Na Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima. Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe |
NENO
LA MSINGI: Wagalatia 3:1
1 Enyi Wagalatia msio na akili, ni
nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya
kuwa amesulibiwa?
Kumbe inawezekana mtu akalogwa akili yake
bila kujua.
Musa alipotaka kutengeneza hema ya
kukutania Mungu alimwelekeza kwa mtu mwenye akili ya kuitengeneza hiyo hema.
Kutoka 35
30 Kisha Musa akawaambia wana wa
Israeli, Angalieni, Bwana amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana
wa Huri, wa kabila ya Yuda;
31 naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina;
32 na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba,
33 na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za werevu kila aina.
34 Naye amemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani.
35 Amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.
31 naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina;
32 na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba,
33 na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za werevu kila aina.
34 Naye amemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani.
35 Amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.
Maandiko matakatifu yanaonyesha kuwa akili
za Mungu hazichunguziki na watu waliookoka kama watoto wa Mungu wanatakiwa
watumie akili zao. Maandiko pia yanasema Mungu ni Mungu mwenye nguvu msifuni
kwa akili; kumbe hata kumsifu Mungu kunahitaji
akili. Leo Mungu afungue akili yako ili maisha yako pia yafunguke kwa kuwa kuna
baadhi ya majibu kuhusu maisha yako yamo kwenye akili zako.
Wachawi wanatuonea wivu kwamba tuna akili
ambayo ndani yake tunapata baadhi ya majibu kuhusu maisha yetu. Hatuhitaji
kumuomba Mungu kwa habari ya mambo hayo wala kumtegemea mtu mwingine. Ukimtegemea mtu utakufa masikini ndio maana
Paulo anawaandikia wagalatia kwamba enyi wagalatia msio na akili ninani
aliyewaloga? Akili zilizorogwa pia zinaitwa akili zilizotiwa giza.
Waefeso 4
17 Basi nasema neno hili, tena
nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika
ubatili wa nia zao;
18 ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao;
19 ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani.
20 Bali ninyi, sivyo mlivyojifunza Kristo;
18 ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao;
19 ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani.
20 Bali ninyi, sivyo mlivyojifunza Kristo;
Mungu alipomuumba mtu alimuumba katika
vipande vitatu;
1.Roho
2.Mwlili
3.Nafsi
kuna kitengo cha nia ambapo mtu anajaza elimu. Pia kuna eneo la hisia na
utashi. Pia kuna eneo la akili. Ndio maana
unaweza kukuta ambaye hajasoma lakini
ana mafanikio makubwa.
Farao
alipotaka kushindana na Musa aliwaita watu wenye akili, wachawi na waganga. Hii
inatuonyesha kwamba kumbe wenye akili ni tofauti na wachawi na waganga. Nebukadreza
naye alikuwa anaita wenye akili, wachawi, na waganga sababu alikuwa anajua
akili inaweza kutumika kama uchawi utashindwa. Kila mtu unayemwona amepewa
akili na Mungu, wapo watu ambao hutuma mashetani ili kufunga akili za watu wengine.
Hapo ndio unakuta mtu anashindwa kufanya jambo kwasababu akili zake zimefungwa.
Akili ni jambo la muhimu sana kwenye maisha ya mtu. Mungu
amekupa akili za kumtosha mkeo na familia yako. Zinapokuwa nyingi kulitosha taifa ndipo
unapofaa kuwa kiongozi. Leo kuna viongozi ambao wana akili zisizowatosha hata
wao wenyewe.
Shetani sio muumbaji bali yeye huiba na
kutumia vibaya vitu alivyoumba Mungu. Hivyo wachawi ambao ni wakala wa shetani
wanaweza kuiba akili aliyokuwekea Mungu na kukuwekea jini au pepo kuja kukaa
ndani yako. Hapo ndipo utakuta kama wewe ni mwanafunzi ukiingia darasani
huelewi. Akili yako imerogwa.
Zaburi 147
5 Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa
nguvu, Akili zake hazina mpaka.
6 Bwana huwategemeza wenye upole, Huwaangusha chini wenye jeuri.
6 Bwana huwategemeza wenye upole, Huwaangusha chini wenye jeuri.
2Samweli 14: 2 Yoabu
akatuma watu waende Tekoa, akaleta kutoka huko mwanamke mwenye akili,
akamwambia, Nakusihi, ujifanye kama unakaa matanga, ukavae nguo za kufiwa,
nakusihi, wala usijitie mafuta, ila ukafanane na mwanamke aliyeomboleza siku
nyingi kwa ajili yake aliyefariki;
20 mtumwa wako Yoabu ameyatenda haya ili kubadili uso wa jambo hili; na
bwana wangu anayo akili, kama akili ya malaika wa Mungu, hata ajue mambo yote
ya duniani.
Yoabu anasema mfalme Daudi anayo akili kama
ya malaika wa Mungu kujua mambo. Kumbe hata malaika nao wana akili. Mfalme kabla
hajafa akamwambia mwanae Suleiman amtendee kwa akili Yoabu, aliyekuwa mkuu wa
majeshi ili aweze kutawala vizuri. Daudi alipofariki Sulemani alishika madaraka
akijua kuwa anatakiwa kumtendea kwa akili
Yoabu. Siku moja Suleiman akaagiza aitiwe Yoabu; Yoabu akaogopa akijua mfalme anataka kumuua akakimbilia hekaluni
kushikilia pembe ya madhabahu. Kwa desturi za wayahudi wakati ule kumuua mtu aliyeshikilia pembe ya madhabahu ni laana.
Yoabu akaenda kushika kwenye madhabahu ya Bwana akisema nitafia hapahapa kwenye
madhabahu ya bwana. Mfalme akasema kwa kuwa
amesema atafia kwenye madhabahu basi muueni kama alivyosema, Yoabu akala
matunda ya kinywa chake.
Yesu akasema, “ mpende bwana Mungu wako kwa
moyo wako wote na kwa akili yako yote.”
Kumbe hata Bwana anapendwa kwa akili zetu. Kina Shedrack, Meshack, na
Abednego walichukuliwa ili walishwe vizuri na kulelewa vizuri ili akili zao
zitumike. Jambo lilipokuwa likitokea walikuwa wanafuatwa kutoa ufafanuzi kwa
akili zao. Biblia inasema mwana wa Adamu amekuja naye ametupa akili.
Utakuta mtu anaangalia televisheni kuanzia
asubuhi mpaka jioni halafu analalamika serikali haiangalii watu wa chini, akili
yake imelogwa. Utakuta mahali mtu kaanzisha biashara kesho mwingine anakuja
pembeni yake na kuanzisha biashara ileile na mwingine na mwingine mpaka inafika
hatua wote hawana wateja. Hawa watu wana tatizo na tatizo lao liko kwenye
akili.
Shetani anapoona una akili na anaamua
kuifunga akili yako. Unakutana na mtu anaishi maisha mabaya ukimuuliza
anakwambia haina shida bora uzima. Au unakutana na mwanamke ukimuuliza anafanya
kazi gani anakujibu ni mama wa nyumbani, ukiuliza kwa muda gani anajibu kwa
ujasiri kwa miaka kumi. Ama unaongea na kijana wa miaka 50, hajaoa na haoni
shida kusema bado anajipanga. Huyu akili zake zimelogwa.
Kuna wachawi wanaochukua akili ya mtu na kuitumia
na mahali pa akili wanabakiza mashetani ambayo yanamfanya anakuwa na laana na
mikosi.
Mithali 12
8 Mtu atasifiwa kwa kadiri ya akili
zake; Bali mwenye moyo wa ukaidi atadharauliwa.
Mtu anasifiwa kwa jinsi akili yake ilivyo.
Mchawi anapochukua akili yako vile vitu unavyotakiwa kuvifanya unashindwa. Utakuta mtu akianza
kusoma kichwa kinauma au anasinzia kumbe akili yake imechukuliwa na inatumiwa mahali fulani.
Au mtu ni mgonjwa lakini chanzo cha ugonjwa wake ni akili kuchukuliwa.
Kama malaika wana akili na sisi lazima tuwe
na akili kama Mungu ana akili na akili zake hazichunguziki kwa nini sisi tulio
watoto wake tusiwe na akili? Lazima akili zetu zirudi kwa jina la Yesu.
Mtu mwingine anasema wameniloga nisipendwe,
nisisafiri, nisipate kazi lakini sio kwamba wamekuloga wamechukua akili, mawazo
unayowaza ndivyo ulivyo.na Wanafilosofia wanasema angalia sana unachokiwaza
kuna siku utakisema. Angalia sana unachokisema kuna siku utakitenda. Angalia
sana unachokitenda kuna siku kitakuwa tabia. Angalia sana tabia yako kuna siku
itakuwa asili yako. Asili ya mtu hujalisha mwisho wake utakuwaje. Hebu jiulize
hapo ulipo una mpango gani wa maendeleo? Utasema labda sina mpango kwa sababu
sina mtaji. Lakini kwa kawaida unatakiwa uanze kuwa na mpango halafu ndipo
upate mtaji ila kwa sababu akili yako imelogwa ndio maana unasubiri upate mtaji
ndio upange mpango.
Akili yako inapolazwa ndio wale tunaowaita
usingizi wa kiroho ingawa unaona lakini umelala usingizi kwenye akili. Huu sio
wakati wa kushangilia ametajirika ni wakati wa kuwaza ameupata wapi utajiri
ule. Si wakati wa kushangilia ameshinda uongozi, ni wakati wa kuwaza ameupata
wapi uongozi ule. Lazima turudishe akili zetu zote zilizoibiwa kwa jina la
Yesu, ni wakati wa kuanza kuitumia akili yako ili kuinua familia yako,ni wakati
wa kutumia akili tuliyopewa na Mungu kutimiza kusudi lake kwenye maisha yetu kwa
jina la Yesu
Ndani yako unahisi unaweza kufanya zaidi ya
hapo, ni kweli ila kuna mahali wameitafuna akili yako na wamekuloga ili
waitumie mahali. Yamkini akili yako inatumika kuzaa watoto wa kijini baharini
lakini akili hiyohiyo ingetumika kuwafanya watu waokoke. Wanapoiiba akili yako
wanakuvisha akili ya uoga na kuondoa ile akili ya ujasiri uliyoumbiwa. Kataa
uoga ulionao kwa jina la Yesu kwa sababu hiyo sio asili yako.
MAOMBI:
Kwa jina la Yesu mtu yeyote aliyechukua
akili yangu akanifunga na magonjwa ninaamuru rudisha akili yangu kwa jina la
Yesu; akili ya biashara, akili ya kusimamia miradi, akili ya kujenga kanisa,
akili za kusafiri rudisha kwa jina la Yesu. Umenijia kwa uchawi nakujia kwa
jina la Bwana wa majeshi, akili njooo kwa jina la Yesu.
Kwa jina la Yesu wale waliotafuna akili
yangu ninawaamuru waitapike akili yangu kwa jina la Yesu . Akili yangu iliyofungiwa
shimoni njoo kwa jina la Yesu, naishinda akili ya uoga kwa jina la Yesu. Kwa
jina la Yesu naamuru akili yangu njoo, akili ya biashara, akili ya ubunifu,
akili ya fedha,njoo kwa jina la Yesu. Mtu yeyote anayetumia akili yangu naamuru
achia akili yangu kwa jina la Yesu, akili ya kuanza biashara , akili ya kufanya
kazi, akili ya kubuni njoo kwa jina la Yesu. Napokonya akili kwa jina la Yesu,
nakunyanganya akili yangu kwa jina la Yesu; uliyemeza akili yangu nakutapisha
kwa jina la Yesu. Ewe mkurugenzi uliyemeza masomo yangu nakutapisha kwa jina la
Yesu, ewe uliyemeza akili yangu ya ubunifu nakunyanganya kwa kwa jina la Yesu,
akili ya kusafiri, akili ya kuongea, akili ya kutenda njoo kwa jina la Yesu. Akili
iliyoko mapangoni, mashimoni, baharini njoo kwa jina la Yesu, akili ya miradi,
akili ya kuanzisha makampuni, akili ya kumtumikia Mungu njoo kwa jina la Yesu.
Rudisha akili yangu kwa jina la Yesu, akili inayotumiwa na majini kutengeneza
bacteria na virusi wa magonjwa nashindana nanyi kwa jina la Yesu. Akili ya
kubuni miradi akili ya kuita miradi, akili ya kuota kazi njooo kwa jina la Yesu.
Akili ya kujua cha kufanya , akili ya kujua cha kutenda njoo kwa jina la Yesu.
Ninaifungua akili yangu kwa jina la Yesu, ninawashambulia mashetani wote na
wachawi wote mnaoishikiila akili yangu
kwa jina la Yesu, akili yangu inayotumika mahala popote ninairudisha kwa jina la Yesu. Naondoa akili
za kishetani na magonjwa yote yaliyowekwa ndani yangu kwa jina la Yesu, vifungo
vya akili ninavifungua kwa jina la Yesu.
Ameni.
Comments