KANISA LA MWANSASU KUFUNGUA CHUO CHA BIBLIA.

Mchungaji na mwimbaji wa nyimbo za injili, Ephraim Mwansasu ambaye pia ni mwanzilishi wa huduma hiyo akitoa historia fupi ya kituo hicho.
DIWANI wa Kata ya Kigogo, Richard Chengula ameongoza mamia ya waumini na wageni waalikwa katika harambee ya kuchangia huduma ya kituo cha Hosanna Life Mission kwa ajili ya kufungua chuo cha biblia wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Bw. Chengula alimwakilisha meya wa manispaa ya Kinondoni ambaye alishindwa kuhudhuria kutokana na sababu ambazo hazikuelezwa.

Harambee hiyo imefanyika leo katika moja ya tawi la kituo cha huduma ya Hosanna kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam.




Baadhi ya waumini wa kituo cha Hosana wakiwa kanisani.




Kanisa la kituo cha huduma cha Hosana Life Mission.

Muonekana wa meza kuu wakisikiliza jambo.

Diwani wa Kata ya Kigogo, Richard Chengula aliyemwakilisha mgeni rasmi meya wa manispaa ya Kinondoni.

Watumishi wa kituo wakiandika majina na ahadi za harambee hiyo.

Ofisa Habari Victoria Mungure akisoma risala.

Ofisa Habari wa wa kituo hicho, Vick akimkabidhi risala mgeni rasmi.

Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza mchungaji Mwansansu.

Comments