Skip to main content
TB JOSHUA ATUMA MSAADA WA CHUPA 4000 ZA MAJI YA UPAKO KUPONYA EBOLA SERRA LEON
Nabii
maarufu ndani na nje ya bara la Afrika TB Joshua wa kanisa la All
nations (Scoan) la nchini Nigeria ametuma chupa 4000 za maji ya upako
pamoja na dola za kimarekani 50,000 nchini Sierra Leon ili kusaidia
kutibu ugonjwa wa ebola ambao umeikamata nchi hiyo.
Nabii Joshua amesema kupitia tovuti ya kanisa lake kwamba maji hayo
yamesafirishwa kwa ndege maalumu ya kukodi ambayo gharama yake pia ni
dola 50,000 na kufanya gharama kamili dola 100,000 (laki moja) kwa
msaada alioutoa akishirikiana na wadau wa Emanuel TV ya kanisa lake.
Katika taarifa yake kupitia tovuti hiyo nabii TB Joshua amesema Mungu
mwenye nguvu atajidhihirisha uweza wake kupitia maji hayo ya upako
ambayo yametolewa kwa watu waliokumbwa na ebola. "Sio maji ndiyo ya
ponya ya wagonjwa ila ni Yesu mwenyewe, lazima mtu anayemuombea mwingine
na yule anayeombewa wawe na imani. lazima imani iwe hai ili kupata
uponyaji kwasababu ndiyo husababisha uponyaji na sio maji ya upako"
amekaririwa nabii Joshua.
Watu waliotumia maji hayo ya upako wamekiri kuwa na imani nayo kutokana
na wengi kufunguliwa na miujiza mingi kutendeka kutoka hali ya kutokuwa
na uwezo wa kuzaa na hatimaye kupata mtoto lakini pia maji hayo yamekuwa
kinga ya risasi kupenya kwenye gari kama mtu mmoja kutoka nchini Ghana
alivyopona mikononi mwa majambazi waliokuwa wakishambulia kwa risasi
gari lake yeye akiwemo ndani bila mafanikio.
Comments