TUJIPE MOYO ILI TUONDOKANE NA DHIKI.

 Na Kabalama Masatu

Yohana16:33
"Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu.Ulimwenguni mnayo dhiki;lakini jipeni moyo;mimi nimeushinda ulimwengu".

Bwana Yesu asifiwe mpendwa wangu......
Hebu tuyaangalie maandiko haya ambayo leo Bwana Yesu anazungumza na sisi.
Yesu anatambua kabisa ili tuwe na amani ni lazima kwanza atuambie jambo na sisi tulifuate lile alilotuambia.
Yako maneno mengi sana ambayo unaweza kuambiwa na watu lakini hayo yote hayawezi kukuletea amani isipokuwa Neno la Kristo peke yake.

Ndani ya Neno lake Kristo ndipo tunapata amani na wala siyo vinginevyo.
Kwa habari ya amani ni lazima kwanza ufuate Neno la Kristo.
Kwa habari ya amani ni lazima kwanza umsikilize Kristo Yesu.
Kwa habari ya kufuata Neno la Kristo ni lazima kwanza uokoke.

Bwana Yesu asifiwe.......
Bwana Yesu anatambua vizuri mno dhiki tuliyonayo hapa duniani,hivyo anatuambia tujipe moyo.
Yamkini wewe una dhiki ya kukosa kibali yaani kukataliwa.
Yamkini wewe una dhiki ya kukosa amani katika ndoa yako.
Yamkini wewe una dhiki ya umasikini.
Yamkini wewe una dhiki ya kutengwa na ndugu zako.
Yamkini wewe una dhiki ya kukosa kazi.
Yamkini wewe una dhiki ya kukosa mtu wa kukusomesha.
Sikia leo Mungu anavyosema kupitia maneno yake Yesu Kristo ya kwamba ujipe moyo.

Kwa habari ya kushinda dhiki inakubidi uwe mvumilvu wala usijeukasema nimevumilia mpaka nimechoka.
Kumbuka kama Bwana kasema jipeni moyo basi uwe na uhakika kwamba atakutolea njia ya kukuondoa katika hiyo dhiki uliyonanyo.
Jambo analolitaka Mungu leo hii kwako wewe ni kufuata kile alichokwambia Yesu Kristo na hapo ndipo utakuwa na amani na hatimaye kuishinda dhiki.
Iko dhiki inayoletwa na shetani,lakini Bwana anasema "jipe moyo" ili uishinde hiyo dhiki.

Comments