NI HATARI SANA KUWA ZEZETA WA KIROHO

Na Abel Suleiman Shiriwa
Kwa kipindi hiki tunao Wakristo ambao binafsi hawapendi kukaa magotini pa Mungu,
Ili kuweza kupata ya rohoni, hawapendi kujifunza maandiko na kuyaelewa yana maanisha nini?
Wanapenda kukariri tu mambo ambayo wanalishwa na Viongozi wao ambao hawapendi kuikemea dhambi, Wanapenda uilembe na kuipamba dhambi, kama apambavyo bi harusi,
Wakikuona wewe unaikemea dhambi, na kuwakemea wale watendao dhambi, basi hukuona ni mtu usiye faa, umechukua jukumu la Mungu, la kuhukumu, hao hawajui tofauti ya hukumu ya kemeo, andiko ambalo linawaponza ni hili.

Mathayo 7:1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.
2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.
3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?
4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?
5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

Andiko hili ni kichaka kikubwa sana cha watendao dhambi cha KUJIFICHIA
Ili wasisemwe juu ya maovu yao wayafanyayo, YAANI Usimkemee juu ya dhambi, atakuambia, USIHUKUMU, Ondoa kwanza boriti lilimo ndani yako.
kwa akili zao wao wanadhani Boriti, ni kitu ambacho kimeganda mwilini, hawajui kuwa Boriti ni TOBA ambayo mtu anapaswa kuifanya, ili imuwezeshe kuwa safi, kuwa safi kwa maana ya UTUMISHI WA MUNGU usio laumiwa, kisha awe na jukumu la kuwaweka sawa watu, waache kufanya maovu, maana unapoingia katika habari ya kumtumikia Yesu, hupaswi kuwa mchafu, kama watu wa Mataifa, Maana Huwezi kumwambia mtu aache ulevi, mtu ambaye unakunywa nae kila siku, bali ya kupasa wewe kuacha kwanza POMBE, NDIPO uweze kumwambia mwingine nae aache kunywa, BORITI “HAPA YESU alikuwa anamaanisha juu ya utakaso, jitakase kisha uone vema kuwaambia na wengine nao pia wajitakase, Sasa mtu ukisha jitakasa na kuwa safi mbele za Mungu, ukimwambia, huyo atendae dhambi, aache kutenda dhambi, anahamaki na kusema umemuhukumu”


YESU ALIMAANISHA NINI KUSEMA MSIHUKUMU?

Mathayo 7:1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.
2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. 


HAPA YESU ALIKUWA ANAMAANISHA HUKUMU YA VITENDO, YAANI KUMUADHIBU MOJA KWA MOJA MTENDA, mfano:
mtu kaiba, kazini, wewe uchukue Jukumu la kumpiga, na hata kumuua, hapo utakuwa umechukua hukumu la kumuhukumu (Kumpa adhabu), maana hujampa nafasi ya kutubia uovu wake, ‘Maana unaweza kumuhukumu kifo mtu wakati wewe nawe una dhambi ambayo umeifanya ambayo nawe yakupasa uuawe’ Kama ambavyo Yesu alivyopelekewa mwanamke aliye zini, na kuwataka hao waliotak kuhukumu yaani kutoa adhabu, wafanye wao hukumu hiyo, ikiwa wao ni wasafi.

Yohana 8:1 [Walikwenda kila mtu nyumbani kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlima wa Mizeituni.
2 Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha.
3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.
4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.
5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?
6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.
10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?
11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]

”HAPA TUNAONA HEKIMA YA YESU KWA WANAFIKI HAO AMBAO WALITAKA KUMKANDAMIZA MWANAMKE KWA KUMPELEKA YEYE PEKE YAKE, ILI AWEZE KUHUKUMIWA, BILA MTU YULE ALIYE ZINI NAE, MAANA MWANAMKE HAWEZI KUZINI PEKE YAKE WALIATAKA ITEKELEZWE HUKUMU YA VITENDO, YAANI MWANAMKE YULE AADHIBIWE KWA KUPIGWA MAWE, YESU AKATAKA KWANZA WAO WAWE SAFI, KABLA YA KUTAKA KUTEKEKELZA HUKUMU YA VITENDO”.
Lakini kauli ya Yesu mwisho inadhihirisha kuwa yule mwanamke ni kweli alifanya uzinzi, ndiyo maana alimwambia, wala mimi sikuhukumu, Enenda zako usiende dhambi tena, Asitende dhambi awe safi ili aweze kupata kibali cha kuingia kwenye ufalme wa Mungu, asiwe kama wale washitaki wake ambao hawataki kuondoa boriti zao. KWA HIVYO ILEWEKE KUWA:-
Kumwambia mtu asitende dhambi, aache dhambi, siyo kumuhukumu, bali ni kuiponya roho yake, kama ambavyo Yesu alimwAmabia mwanamke, asitende dhambi, Hakumpa hukumu ya mwili.. Bali onyo la kinywa.
Ezekieli 18:23 Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?
24 Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa.

KWA HIVYO KUWAAMBIA WATUBU WAACHE DHAMBI ZAO, SIYO KUWAHUKUMU, BALI NI KUWASAIDIA WASIJE KUFA KATIKA DHAMBI ZAO, MAANA SHARTI LA KUHUBIRI INJILI, NI KUWAAMBAIA WATU WATUBU, NA KUBATIZWA, WAPATE ONDOLEO LA DHAMBI, NA SIKUWAHUKUMU, KWA MAANA YA KUWAPA ADHABU YA MWILI.
Ni makosa makubwa sana mbele za Mungu, kukaa kimya, yaani kushindwa kumwambia mtu muovu aache njia yake mbaya, maana roho ya mtu yule Mungu ataitaka kwako, lakini ukimwambia utakuwa umenawa, huna hatia.
Ezekieli 18 Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
19 Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.


MUNGU akubariki 
By  Abel Suleiman Shiriwa

Comments