KUMCHA MUNGU NI MUHIMU ZAIDI KWA KIJANA ILI AYAFIKIE MAISHA MAZURI YA NDOA.

BWANA YESU asifiwe!

Ingawa Ni Kweli Kabisa Kwamba Kila Mwanamke/Mwanaume Aliyeumbwa Na MUNGU, Amewekewa Mwanaume/Mwanamke  Wa Kufunga Nae Ndoa, Lakini Unaweza Kuupoteza Mpango Huo Ambao Umewekwa Kwa Ajili Yako Kwa Sababu Ya Tabia. 

Biblia Inasema Hivi Hata Kama Wewe Ni Mzuri Sana Wa Umbo "Mithali 31:30- Upendeleo Hudanganya, Na Uzuri Ni Ubatili; Bali Mwanamke Amchaye BWANA, Ndiye Atakayesifiwa."

Anayemcha MUNGU Ndiye Mzuri Na Muhimu Zaidi. 
Ndugu Yangu Weka Mazingira Vizuri Ili Watu Wakikuona Tu Waseme " Yule Binti Anafaa Kuwa Mke Mwema Wa Mtu". 

-Kuna Msemo Usemao " Utandikavyo Kitanda, Ndivyo Utakavyokilalia" Umetandikaje Kitanda Chako? Yaani Umeishije Katika Miaka Yako Ya Ubinti Ili Upate Mchumba Sahihi?. Je Umetengeneza Au Umeharibu Maisha Yako. Vile Ulivyotenda Ndivyo Ndivyo Utakavyokuwa Wakati Huu Ukihitaji Kijana Wa Kukuchumbia. 

-Ni Vizuri Binti Kubaki Na Bikra Ya Awali Na Hata Bikra Ya Pili Yaani Alipozaliwa Upya Kwa Damu Ya YESU Hakutenda Tena Uzinzi. Ukifanya Hivyo MUNGU Atakubariki Na Utakuwa Unajitengenezea Mazingira Ya Kuolewa.

-Vijana wengi wasiomcha MUNGU hutaka sana kuoa wasichana wacha MUNGU. Ndugu unaweza ukampata mcha MUNGU lakini hiyo haitakuepusha na jehanamu. jambo la kuokoka ni la kila mmoja anayetaka kuishi maisha ya furaha duniani na mbinguni pia.
 KUOKOKA Wala Sio Ombi Mpaka Ubembelezwe, KUOKOKA Ni Amri Tena Ni Sheria Kwa Wewe Tu Ambaye Huitaki Jehanamu. Mpokee YESU KRISTO Leo.
 Biblia inasema ''Tubuni Basi, Mrejee, Ili Dhambi Zenu Zifutwe, Zipate Kuja Nyakati Za Kuburudishwa Kwa Kuwako Kwake BWANA Matendo 3:19

 =Shika pointi hii: Aina Ya Marafiki Ulio Nao, Huashiria Wewe Ni Mtu Wa Aina Gani. Wengi Wameingia Dhambini Kwa Sababu Ya Marafiki. Usikubali Kufungwa Nira Moja Na Marafiki Waasherati Au Wachawi Maana Hata Wewe Utaonekana Mwasherati Au Mchawi Hata Kama Hufanyi Hayo. Wadada Wengi Wameshindwa Kuolewa Kwa Sababu Ya Marafiki Waliotekwa Na Shetani. Maana Kijana Akitaka Kuoa Lazima Aulize Kwanza Mienendo Ya Huyo Binti Na Tabia Yake, Majibu Atakayoyapata Ni Kwamba " Sidhani Kama Huyo Binti Katulia Maana Marafiki Zake Ni Makahaba" Kijana Anaghairi Maana Amekukuta Umebeba Ukahaba Hata Kama Ukahaba Huo Sio Wako Ila Ni Wa Marafiki Zako Uwapendao. Hii Ni Tafakari Ngumu Lakini Ni Nyepesi.

 =Pointi nyingine  ni hii: Madhara Ya Kuwasemasema Watu Ni Haya. Kile Utakachosema Kuhusu Kaka/dada Fulani Sio Tu Kwamba Kitamfikia Yeye Peke Yake, Bali Kitasambaa Kwa Wengine Wengi Ambao Nao Wataanza Kukukwepa Na Wengine Kuapa Kabisa Kutokujihusisha Na Wewe Kwa Njia Yeyote Ile. Na Kwa Sababu Ya Hayo Watu Wengi Wamekosa Sifa Za Kuolewa Au Kuoa Kutoka Kwa Watu Makini Wanaojitambu.

Hakuna mwanadamu aliye kisiwa hivyo kijana  Jifunze Kusikia Kutoka Kwa Watu Wema, Jifunze Huheshimu Watu, Pokea Roho Ya Kunyenyekea. Kataa Kujiinua Pia Kataa Kujiachia Kwa Kila Mtu, Jifunze Kunyenyekea, Salimia Wanaume Na Wanawake Bila Kujali Hali Zao Za Maisha. Ishi Kama MUNGU Apendavyo


 =Nilionalo Mimi Ni Hili; Wadada Wengi Hawapendani, Na Wakaka Wakitaka Kumchumbia Mtu Hupenda Kuulizia Tabia Ya Mlengwa Kwa Watu Wa Karibu. Balaa Ni Kwamba Aulize Mdada Kuhusu Mwenendo Wa Mdada Mwenzake Anayetakiwa Ili Achumbiwe, Utasikia " Huyo Mcharuko Balaa Tena Hafai, Atakusumbua Bure Kakangu" Kumbe Si Kweli. Mnisamehe Ndugu Zangu Lakini Mimi Binafsi Nimeliona Mara Nyingi Sana.

 Kijana hakikisha unaambatana na MWOKOZI YESU KRISTO katika hatua zako zote. Kama una kifungo hakikisha unafunguliwa kwa maombi, maana yapo maagano hata ya kurithi hivyo yanaweza kukukwamisha katika ratiba yako ya kuolewa/ Kuoa .Ukirithi Jina Baya Lazima Na Mabaya Yakuvae. Ndio Sababu BWANA YESU Alikuja Duniani Kuwasaidia Wanadamu Wanyonge Wanaoteswa Hata Na Majina Yao. YESU Alidhihirishwa Ili Azivunje Kazi Zote Za shetani( 1 Yohana 3:8b). Mwite Naye Ataitika Na Utapona.
 Jifunze Kuheshimu Watu Na Kuishi Maisha Ya Kawaida, Vaa Nguo Vizuri Na Zenye Kusitiri Mwili Wako, Epuka Kuvaa Nguo Za Kikahaba, Pia Epuka Kuvaa Nguo Zenye Kung'aa Sana Maana Utaonekana Kama Yezebeli, Yaani Wanawake Wanaowatawala Waume Zao Na Kupenda Kujisifu Na Kutumbukia Kwenye Uasherati. Watu Wanapenda Kuona Utukufu Wa MUNGU Ukiangaza Kwako Binti. MUNGU Anakupenda Sana Na Anakuwazia Mema Sana. BWANA YESU Anakuhitaji Kwenye Ufalme Wake. Kataa Dhambi, Ogopa Dhambi, Usifanye Dhambi Na Ikimbie Dhambi.

Kijana hakikisha hujitengi na mpingi , na Biblia inasema hivi kwa watu wote wakiwemo vijana. BWANA YESU Anasema: Mwenye Kudhulumu Na Azidi Kudhulumu; Na Mwenye Haki Azidi Kufanya Haki; Na Mtakatifu Azidi Kutakaswa. Tazama, Naja Upesi, Na Ujira Wangu U Pamoja Nami, Kumlipa Kila Mtu Kama Kazi Yake Ilivyo - Ufunuo 22:11-12. Ndugu Yangu Kazi(matendo) Yako Ikoje. Kataa Dhambi, Ogopa Dhambi, Usifanye Dhambi Na Ikimbie Dhambi. BWANA YESU Anakupenda Sana.
Ubarikiwe sana na wewe uliyeko kwenye process ya kutafuta mchumba nakuomba uzingatie hayo hapo juu, kumbuka tunaishi katika dunia yenye kila aina ya ubaya. tunamhitaji BWANA YESU ili tupone.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.

                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292
 
              mabula1986@gmail.com
  MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

  MUNGU Akubariki.

Comments