wa
mauti yaani mjumbe wa ibilisi aliyevaa miili na hii inatufundisha watu wa Mungu
kuwa siyo kila mwenye mwili ni mtu lazima unapokutana na mtu lazima uombe kabla
ya kushirikiana au kumkaribisha kwako.
Ezra 9:2,
2 Maana
wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi mbegu takatifu
wamejichanganya na watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na mashehe
umetangulia katika kosa hili.
Mbegu takatifu wamejichanganya na
watu wa mataifa, utaona mashetani wanajitahidi kujichanganya na watu ili uzao
wa Mungu (mtakatifu) uchafuke na kusudi la Mungu lishindwe kutimia kwa watu
wake.
Katika jina la Yesu mtu yeyote asiye mwanadamu
na amejichanganya katika familia yangu, biashara yangu ndoa yangu na kazi yangu leo naamuru ayeyuke kwa jina la Yesu.
Namna shetani aliyevaa mwili
anavyoweza kumdhhuru mtu:
1.Anaweza kukurushia matatizo kwa
kukwangalia tu. Na wakala wa shetani wanapata nguvu hizo kutoka ama baharini au
kwenye mito ambayo ni vituo vya kuongeza nguvu za kishetani. Zaburi
91:1-5, Yuda 1:6, Ufunuo 12:7, katika maandiko hayo unaweza kuona jinsi
shetani anavyoweza kuvaa mwili na kurusha mishale ili kuwadhuru watu wengine.
Mtu pia anaweza kurushiwa mishale tangia tumboni na akazaliwa na vifungo
ambavyo vinaweza kutesa maisha yake.
III. MAOMBI.
Kwa damu ya Yesu baba naomba
msamaha kwa jambo lolote nililotenda kwa kujua au bila kujua na likampa shetani
nguvu ya kunirushia mishale. Kwa damu ya Yesu bwana Yesu nisamehe na unipe
nguvu ya kung’oa mishale yote iliyorushwa kwangu. Kwa jina la Yesu Mungu unipe
uwezo wa kumtambua na kumshinda adui yangu shetani aliyevaa mwili na kuishi nami
au kushirikiana nami katika maisha yangu.
Katika jina la Yesu kila mtu yeyote anayenirushia vitu kwa macho yake au
anawarushia watoto wangu au ndugu zangu
naamuru vimrudie yeye mwenyewe
kwa jina la Yesu. kwa jina la Yesu mtu yeyote anayenirushia mishale ya magonjwa,
balaa, laana, kushindwa, kuachwa ,mikosi naamuru vimrudie yeye kwa jina la Yesu.
katika jina la Yesu naamuru mishale yote
na vitu vyote vilivyorushwa kwangu ving’oke na kumrudia yeye. katika jina la
Yesu narudisha mishale yote ya mauti iliyotumwa kwangu iwarudie wao na mimi na
watu wangu tutakuwa salama. Na kuanzia leo mwanadamu yeyote aliyevaa mwili
kumbe ni shetani nikimwona lazima nimtambue katika jina la Yesu.
‘’ Imeandikwa nitakuokoa na mshale urukao mchana’’ jina la Yesu naamuru mishale yote niliyotupiwa tangia
tumboni, mishale ya mauti, mishale ya balaa, naamuru ing’oke katika jina la
Yesu. Imeandikwa kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa nami naamuru
mishale ya mauti iliyotupwa kwangu ing’oke kwa jina la Yeskatika jina la yesu nang’oa
mishale ya laana ya familia niliyotupiwa tangu tumboni, mishale ya umasikini,
mishale ya magonjwa naamuru ng’oka kwa jina la Yesu. Kila mishale iliyotumwa
ili nisisonge mbele katika wokovu na maisha yangu naamuru rudi kwa aliyekutuma
kwa jina la Yesu.
‘’Imeandikwa Pinde za mashujaa
zimevunjika’’, kwa jina la Yesu navunja pinde zote ambazo mashetani
wanatumia kunirushia mishale magonjwa,
balaa, umasikini, kukataliwa, aibu, kwa jina la Yesu naamuru pinde zao zote
zivunjike na ghala za mishale yao ziteketee kwa moto kwa jina la Yesu.
‘’Imeandikwa kila pando asilolipanda baba yangu wa mbinguni
litang’olewa’’, leo kwa jina la Yesu
nawakamata kwa mikono ya chuma katika ulimwengu wa roho mashetani wote waliovaa miili Dar es salaam na
kuwang’oa kwenye miili yao warudi kuzimu na miili yao naizika kwa jina la Yesu. Nawafuata mashetani wote
waliovaa miili Morogoro nawang’oa na kuwaamuru warudi kwao kuzimu kwa jina la
Yesu. Nawanyofoa kwenye miili mashetani wote walioko Mwanza nawamuru kurudi
kuzimu na kuachia maisha ya watu wa Mungu kwa jina la Yesu, Nawafuata mashetani
wote walioko Kagera ambao wameoa na kuolewa na wanadamu na wamesababisha
matatizo kwenye maisha ya watu nawang’oa na kuwaponda vichwa vyao na
kuwarudisha kuzimu na miili yao izikwe kwa jina la Yesu. Naikamata Tanzania
yote na mikoa yote kila shetani aliyevaa mwili lazima ang’oke na kurudi kuzimu
kwa jina la Yesu.
Amen
![]() |
Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe |
Comments