Baada ya watu kuonewa na huyu shetani kwa muda
mrefu sana, sasa Mungu kwa kupitia mtumishi wake Mchungaji Evarest
Shaban atawasha moto wa Injili akishirikiana na watumishi wa Mungu
kutoka mataifa mbalimbali kama vile Uganda, Tanzania na Kenya. Waimbaji
mbalimbali watachukua nafasi zao za uimbaji kwaajili ya kumtukuza Mungu
na kumzomea adui mkubwa duniani aitwaye shetani mwenye jina baya kuliko
yote duniani na mbinguni. Siku hiyo itakuwa ni siku ya pekee sana, watu
watabarikiwa na kuinuliwa, watu wataokoka siku hiyo. Mkutano utafanyika
katika kanisa la Jeus Deliverance Centre Tegeta Pwani. Panda magari ya
Boko/Bunju shuka njia panda ya Chanika uliza ofisi za serikali za mitaa
utaonyeshwa kanisa. Kazi ya Bwana itaanza siku ya tarehe 01 hadi 07/09/2014 kuanzia
saa 9:30 jioni -12:00 jioni. Mawasiliano yetu ni + 255 716 968 033 au +255 765
034 353
Comments