VIKWAZO VYA KUFIKIA HATMA YAKO(HOFU)

Na Mch. Mwangasa (SNP, Ufufuo Na Uzima, MOSHI)


Utangulizi: Hesabu 13:17-> , Musa aliwatuma watu 12 wakachunguze nchi, waliokuwa ameahidiwa. Na baada ya kuichunguza nchi kila mmoja akaja na majibu. Wakaeleza mambo mazuri katika ile nchi, kwamba kuna maziwa na asali, lakini wakaja na taarifa nyingine kuwa nchi inakula watu na kuna wanefiri.. Tunaweza kutambua kirahisi kuwa hawa watu walipo waona waliingia kwenye hofu.. kumbe hofu yaweza kuhatarisha hatma yako..
Nguvu ya Milango ya Fahamu katika kuleta hofu
Binadamu ana milango ya fahamu mfano macho, pua, masikio n.k. vitu hivi vyaweza kutumika kumtukuza Mungu au kukukatisha tamaa,

i) HOFU KWA KUONA
 
kimsingi watu hawa waliingiwa na hofu kwasababu ya macho yao.. na haya macho yakawafanya wasahau yote ambayo Mungu aliwatendea hapo kwanza. Walisahau jinsi Mungu aliwavusha bahari ya shamu.. kumbe hata kwenye maisha ya kawaida Mtu unaweza kusahau matendo makuu ya Mungu aliyowahi kukutendea. Kwasababu tu ya hofu, kumbe hofu yaweza kukufanya ukose hatma yako..
 
ii) HOFU KWA KUSIKIA
 
Baada ya hawa watu kurudi, kutoka kutazama wakaja na taarifa mpya, katika wale 12, 10 wakasema yale mambo ya kukatisha tamaa, na makutano walivyosikia waka vunjika moyo. Na hii ikawapelekea kukata tama na kutaka kuwapiga mawe Kalebu na Joshua ambao walisema kuwa Mungu aweza kuwaokoa na watu wale. Kumbe Hofu yaweza kuingia kwasababu ya kusikia.. na ikakupelekea ukate tama ya kuishi na hivyo kuharibu hatma yako.
Nguvu ya taarifa;
Taarifa yaweza kukufanya urudi nyuma kwa kuingiwa na hofu, wana wa Israel nao waliingiwa na hofu, hadi wakanena maneno ya makufuru. Kumbe taarifa ni za kuzitilia maanani taarifa yaweza kumfanya mtu atende dhambi ya hofu (kwa maana biblia inasema kuwa kila jambo linalotendwa pasipo imani ni dhambi,) hofu ni dhambi.

Madhara ya Hofu
 
Hofu yaweza kukusababisha kutokujiamini, kukata tamaa, inavunja nguvu ya imani, kurudi nyuma, kuishiwa nguvu, kuchoka na unaweza kutamani kujaribu njia nyingine ambayo ni mkato. Hofu ni mwanzo wa kushindwa. Mfano: Kuna mtu alikuwa na mgodi ambao aliuchimba miaka mingi lakini hakupata dhahabu na miaka ilipokwenda akaamua kuliuza kwa kupata hofu kuwa miaka itapita na ataliacha kuwa halina kitu. Siku chache baada ya kuliuza, akapita mgodini akamkuta Yule mtu aliyemuuzia anapakua dhahabu, baada ya kumuuliza akamwambia , nakushukuru sana maana baada tu ya kuniuzia mgodi sikulazimika hata kutumia mashine. Maana dhahabu zilikuwa dhahabu.
Kumbe wakati mwingine hofu yaweza kukufanya ukate tamaa wakati unakaribia kwenye hatma yako. Wana wa Israel walipoisikia ile habari wakaamua kulia usiku kucha, na kuunza kusema bora Mungu angewaacha kule Misri, hii yote ni kwasababu hofu walizozipata kutoka kwenye taarifa ya wapelelezi 10.
Nguvu ya Ujasiri
Esta 5:1-> .., Ilipotangazwa amri kuwa wana wa Israel wauwawe, Esta ahakuogopa bali walichukua hatua ya kuomba na kuchukua hatua ya kwenda kwe mfalme kinyume na desturi. Huu Ujasiri wa Esta ukawaokoa kutoka katika kuangamia kumbe kuna uweza katika ujasiri. Mungu hakutuumbia roho ya uoga.
Joshua 3 :1->.., wana wa Israel walipofika karibu kabisa ya kanaani. Hili neno *karibu kabisa* ni la muhimu likimaanisha walikuwa karibu na hatma yao. Na inawezekana umekaribia kufika karibu na hatma yako, ndipo wakakutana na mto Yordani wakpata hofu kwa vile mto ulikuwa umefurika, na wakasahau kuwa Mungu aliwavusha kwenye bahari.. ya shamu.
Kumbe waweza kukaa unamtukuza Mungu na matendo yake makuu na ukataja uweza wake, na kusimulia matendo makuu lakini hofu ikikuingia tu hayo yote utayasahau. Hofu yaweza kukusahaulisha uweza wa Mungu aliokutendea. Lakini jambo la ajabu likatokea, ujasiri wa Joshua ukawafanya kuvuka tena kwa kukanyaga maji yakiwa yanatembea.

Ushindi Juu Ya Hofu.

Ukishinda hofu moja kwa moja unaondoa vikwazo kwa hatma yako na Baraka zetu. Mungu ametupa kushinda dhambi ya hofu.. na ndio maana ni vizuri toks motto akiwa mdogo kusikia maneno mazuri ya kumletea ujasiri na si kumtia hofu na kumkatisha tamaa. Mungu ametutengenezea hatma njema lakini lakini hofu yaweza kutuondoa kwenye hatma hii..
Wana wa Israel walibeba sanduku la agano ambalo ndani yake kulikuwa na vitu vyenye kumbukumbu ya uwez a wa Mungu. Hivyo hata sisi tuna wokovu ndani ya wokovu kuna Jina la Yesu na ndani kuna uweza na ujasiri kumbe ujasiri wetu unatoka kwenye jina la Yesu ndani ya wokovu.

Mungu akubariki.

Comments