HAKUNA FULISH AGE KWA WALIOMWAMINI YESU

Na Godfrey Miyonjo.
NENO LA UPONYAJI KWA VIJANA.
"HAKUNA FULISH AGE KWA WALIOMWAMINI YESU"

Shetani ni mdanganyifu sana, yeye ni mwongo tena ni baba wa huo, anawadanganya vijana eti kuna umri wa kufanya uchafu, kitu ambacho siyo kweli.

Biblia inatutaka tuwe waaminifu hata kufa, pia inasema kuwa dhambi ya uasi ni kama dhambi ya uchawi.

Biblia inatufunza mengi kupitia watumishi wa MUNGU ambao walimtumikia MUNGU tokea udogo wao.
Wapo akina Yeremia, Danieli, Yosia, n.k.

Hawa watu ukisoma habari zao hauwezi kukuta sehemu imeandikwa "eti waliasi katika kipindi cha fulish age"

Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; akatawala miaka thelathini na mmoja katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Yedia, binti Adaya wa Bozkathi. Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, akaenda katika njia yote ya Daudi baba yake, wala hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto 2 FALME 22:1-2 ''Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; akatawala miaka thelathini na mmoja katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Yedida, binti Adaya wa Bozkathi.  Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, akaenda katika njia yote ya Daudi baba yake, wala hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto.   ''

CHONDE CHONDE KIJANA, USITENDE DHAMBI KWA KISINGIZIO KUWA UPO KATIKA "FULISH AGE", KWANI WATENDA DHAMBI WOTE HAWAENDI MBINGUNI.
MUNGU akubariki sana.
By Geofrey Miyonjo.

Comments