
![]() |
Rose Muhando |
Rose Muhando anawania tuzo ya mwimbaji wa kike wa mwaka Female artiste of the year ikiwa ni mara yake ya kwanza kuwemo katika tuzo hizo. Yeye anawania tuzo na waimbaji wengine maarufu Afrika akiwemo Ntokozo Mbambo, Vicky Vilakazi, Diana Hamilton, Winnie Mashaba, Gloria Muliro pamoja na Sarah K wote wa Kenya pamoja na waimbaji wengine ikiwa jumla ya waimbaji 15. Kikubwa ni kumpigia kura ROSE MUHANDO katika kipengele hiki.
![]() |
Christina Shusho. |
Aidha tuzo ya pili anayowania mwanamama Christina Shusho ni tuzo ya video bora ya mwaka Video of the year kupitia wimbo wake wa 'Nataka Nimjue' tuzo ambayo anawania na wanamuziki wengine kama Tehila Crew la Nigeria ambao pia mwaka jana waliondoka na tuzo, Daddy Owen wa Kenya, Sammie Okposo wa Nigeria na waimbaji wengine wanaofanya jumla ya waimbaji 15 wanaowania tuzo hizo. Kikubwa sie ni CHRISTINA SHUSHO wa kumpigia kura ingawa katika kipengele hiki kutakuwa na ushindani mkubwa hasa ikizingatiwa kwamba Afrika magharibi wanawapigia kura za kutosha waimbaji wao hata sisi tukijituma tunaweza.
Kwa mara ya kwanza katika historia mwanakaka Gazuko Junior kupitia uimbaji wake wa kufokafoka Afro Rap Artiste of the Year na waimbaji kutoka Uholanzi, Uingereza, Nigeria, Ghana, Malawi, Kenya, Botswana pamoja na Zambia. Kikubwa ni kumpigia kura GAZUKO JUNIOR ili tuzo ije Tanzania. ama rap anawania tuzo ya mwimbaji bora wa rap wa mwaka Ili kupiga kura BONYEZA HAPA
KUMBUKA ZIMEBAKI SIKU 3 TU KABLA ZOEZI LA UPIGAJI KURA KUFUNGWA. UNARUHUSIWA KUPIGA MARA NYINGI UWEZAVYO. -
Comments