PETER MABULA: SHUHUDA ZANGU MBILI NI HIZI.

BWANA YESU asifiwe ndugu zangu.
Leo naomba nikishuhudie shuhuda mbili za mambo ambayo mimi mwenyewe yalinitokea, hua nina shuhuda nyingi sana ambapo BWANA aliniponya au kunionyesha jambo fulani ambalo hata siku moja sijawahi kuliwaza.

Karibu.
Katika Kila Maneno 100 Ninayoongea Siku Zote, Natamani 98 Katika Hayo 100 Niliyoongea Niwe Nimemtaja BWANA YESU Maana Ametenda Makuu Sana Maishani Mwangu, Mwaka 2010 nilipata ajali mbaya sana nikiwa Zanzibar. Nilikuwa natoka Chukwani naenda Migombani saa 3 Usiku. Wakati wa kushuka Dereva alikuwa amelewa hivyo ile naanza kushuka tu aliondoa gari na kupelekea kunirusha juu sana, nidondokea Lami na kuzimia pale pale katikati ya Barabara, Watu Walisema Nimekufa Baada Ya Kuzimia Masaa 15, Baada Ya Kupata Ajali , Lakini Muda Huo BWANA Alikua Amenichukua Katika Ulimwengu Wa Roho Na Kunionyesha Mambo Ya Mbeleni Ambayo Nitatakiwa Kuyatenda Kihuduma, Hiyo Ilikua December 27 Mwaka 2010. Namshukuru sana BWANA YESU maana licha ya kukataliwa katika Hospital ya migombani maana madaktari pale walisema siwezi  kupona na hawana vifaa vya kunitibu, nilipelekwa Hospital ya Bububu na madaktari huko na wao walisema ni ngumu sana mimi kupona , wakidai Damu yangu imechanganyikana na ubongo hivyo matibabu yangu lazima nipelekwe India ndani ya Masaa 12 na kwa hali niliyokua nao isingewezekana kuwahi India maana nilikuwa nimezidiwa sana, Tangu Hospital ya kwanza hadi hii ya pili nilikuwa bado sijajitambua. Lakini maajabu ya BWANA YESU yalitokea maana kesho yake nilizinduka kutoka katika kuzimia na kuwakuta watu wamekata tamaa ya mimi kuishi. Watu wa kanisani waliingia kwenye maombi ya kufunga na cha ajabu Dokta mmoja alisema mbele yangu kwamba Siwezi kumaliza masaa 24 yaliyofuata nikiwa hadi, wamama wa kanisani waliokuwepo muda huo waliangua kilio kikuu sana, cha ajabu mimi licha ya kuisikia sauti hiyo ya Dokta wala haikunishughulisha maana wakati nimezimia hayo masaa 15 BWANA alikuwa ananionyesha mambo mengi tu ambayo mimi nitayafanya katika huduma ya kumtumikia Yeye. Niliwaza moyoni kwamba ''Daktari wa duniani asaema nakufa masaa machache yajayo lakini Daktari wa mbinguni ambaye ni BWANA YESU amesema nitamtumikia na kusitawi sana.''  Nilikaa Hospitali kwa siku 6 tu, siku ya 7 nikatoka nikiwa mzima kabisa na baada ya mwezi mmoja sikuwa hata na kovu lolote la ajali na hata wewe ungeambiwa kwamba ' Huyu alipata ajali wiki 3 zilizopita na kupelekea madaktari kusema haponi, ungekataa'' Siku ya ajali nilipata makovu mengi lakini BWANA YESU aliyaponya ghafla hadi siku natoka madaktari walisema hakika mimi ni mgonjwa wa ajabu,. mimi hayo sijui ila namshukuru tu BWANA wa uzima kwa uzima wake kwangu.
 Nampenda Sana BWANA YESU. Ndugu Uliyempokea BWANA YESU, Nakutia Moyo Kwamba Uko Upande Sahihi Na Hakuna Uzima Kwingine Nje YESU Na Kama Wewe Hujaokoa Nakuomba Okoka Leo. BWANA YESU Anatupenda Sana Wanadamu Na Ndio Maana Alijitoa Ili Afe Kwa Ajili Ya Wanadamu, Ndugu Mpokee Huyo Maana Hakuna Uzima Kwingine. Na Ndio Maana Hata Jina Lake Mimi Huliandika Kwa Herufi Kubwa Zote, Ili Jina Hilo Lionekane Kwa Urahisi. Natamani Katika Jumbe Zangu Zote Watu Waone Jina La YESU Zaidi Ya Vyote. Ndugu, Ni YESU KRISTO Pekee Anayeweza Kukuokoa Katika Yote. 

MUNGU akubariki sana na ushuhuda wa pili ni huu kwa leo.

 Nampenda Sana BWANA YESU Maana Yeye Alinipenda Kwanza. Tarehe 29 August 2013 Ilikuwa Ni Siku Yangu Ya Kuzaliwa Nikitimiza Miaka 27, Na Siku Hiyo Askofu Moses Kulola Alifariki. Siku Hiyo Usiku Katika Maono Nilijikuta Mbinguni. BWANA YESU Alikua Amekaa Katika Kiti Cha Kung'aa, Akaniambia " Mtumishi Wangu Moses Amemaliza Kazi Niliyomtuma Duniani" Wakati Akisema Hayo Niliona Kundi La Watu Na Askofu Kulola Akiwa Mmoja Wao Wakiwa Na Furaha. Baada Ya Tukio Hilo BWANA YESU Akaniambia " Chukua Hiyo" Nikatazama Pembeni Yangu Kuna Meza Ya Kioo Na Juu Ya Meza Hiyo Kuna Jagi Kama Birika La Vioo Linang'aa Likiwa Na Maji Ndani Yake, Nikalibeba Lile Jagi Na Akaniambia Nimwage Maji Yaliyokuwemo Ndani Yake, Nikaanza Kumwaga, Wakati Namwaga Nikaona Kundi La Watu, Na Kadri Ninavyomwaga, Ndivyo Wale Watu Wanaongezeka Na Kuwa Maelfu Ya Watu. Baada ya hapo nikajua maji yameisha kwenye jagi kumbe bado yamo ila kidogo akaniambia niyamwage na hayo  Nikaanza Kumwaga Tena Na Kuona Kundi Jingine La Watu, Akasema Moses Kulola Kazi Kubwa Ameifanya Hayo maji ambayo nimeyamwaga mwanzo na kuonekana maelfu ya watu  hiyo ndio kazi aliyoifanya Moses Kulola na haya ambayo nimeyamwaga awali ya pili ni kazi ambayo tunatakiwa tufanye wahubiri wa Tanzania waliopo sasa. Ndugu zangu sio kwamba hayo maji kidogo ya pili ni idadi dogo ya watu hapana ni wengi sana yaani kwa kukadiria kwangu ni kama Milioni 3. Baada ya kuambiwa na kuona hayo nilijikuta niko tena Nyumbani kwangu kawe ninapoishi. Ushuhuda huu ulinifanya nijitambua kwamba na mimi ni mmoja ya wahubiri wa injili katika Tanzania. Mwanzo sikujua kama na mimi ni mhubiri lakini wakati huo nilijitambua rasmi. Nilianza kuwaza hivi kweli BWANA YESU ameamua kuniunganisha na mimi Peter katika kundi  moja na Watumishi wake aliowainua sana na ambayo nawapenda sana, kama vile wao walivyo wahubiri wa injili na mimi pia, Niliwatafakari sana akina Mwl Mwakasege na wengine wengi ambao MUNGU ameinua huduma zao na nikabaki na neno moja ambalo mwanzo sikulipa umuhimu mkubwa kwamba Wao ni wahubiri kutoka Tanzania na mimi pia vilevile ni mhubiri kutoka Tanzania.
Namshukuru MUNGU sana.
na siku nyingine nikipata nafasi nitakushuhudia mambo mengine zaidi maana nina shuhuda nyingi sana kama vile ambavyo na wewe ndugu yangu una shuhuda nyingi, pia kama na wewe utapenda ushuhudie karibu. Kinachotakiwa ni shuhuda za ukweli tu pamoja na kumtukuza MUNGU aliye hai. Tumia anuani na au namba za simu hapo chini na ushuhuda wako utawekwa hapa. barikiwa.

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292 

                     mabula1986@gmail.com
                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
 MUNGU Akubariki.

Comments