ROSE MUHANDO NA CHRISTINA SHUSHO WASHINDWA KUNG'AA KATIKA TUZO ZA AFRICA.

Hatimaye tuzo za injili za Africa gospel music awards kwa mwaka 2014 zilitolewa usiku wa jumapili hii huko jijini London nchini Uingereza na kushuhudia waimbaji watatu kutoka nchini Tanzania ambao walipendekezwa kuwania tuzo hizo wakitoka mikono mitupu. 

Photo: A night  dedicated to recognition, appreciation, performance, productivity, profiling and networking! 24/08Tuzo hizo ambazo zilikuwa zikifanyika kwa mara ya tano, ni waimbaji wa nchi jirani ya Kenya ndio waliondoka na tuzo kwa mwaka huu pamoja na waimbaji wengine kutoka barani Afrika hususani Afrika magharibi, Ghana na Nigeria. Katika tuzo hizo Tanzania ilikuwa ikiwakilishwa na waimbaji watatu Rose Muhando aliyekuwa akiwania tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa mwaka barani Afrika tuzo ambayo imetwaliwa na wadada wawili Diana Hamilton pamoja na Nikki Laoye. 

Aidha kwa upande wa Christina Shusho aliyekuwa akiwania tuzo mbili ikiwemo ya video bora ya mwaka kupitia wimbo wake wa Nataka nimjue, tuzo hiyo imechukuliwa na Sammy Okposo wa Nigeria kupitia wimbo wake wa 'Who tell you say', huku tuzo ya mwimbaji bora wa Afrika mashariki ikichukuliwa na mwanakaka Bahati kutoka nchini Kenya. Aidha kwa mara ya kwanza mwimbaji wa muziki wa kufokafoka ama rap za injili Gazuko Junior aliyeandika historia ya kuwa mwimbaji wa kwanza wa mtindo huo kutoka nchini kuingia katika tuzo hizo hakuweza kuipata tuzo hiyo ambayo ilichukuliwa na Miller Luwoye wa Uingereza.  

Tunawapongeza waimbaji wote waliopendekezwa kuwania tuzo hizo kwakuwa hiyo ni hatua kubwa sana ambayo inaonyesha muziki wao na huduma yao kutambuliwa kimataifa, pia kwa wapigaji kura itabidi tuongeze juhudi mara dufu mwakani ili kura zitoshe na hatimaye tuzo hizo zije Tanzania. Mungu awabariki sana, ukitaka kuona orodha kamili ya washindi wa tuzo hizo ziko hapo chini.

Mtazame Sammy Okposo na video yake iliyochukua tuzo -






AFRICA GOSPEL MUSIC AWARDS WINNERS 2014



 DISCOVERY OF THE YEAR
          Akesse Brempong(Ghana) &
          Meskeerem Getu(Ethiopia)

ARTISTE OF THE YEAR CENTRAL AFRICA
Gaby Irene Kamanzi(Rwanda)

ARTISTE OF THE YEAR WEST AFRICA
Cwesi Oteng

ARTISTE OF THE YEAR EAST AFRICA
Bahati

ARTISTE OF THE YEAR USA & CANADA
Dee Jones & Nii Addo

ARTISTE OF THE YEAR EUROPE
Allen Caiquo(UK)

ARTISTE OF THE YEAR SOUTHERN AFRICA
Pompi(Zambia)

ARTISTE OF THE YEAR NORTH AFRICA/M.EAST & ASIA
Bro. Philemon(China)

 VIDEO OF THE YEAR
  Who tell you say – Sammy Okposo

FEMALE ARTIST OF THE YEAR
Nikki Laoye & Diana Hamilton

RADIO PROGRAMME & DJ OF THE YEAR
Sunday Best – Sabina
Adorn Live Worship – K. Idan

TV PROGRAM OF THE YEAR
 Divine Jams – Tina Owinyi (Uganda)

AFRO RAP ARTISTE OF THE YEAR
David Kalilani(Malawi)

AFRO JAZZ ARTISTE OF THE YEAR
 Miller Luwoye(UK)

GROUP/CHOIR OF THE YEAR
Loveworld Music Ministry Durban(South Africa)

EVENT OF THE YEAR
Africa Worships- Sonnie Badu

PRODUCER OF THE YEAR
        Koda

SONG OF THE YEAR
        I know who I am - Sinach

ALBUM OF THE YEAR
        Justified - Eben(Nigeria)

MALE ARTISTE OF THE YEAR
        Cwesi Oteng(Ghana)

TRAILBLAZER AWARD
        Gabriel Eziashi(UK)
          Rose Muhando(Tanzania)

INSPIRATION AWARD
        Royal Priesthood(Ghana)
          Tim Tehilla Crew(Nigeria)

AGMA SPECIAL AWARDS
Shabach
Fred Williams
Wole Awolola
Uvi Orogun

CONTRIBUTION AWARD FOR THE PROMOTION OF AFRICAN GOSPEL MUSIC
        Zanele Mbokazi – CEO of Crown Gospel Awards(South Africa)
          U – Chenna- Destiny Child Talent Show(Nigeria)
          Alordia(UK Promoter)

LIFETIME ACHIEVEMENT AWARDS
Rev. Tim Omotoso (South Africa)

Comments