MWL. MWAKASEGE ANAWAPIGA MSASA WACHUNGAJI WA MORAVIAN NCHINI

Mwalimu Christopher Mwakasege katikati akiwa amekaa na maaskofu wa Moravian.
Baada ya mgogoro wa muda mrefu ndani ya kanisa la Moravian nchini (KMT) wachungaji wa kanisa hilo nchini wapo mkoani Dodoma kwa semina ya kuwekana sawa katika huduma ikifundishwa na mwalimu Christopher Mwakasege ambaye amealikwa kama mfundishaji katika semina hiyo.

 Semina hiyo ambayo imeanza siku ya leo licha ya kuhudhuriwa na maaskofu na wachungaji wa kanisa hilo nchini pia mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi alikuwepo katika ufunguzi wa semina hiyo asubuhi ya leo kwakupata nafasi ya kuzungumza machache na kuwakaribisha viongozi wa kanisa hilo mkoani humo. 

Ni takribani miaka mitatu sasa tangu mgogoro ufukute ndani ya kanisa hilo huku siku za karibuni ikishuhudiwa baadhi ya wachungaji wakivuliwa madaraka ya kuongoza sharika zao kutokana na mgogoro huo. Mwaka 1997 ulitokea mgogoro mkubwa ndani ya kanisa hilo pale watu wa kutoka Kyela waliponyimwa haki ya kuwa na jimbo lao huku pia ikidaiwa kitendo cha mchungaji kutotambua cheti cha safari cha mmoja wa waumini wa kanisa hilo kutoka Kyela katika ibada ya jumapili iliyofanyika usharika wa Mabibo jijini Dar es salaam ndipo mgawanyo ulipotokea na kuzaa kanisa jipya la Kiinjili la Moravian Tanzania ambalo kwasasa linazidi kupanua wigo wake katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kadhalika na mikoani. 

Endapo mgogoro huu uliopo usipoisha kwa amani kuna uwezekano kanisa la tatu la Moravian huenda likaanzishwa nchini. Mungu aingilie kati.

AMEN 




Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt Rehema Nchimbi akitoa neno la ukaribisho.

Mwalimu Christopher Mwakasege akipiga gombo kwa wachungaji.

  Maaskofu na wachungaji wakiwa katika semina hiyo. 




Hii ndio hali katika semina hiyo ©Mapasa Ipyana

Comments