KANISA LA JESUS DELIVERANCE CENTRE LAANDAA SIKU 15 ZA OPARESHENI FUTA MACHOZI - TEGETA DAR ES SALAAM


Mchungaji Evarist T. Shabani wa kanisa la Jesus Deliverance Centre akishirikiana na watumishi wengine ameaanda mkutano mkubwa kanisani kwake Tegeta wa siku 15 za Oparesheni Futa Machozi. Mkutano huu utahubiriwa na watumishi wa Mungu wanne Dr. Wilfred Uhuru kutoka Kenya, Mch. Jeofrey Ngereje kutoka Tanzania, Apostle Joshua Tumba kutoka Kenya na mwenyeji Mch. Evarist T. Shaban ambao wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kile walichotumwa na Bwana kwaajili yako kinakufikia na kibadilishe maisha yako.

Mch. Evarist T. Shaban

Watu wengi wamekuwa wakitoa machozi kutokana na majaribu wanayopitia ya kimaisha, lakini leo watumishi wa Mungu wamefanya maombi kwa Mungu ili siku ya mkutano huu hayo amachozi ambayo umekuwa ukiyatoa kutoka na maumivu ya moyo na pengine magonjwa yatakwenda kuvutwa kwa damu ya Yesu Kristo. Kazi kubwa uliyonayo wewe mwenye kutoa machozi ni kutenga muda wako wa kufika eneo hilo na ukiwa na imani ya kwamba Mungu wa mbinguni anakwenda kufuata machozi yako kwa kupitia watumishi wake aliowachagua kwa kazi hii ya kumtumikia.Yawezekana umezunguka sana kutafuta majibu yako na ikashindikana, ukaamua kukata tamaa, lakini nataka kukuambia ya kwamba huu ni wakati wako wa kupokea baraka za Mungu. Unachotakiwa ni kujitakasa na kuishi kama vile Mungu anavyotaka uishi, tumia muda mwingi kusoma Neno la Mungu na kufuata kile anachokuambia kwa kupitia Neno lake. Acha kuchanganya Imani yako na imani zingine potofu.


Tunakuomba sana katika mkutano huu uje na marafiki zako na ndugu zako ili waweze kupokea baraka za Mungu na washuhudie utakavyompokea huyu Yesu Kristo ambaye atafanyika kama kitambaa cha kufuta machozi yako ya taabu za hapa duniani. Katika mkutano huu kutakuwa na waimbaji mbalimbali kama Stara Thomas, Atosha Kissava, Grace Rwegasha, Leah Amos, Sarah Mvungi na Zacharia Kenyatta. Mungu wangu na akubariki sana

Comments