Na AP Hosea Shabban akihubiri, Ufufuo na Uzima Moshi Kilimanjaro. |
Mithali 1:7, Mith 8:13, Mith
9:10, Mith 14:26,
Tunahitaji maaarifa katika
utendaji wote wa kazi zetu na zaidi sana Kazi ya Bwana. Na maandiko
yanatuambia;
“Kumcha
Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu “
Ni kweli kwamba tunaweza
kupata maarifa kwa kuwaangilia watu wengine namna wanavyotenda, kwa kuwaangalia
waliotutangulia lakini biblia imetuelezea KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA MAARIFA.
Tukiisha kujua kumcha Bwana
ndio chanzo cha maarifa sasa tunamchaje Bwana?
Jibu ni Tunamcha Bwana Kwa kuchukia
uovu.
Tunapomcha Bwana, tunapewa
maarifa ya Kimungu yanayotuwezesha kukabiliana na changamoto au matatizo
mbalimbali. Maarifa haya yatatuongoza kunena kwa usahihi, yatatuelekeza namna
ya kutoka kwenye vifungo na matatizo tuliyoshikiliwa kwayo. Ili tuweze kuitenda
kazi ya Mungu kwa usahihi tunayahitaji maarifa haya.
Maandiko mengine yametueleza
wamba, Kumcha Bwana kwaongeza siku za mtu za kuishi, Kumcha
Bwana ni tumaini imara, Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na
tanzi za mauti.
Ni maombi yangu
kwamba Mungu afanyike chemichemi ya uzima, siku zako za kuishi ziongezeke,
akuepushe na tanzi za mauti, Bwana afanyike tumaini imara kwako wakati
ukiongeza maarifa mengi kwa kumcha Bwana na chochote kilichotengenezwa kwa
kukosa maarifa haya kivunjike, tanzi za magonjwa na kuonewa ziharibike na
ufanikiwe kwa haya Maarifa ya Kimungu Amen.
Hapa chini ni habari picha katika ibada ya juzi ambapo ujumbe huo wa KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA MAARIFA ulifundishwa.
Hapa chini ni habari picha katika ibada ya juzi ambapo ujumbe huo wa KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA MAARIFA ulifundishwa.
Comments