TAMBUA THAMANI YA KUNENA KWA LUGHA MPYA.

Na Nickson Mabena


Matendo 2:4
''Wote Wakajazwa Roho Mtakatifu, Wakaanza kusema kwa LUGHA NYINGINE, kama Roho alivyowajalia kutamka.''

Baada tu ya Kumpokea Yesu Kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yangu, haikupita mda sana nikajazwa Roho Mtakatifu, nikaanza Kunena kwa Lugha...
Nakumbuka Iliku nimehudhuria Ibada ya Jumapili Katika Kanisa la EAGT-City Center kwa Pastor F. J.Katunzi, nikakutana na Somo la ROHO MTAKATIFU, Baadae Waliitwa Mbele Watu ambao Wangetamani Kujazwa Roho Mtakatifu, na mimi Nilitoka Mbele, baada ya Maombi nikaanza Kunena na mimi.
Ghafla Maombi yangu yalibadilika, Nikawa Najiamini sasa kama Mimi ni Mkristo wa Kweli.
Leo Sita Zungumzia UJAZO WA ROHO MTAKATIFU, Ila Kwa Sehemu, nataka nizungumzie Kwa Sehemu, UTHAMANI WA KUNENA KWA LUGHA MPYA, ambayo ni Matokeo ya Kujazwa Roho Mtakatifu. Nianze na Sehemu ya Kwanza ya Somo. SehemU 1.

Kunena Kwa Lugha Kuna thamani, Kwa Sababu:-
1.Ni fundisho la Kibiblia. Mdo 10:44-46.
''..... Kwa maana Waliwasikia Wakisema Kwa Lugha...''


 2.Ni Aina ya Maombi Mbele Za Mungu.
1Kor 14:2
''Maana yeye anenaye kwa Lugha, hasemi na Watu, bali husema na Mungu; maana hakuna Asikiaye; lakini anena mambo ya Siri katika roho yake.''
Katika Mambo ya Muhimu katika Maisha ya Mkristo, ni Maombi. Na Kama Mtu anahitaji Matokeo makubwa, au ya haraka basi ni Muhimu aombe kwa Kunena kwa Lugha, Binafsi napenda sana kuomba kwa kunena kwa Lugha, Kama hujaanza kunena, basi tamani na Mungu ni Mwaminifu sana atakujaza (Luka 7:37).
Pia tusome pamoja Maandiko yafuatayo
''Kadhalika Roho hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.'' RUMI 8:26
Kuna Watu hutamani Sana kuomba kwa Mda Mrefu, Ila Wanashindwa, Hebu Anza kuomba kwa Kunena.


MUNGU akubariki sana.
By Nickson Mabena.

Comments