KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA.

 Na Kabalama Masatu


BWANA yesu asifiweeee.......
Leo tujifunze somo hili...
Mlango-Ni sehemu katika nyumba inayokuwezesha kupita ili uingie ndani au tukoke.
Mtu yeyote mwenye kuingia ndani ni lazima apite mlangoni kama ikitokea akapita sehemu nyingine tofauti na mlangoni basi huyo hatakuwa na makusudi mazuri kwako.
Kama ukienda kwa mtu na kukuta malango umefungwa basi hautaweza kabisa kuingia na badala yake utakomea nje.
Sasa leo,Bwana Yesu anataka kufungua milango yote iliyofungwa na kutusababisha tusiingie katika mafanikio.
Katika Ufunuo3:8 imeandikwa:-
"Nayajua matendo yako.Tazama,nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako,ambao hapana awezaye kuufunga,kwa kuwa unazo nguvu kidogo,nawe umelitunza neno langu,wala hukulikana jina langu".
Alleluyaaaa.......
Maandiko yanazungumza juu ya mlango ulio mbele yako,ambao hakuna awezaye kuufunga.
Mungu mwenyewe ametoa mlango uliyo wazi kabisa kwa kila mtu mwenye kufuata maneno yake.
Mtu huyu ndiye aliyepewa neema hii ya pekee.
Ili baraka za Mungu zije kwako ni lazima kwanza mlango wako uwe wazi.
Ili ufanikiwe katika maisha yako ni lazima kwanza mlango wako uwe wazi.

Ili upate upenyo wa kufahulu katika mipango yako ni lazima kwanza mlango wako uwe wazi.
Iko hivi; Kama mlango wa nyumba yako umefungwa na huna uwezo(funguo) za kuufungua huo mlango basi uwe na uhakika wa kukaa hapo mpaka pale aliyefunga atakapoamua kukufungulia ndipo utapata nafasi ya kuingia.
Vivyo hivyo kama mlango wako wa mafanikio umefungwa na shetani basi itakulazimu ukae katika mateso mpaka pale atakapo kuja mwenye nguvu kukufungulia.

Maisha ya watu wengi yapo katika mateso na dhiki ingawa wameokoka;milango yao ya upenyo bado imefungwa na wao hawajajua ni kwa nini wako katika mateso hayo.
Leo Mungu anataka uchukue hatua ya kufungua mlango wako wa mafanikio.
Chunguza ni wapi pamefungwa,chunguza misingi yako...........














 Ufunuo3:8:-
"Nayajua matendo yako.Tazama,nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako,ambao hapana awezaye kuufunga,kwa kuwa unazo nguvu kidogo,nawe umelitunza neno langu,wala hukulikana jina langu".

Alleluyaaaaa........

Maandiko yanathibitisha juu ya uwepo wa mlango uliofunguliwa mbele yako;ambao hapana awezaye kuufunga.
Ili mlango wako uendelee kuwa wazi siku zote ni lazima kwanza uwe na mamlaka juu ya nyumba yako;kama hauna mamlaka na nyumba yako basi ni wazi kwamba kila mtu anao uwezo wa kufunga nyumba yako na kukuzuia wewe usiingie.

Kwa habari ya mlango wako wa mafanikio (upenyo) ni lazima kwanza utambue msingi wako.

Pamoja na kuokoka,kama bado hujachunguza msingi wako basi itakupa shida sana kupata upenyo wa mafanikio katika ulimwengu wa roho maana msingi wako unaweza kusimama kama mlango ambao umefungwa na hivyo kukosa nafasi ya kuingia ndani.

Msingi ni asili/chanzo/chimbuko la mtu/kitu fulani.

Unaweza ukakuta chimbuko la ukoo ilikuwa ni kufanya matambiko na kwenda kuabudu sanamu na kipindi hicho wewe ulikuwepo ingawa ulikuwa hujazaliwa.
Unajua mwanadamu ni mtu hata kabla hajazaliwa.

Unanielewa?

Iko hivi;

Mtu huwa kwenye ile mbegu ya uhai iliyoko katika viuno vya baba yake;anakuwa binadamu baada ya kutengenezewa mwili anapofika katika tumbo la mama na kuishi pale miezi tisa.

Unalielewa jambo hili?

Sasa kama ufunuo3:8 inasema nimekupa mlango uliyofunguliwa mbele yako;sasa ni kwa nini bado uko chini kimaisha...........?!!

Ukifuatilia misingi yako ndipo utaelewa ya kwamba pengine mlango wa mafanikio ulifungwa hata kabla wewe kuzaliwa na wewe ulipozaliwa na kukua ukasikia injili ukaamua kuokoka ukadhani mambo yamekwisha;mimi nakwambia bado hayajaisha ni lazima utambue ni patano gani liliwekwa na wazazi wako huko nyuma......
ITAENDELEA KATIKA SEHEMU YA TATU..........
0753-305957;
0789-628226;
0717-624035.

Comments