Mungu ameweka kitu cha pekee kwa mwimbaji huyu kutoka Tanzania, huduma aliyonayo ni ya aina yake, uimbaji alionao ni wa kipekee kabisa, sauti yake na mpangilio wa maneno katika nyimbo zake ni wa kipekee kabisa. Hakika Mungu atabaki kuitwa Mungu. Na Mungu anamtumia kama chombo chake kuleta ujumbe kwetu sisi wanadamu
Jumapili ya hii itakuwa ni siku yako ya kipekee kushuhudia matendo makuu ya Mungu kwa njia ya uimbaji kutoka kwa mwanadada wa Yesu aliyeamua maisha yake kuwa kwa Yesu na uimbaji wake ni wa kumtukuza Mungu. Dada huyu aliyoona hakuna faida ya kuimba nyimbo za kijamii bali ni kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu. Kuna vitu ataenda kuachilia katika madhabahu ya kanisa la Askofu Katunzi wa PTA pale Sabasaba na watu wataenda kufunguliwa kwa njia ya uimbaji. Siku hiyo utajua maana ya NAUCHEKA KWAKATI UJAO una maanisha nini?
Watu wa Mungu, kama siku hiyo utakuwa hauna la kukuzuia kufika mahali pale basi nakuomba sana ufike ili Mungu afanye jambo katika maisha yako kwa kupitia uimbaji wa Leah Amosi. Tumeombewa sana na wachungaji, maaskofu, wainjilisti, walimu, mashemasi, mapadre, sasa ni zamu ya waimbaji kufanya kazi ya Bwana kwa njia ya uimbaji ili wewe na mimi tuinuliwe
Mimi nisikuchoshe sana ila nikukumbushe kuwa kutakuwa na waimbaji wengi sana kama unavyowaona katika tangazo hapo chini

Comments