KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA.(Sehemu ya mwisho)

 Na Kabalama Masatu

Bwana Yesu asifiweee.....
Alleluyaaa........
Msingi wa somo tunaupata katika ufunuo3:8.
Ilipoishia.....
Ulipookoka ukadhani mambo yamekwisha;lakini mimi nakwambia bado hayajaisha ni lazima utambue ni patano gani liliwekwa na wazazi wako.

Endelea........

Ukisoma Mwanzo14:17-20;

Waebrania7:9-10 utaona maandiko yanaeleza kuwa Ibrahimu alikutana na Melkizedeki alipokuwa anatoka kumkomboa Luthu nduguye; na akampa sehemu ya kumi ya mali zote na hivyo Lawi naye akashiriki tendo hilo la kutoa zaka.

Jiulize sasa Lawi ameshiriki vipi?
Labda nikwambie hivi kipindi hicho Lawi alikuwa hajafikiriwa kuzaliwa maana hata Isaka ambaye ni babu yake Lawi alikuwa hajazaliwa,maana Ibrahimu alimzaa Isaka,Isaka akamzaa Yakobo na Yakobo ndiye akamzaa Lawi.


Kwa hiyo Ibrahimu kwa Lawi ni babu wa pili.
Hebu fikiri jambo hili;Lawi anatoa sehemu ya kumi akiwa katika viuno vya Ibrahimu.


Hili ni jambo la kutafakari sana pale tunapotafuta upenyo wa kufungua milango iliyowekwa na Mungu lakini ikafungwa na adui na hivyo kusababisha mambo yetu yasifanikiwe.
Kama Ibrahimu angeshiriki ouvu kwa kipindi hicho basi ni wazi kwamba hata Lawi angekuwa ameshiriki huo uovu akiwa katika viuno vya Ibrahimu.


Kama Lawi alishiriki jambo jema la kutoa fungu la kumi;vivyo hivyo mtu anaweza pia kushiriki matendo mabaya akiwa katika viuno vya baba yake.


Kumbuka mbegu ya mtu ni memory card ya maisha yake,hutunza vitu vitakavyomtokea huyu mtu toka kizazi na kizazi hivyo huwezi kuwa tofauti na kizazi chako ulikozaliwa mpaka uhamishe mtandao wako toka misingi mibovu ya vizazi na kuikabidhi itawaliwe na Mungu mwenye mema yote kwa ajili yako.
Sasa unisikilize kwa makini;
Zaburi11:3 imeandikwa:-
"Kama misingi ikiharibika mwenye haki atafanya nini?"
mwimba Zaburi anatambua shida ya misingi mibovu inavyoweza kukwamisha mlango wako wa mafanikio;sasa anasema je,mwenye haki afanye nini?
Dawa ya misingi mibovu ni sisi kujihamisha na kujiweka mahali pa neema ya Mungu wetu.
MWISHO.

 0753-305957;
0789-628226;
0717-624035.

Comments