NA MCHUNGAJI KIONGOZI: JOSEPHAT GWAJIMA,Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe |
Watu wengi wanadhani Mungu ana nguvu na ana
uwezo na ni muumbaji lakini wamesahau ana akili ameumba kwa akili na wale
wanaomuabudu wana akili
ZABURI
147: 5.
5 Bwana
wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka.
Tunaanza kuona Mungu ana akili na akili
zake hazina mipaka wala hazichunguziki.
Sasa kuna kifungo ambacho unaweza kumwona
mtu yuko vizuri lakini akili yake imefungwa. Sasa kwanini Mungu ametupa akili
ni kwasababu kuna mambo mengine tunaweza kuyafanya kwa akili. Unaweza kumshuhudia
mtu anakwambia jambo mpaka uka mshangaa jambo hilo hawezi kulifanya kwa akili ndio
maana Mungu alivyowaumba watu akaweka mambo mengine tusimsumbue ila tutumie
akili zetu. Shetani
naye anawafunga watu akili ndio maana ya kifungo cha akili.
Ndio maana akili ya mahesabu ni tofauti na akili ya maisha na akili ya kufanyia
bihashara nitofauti na akili ya kufanyia akaunti shuleni. Unaweza ukamkuta mtu
anajua mahesabu lakini hana akili ya kuendesha kampuni.
Unamkuta mtu anaakili ya darasani na
amekosa akili ya kutunza familia yake na ndio maana imeandikwa “enyi waume
ishini na wake zenu kwa akili” unakuta mtu anaakili ya bihashara lakini hana
akili ya kutunza familia yake na leo watu wa namna hiyo wanatakiwa wawe na
akili kwa jina la Yesu. Mungu yupo kila mahali, kila sehemu kila mahali
ulimwenguni kote na AKILI ZAKE HAZICHUNGUZIKI. Kama Mungu ana akili na akili zake
hazichunguziki na amekuzaa wewe maana yake ulipompokea Yesu ukazaliwa mara ya
pili baada ya kuzaliwa na wazazi wa mwili ukazaliwa kwa Damu ya mwanakondoo
kwanini aliyekuzaa awe na akili alafu wewe usiwe na akili? lazima uwe na akili
kama Mungu alivyo na akili. Imeandikwa “kila kilichozaliwa na Mungu huushinda
ulimwengu” maana yake tunaamua kama Baba yetu, tuna rudisha kama Baba yetu, tu
kama Baba yetu Mungu wa Mbinguni na sisi aliyetuzaa tuna asili yake.
Kuna baadhi ya majibu yako ndani ya akili
yako. Ndio maana wazungu wanakuja Afrika kutuchezea kama toy wanatuletea miradi
isiyo na maana ni kwasababu wana akili ndio maana imeandikwa kwenye Biblia enyi
wagalatia msio na akili ni nani aliye waloga?!
Mithali 3:19
19 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi
ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;
Kuna watu wakianza kufikiria mambo ya maana
wanaumwa akili na wengine wanahela mkonononi lakini hawajui jinsi ya kizitumia
na kuna watu wanatumia akili za watu kufikiria na kufanya maamuzi na wengine
wameibiwa akili zao hawawezi kufanya mambo ya kimaendeleo. Wengine wanasema
eneo la thamani kubwa ni kaburini ambapo zimelala nyimbo ambazo
hazikuimbwa, kuna mahubiri yamelala
ambayo haya kuhubiriwa, kuna ndege zimelala ambazo hazikutengenezwa.
Isaya 40:28
28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye
Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili
zake hazichunguziki.
Wachawi wanaweza kumloga mtu akili yake na
uchawi ni akili ya kishetani ambayo unafanya kazi ya kuzuia akili za watu.
Wagalatia 3:1-
1 Enyi Wagalatia msio na akili, ni
nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya
kuwa amesulibiwa?
Kadiri unapozidi kupata maarifa unazidi
kujijazia uoga maarifa kama ya kadiri unavyozidi kusoma unapatwa na uoga Fulani
mfano ulipokuwa kijijini ulikuwa unakunywa maji ya kisima lakini sasa hivi
unajua kuna backteria. Magonjwa duniani
yamegawanyika katika makundi mawili; magonjwa ya bacteria na virusi na yote
yanaweza kusikia sauti ya Bwana Yesu kristo yakaambiwa ondoka nayaka ondoka na
backteria yanaweza kutibika na virusi ndio hayawezi kutibika. Kuna backteria wazuri
kama wale wanaogandisha maziwa yanganda lakini hawana madhara ni viumbe na
tumepewa akili ya kuvitambua na kuviondoa kwenye miili yetu kwa jina la Yesu. Ndiomaana
mfalme wa misri alipokuwa akipatwa na matatizo alikuwa anaita watu wa aina tatu
wenye akili, wachawi, na waganga.
Kutoka 7:11
11 Ndipo Farao naye akawaita wenye
akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.
Wenye akili wanauwezo kuliko wachawi na
waganga, akili ya kumwambia mtu jambo akalifahamu na kukubaliana nalo hiyo ni
akili ya mtu. Unakuta mtu anatakiwa kuolewa na unamwona mtu hajawahi kunena na
haonekani mkesha na hata kwenye ministry hayupo lakini ana gari zuri na kazi
nzuri hapo hauhitaji maombi wala kumuuliza Bwana hapo unatakiwa utumie akili.
Biblia inasema mtu akizaliwa akaishi miaka mia asipate chakula kizuri na
asiishi vizuri ni afadhali mimba iliyoharibika. Mfano kipepeo anarangi nzuri
lakini alianza yai akaja buu ambalo ni funza linaelekea kuwa kipepeo sasa watu
wanaogopa buu, wanashindwa kupigana ili wafanikiwe. Maisha ni vita ya kupigana
ili tupate kushinda. Naamuru kwa jina la
Yesu akili yangu iachiwe.
Kutoka 35:35
35 Amewajaza watu hao akili za moyoni,
ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu,
na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya
zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao
wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.Mungu alikuwa anamwambia Musa katikati yako nimewaweka watu wenye akili wanaoweza kufanya mambo makubwa.
Kumbukumbu ya torati 1:15
15 Basi nikatwaa vichwa vya kabila zenu wenye akili, waliojulikana, nikawafanya wawe vichwa juu yenu, maakida ya elfu elfu, na maakida ya mia mia, na maakida ya hamsini hamsini, na maakida ya kumi kumi, na wenye amri, kwa kadiri ya kabila zenu.
Kila mtu ni baunsa wa kitu fulani kwenye maisha, na pale ambapo mwanadamu amekufa na akili yake imelaza vitu ambavyo havijatokea. Biblia inasema Watu wanaomjua Mungu wao watakuwa hodari watatenda mambo makuu.
1 MAMBO YA NYAKATI12:32
32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye
akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao
walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
Mungu alipokuumba wewe aliweka akili ndani
uitumie wewe na kutatua matatizo yako. Adui mkubwa wa mafanikio yako ni
mafanikio yako ya leo, unapofanikiwa leo usiridhike mwambie Mungu nimefanikiwa
kwanza nataka nitende tena zaidi. Kama rohoni
mtu yupo vizuri ukimsikiliza mtu unajua mtu huyu atafika mbali. Wachawi wanakuja
kwenye kichwa chako wakati umelala
wanaona kuna kiongozi mkubwa wa taifa yupo hapa na wanachukua hiyo akili ya
uongozi wanaenda kuweka kwa mwanasiasa Fulani ndio maana mtu unamrudisha
anakwambia nilikuwa Bungeni nyuma ya kiti
cha spika anasema alikuwa anamsaidia spika asiumbuke maana yake alipewa
akili ya kuendesha Bunge, lakini sasa watu wa dunia hii wanakuja kuichuka akili
ya mtu anayetakiwa kuwa spika anaendesha bodaboda kwanini? Ni kwasababu
wameichukua akili yake wanaitumia mahali, alafu wewe utajuaje sasa kama akili
yako inatumiwa sehemu
1.
Akili yako inapanga mipango
ambayo wewe hutaki na hujawahi kuwaza kuifanya, Mipango inayopangwa kule kwenye
akili yako inakujia na wewe umekaa na hujawahi kufanya hiyo unayoiwaza na
huwezi jua kwamba akili yako inatumika mahali wamekunyanganya kile
kinachokusaidia kutembea kwenye mafanikio yako. Shetani anatumia akili za watu
walizopewa na Mungu kuendesha dunia hii atakavyo
2.
Kuna mtu amefunga akili yako
hii ni pale unapoanza kupanga mipango ya maendeleo kichwa kinauma na unashindwa
kuendelea kufikiria na hakuna nchi kavu ila kuna akili kavu na kama
hujafanikiwa usimtafute mtu wa kumlaumu bali unatakiwa umwambie Bwana aifungue
akili yako uitumie kuendelea. Unachotakiwa kuwa nacho kiko ndani ya kichwa
chako hakiko mbinguni unatakiwa uombe naondoa giza lililotanda kwenye akili
yangu.
Shule inaongoza akili ya mtu ili aweze
kufanya jambo Fulani na sio inayoweza kumpa mtu uwezo wa kufanya jambo mfano
magari haya yanayoonekana leo ni kwa kutumia akili ya mtu. Kataa kukaa pale
ulipo na kuridhika uanze kwa kile kidogo ulicho nacho kwa kutumia akili. Mfano
mwanzilishi wa kampuni ya Samsung kule korea ya kusini kama angekufa kabla
hajatoa simu ungeenda kule kaburini kwake ungeona simu zote zimelala kaburini
kama una macho ya rohoni. Sio kiwango cha elimu ndio kinakutambulisha wewe
ninani bali ni akili ile uliyo nayo ndio inayokutabulisha, lakini kuna
mashetani maalum ambayo yanakuja kushikilia akili ya mtu na lazima yatoke kwa
jina la Yesu.
Kwa mamlaka ya Jina la Yesu ninaamuru akili
yangu ilinayotumiwa na waganga achia kwa jina la Yesu akili yangu irudi, akili
inayotumika mahali Fulani ninaamuru akili yangu irudi kwa jina la Yesu, akili
yenye mipango ya kujenga kiwanda achilia kwa jina la Yesu, akili ya kusimamia
kampuni ninaamuru irudi kwa jina la Yesu, wale wanaoilinda akili yangu
isisimame ninaamuru waachie kwa jina la Yesu. Sehemu yeyote ambapo akili yangu
inatumika ninaamuru waachie kwa jina la Yesu, ninrudisha akili yangu kwa jina
la Yesu na wale wanaochukua akili yangu ninawafyeka kwa jia la Yesu. Akili
iliyozuiwa na wachawi na mashetani niniachilia kwa jina la Yesu. Ninaamuru kwa
jina la Yesu wale wanaotumia akili yangu
mahala popote ninawafyeka kwa jina la Yesu ninasimama kinyume na mjenzi yeyote
anayetumia akili ya mtu kujenga utawala wake kujenga ninawateketeza kwa jina la
Yesu, ile akili iliyojenga miji ya kishetani ninapindua kwa jina la Yesu. Akili
inayowaza mambo ya mafanikio naamuru iamke kwa jina la Yesu. Imeandikwa watu
hawa ni ‘watu walioibiwa na kutekwa’ ninaamuru akili iliyoibiwa irudi kwa jina
la Yesu kristo kwa damu ya Yesu. Katika jina la Yesu nabomoa ngome inayozuia
akili kwa damu ya Yesu. Naondoa wigo uliowekwa kwenye akili yangu kwa jina la
Yesu, naondoa wigo wa hofu, naondoa wingi wa mashaka kwa damu ya Yesu.
Ninabomoa madhabahu zao zinazoshikilia akili kwa damu ya Yesu. Akili ya kujua
kitu cha kufanya, akili ya kufanya maamuzi, akili ya kuanzisha bihashara akili
ya kujenga kiwanda, akili ya mipango, akili ya kufanya biashara ifunguke kwa
jina la Yesu, akili ya ubunifu iamke kwa jina la Yesu, kifungo cha akili, kufa
mipango naivunja mipango ya kishetani kwa jina la Yesu, akili za kishetani
nazivunja kwa jina la Yesu.
Asante Mungu Baba, asante Bwana Yesu asante
Yesu kwa kunipa akili asante Yesu kwa kunipa akili kwa jina la Yesu.
![]() |
Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe |
AMEN.
Comments