Mwimbaji nguli wa muziki wa Injili hapa
Tanzania,aliyefahamika kwa wengi kama Steven Mwikwabe, ameamua kufumua
michakato yote na malengo yote ya ndoto ya kizamani na kuja na mtazamo
mpya.
Uamuzi huu ameufanya baada ya kuwa
ametoa albamu tatu tangu mwaka 2007 hadi mwaka 2013.Albamu ya kwanza
ilikuwa Roho kaa ndani yangu,ya pili ilikuwa Rafiki wa kweli ambayo
ilimtambulisha sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi na kumfanya
kuingia katika "AMERICAN SONGWRITTING COMPETITION" mwaka 2012.
Kupitia changamoto hii wimbo wake wa
Rafiki wa kweli aliouweka katika kinyang'anyiro hicho,alijikuta
akijifunza vitu kutoka kwa watu ambao walikuwa ni wapinzani wake.
Ndipo alipoamua kufanya mabadiliko ya
muziki wake.Japo alitoa toleo jingine ambalo halikuwa na mabadiliko
makubwa,ambalo ni "WEWE WAJUA".Baada ya kusikiliza kazi hii ya
tatu,aliamua kubadilisha mazingira ili kupata mwelekeo mpya wa
kimziki,utokanao na asili yake.
Sasa,kutokana na historia ya hapo nyuma
na kuona kwa mtazamo jinsi nyimbo za Tanzania zinavyochukuliwa nje ya
nchi,akagundua panahitajika ubunifu mpya.Baada ya kutulia na kumuomba
Mungu kwa muda mrefu,ameweza kuchukua maamuzi magumu ya kuanza moja na
miundo mipya kihuduma,kimasoko,kimahadhi na maudhui yenye taswira mpya.
Ni gharama kubwa kuchukua maamuzi kama
haya kisaikolojia,lakini Mungu aliepanda mbegu ya uimbaji ndani yake
hakuwahi kubadilisha majina ya waliotangulia ikawa shida,hivyo hata
kwake anaona ni uzao mpya utakaoleta mapya katika jamii inayomjua Mungu
na isiyomjua.
Kwa sasa ni wakati wa kuendelea
kutengeneza na kuvumbua kilichojificha ili kiweze kuwa wazi kwa walio
wengi,zoezi hili ni zoezi gumu ambalo hutumia muda mwingi kufikiria
namna itakavyowezekana kwa nguvu za Mungu kupenya ndani ya wote
wasiokijua kile kijacho.
Anawashukuru wote waliokuwa naye bega
kwa bega katika huduma na tarajia ujio mpya wenye mlengo mpya,nia mpya
mpya,mahadhi mapya na huduma yenye mtazamo mpya unaoendana na mabadiliko
ya kiteknolojia.
Kumpata Steve Wamara,tumia namba hizi:-
+255 684-107 900
+255 656-999 965
Au
Email:stevewamara@gmail.com
Comments