
BWANA YESU
asifiwe.
Mhubiri
3:1-2a ‘’Kwa kila jambo kuna majira
yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati
wa kufa’’
MUNGU
amenipa ujumbe kwa ajili yako na kwa ajili yangu pia. Kila mtu ajiulize na
kujijibu. Maswali haya yatakufanya ujitambue na utambue unaishi kwa sababu gani
na pia kama ukiondoka leo utaenda wapi.
A.
Mimi
ni nani?
B.
Kwanini
niko hai leo?
C.
Kwanini
MUNGU aliniumba?
D.Dunia imejaa dhambi, je nitaponaje?
E.Je
natakiwa kufanya nini muda ambao niko hai?
F.
Nikiondoka
duniani nitaenda wapi?
G.Nitakuwa wapi milele ijayo?
Karibu.
1.
Mimi ni nani?
‘’MUNGU
akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa
baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye
kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
MUNGU akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. MUNGU akawabarikia, MUNGU akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.-Mwanzo 1:26-28.
MUNGU akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. MUNGU akawabarikia, MUNGU akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.-Mwanzo 1:26-28.
-Kila
mwanadamu aliumbwa na MUNGU. Mwanzo MUNGU alimuumba Adamu na Eva na kupitia hao
sisi sote tuliumbwa.
-Muumbaji ni
MUNGU ndio maana sio kila mwanamke anazaa. Sio kila mwanamume anazaa. Mtoto
huja kwa kibali cha MUNGU na kwa makusudi ya MUNGU. Ndio maana kila mara
makanisani tunasikia wanandoa wakishuhudia kwamba ‘’Tunamshukuru MUNGU kwa
kutupa zawadi ya mtoto’’ Sijawahi kumuona binadamu hata mmoja anayejisifia
kwamba ‘’Najishukuru kwa sababu nimezaa’’ bali wote kwa kutambua kwamba
aliyeleta mtoto ni MUNGU na sio mwanadamu. Ayubu 10:8 ‘’Mikono yako imeniumba
na kunifinyanga; Nawe utageuka na kuniangamiza?’’
Mpe MUNGU
utukufu na heshima kwa sababu yeye ndiye aliyekuumba. Tambua kwamba
-MUNGU
anakupenda kuliko wote wanaokupenda.
-MUNGU
hataki uangamie.
-MUNGU
anakupa pumzi ya uhai bure.
-MUNGU
ameandaa njia ya wokovu kwa ajili yako.
2.
.Kwanini
niko hai leo?
Maombolezo
3:22 ‘’Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.’’
Ndugu yangu
kama unadhani kwamba uko hai kwa sababu ya dawa uliyopewa na mganga pole sana.
Kma unadhani
uko hai kwa sababu ya pesa zako pole sana.
Kama
unadhani uko hai kwa sababu mlinzi uliyemwajiri pole sana.
Wanaokufa
wengi wana walinzi kama wewe, wanatumia
dawa za kienyeji kama wewe lakini wamekufa na kingine hakuna mganga wa kienyeji
ambaye anaishi siku zote bali hata wao hufa tu. Ndugu uko hai kwa sababu ya
Neema na ulinzi wa MUNGU BABA wa mbinguni.
Ndugu mpe
utukufu yeye na tena amekuacha uwe hai leo kwa sababu maalumu, Tumika kwa BWANA
, Mche MUNGU, Tengeneza maisha yako na tumika katika kuwasaidie wengine ili
wamjue BWANA anayeokoa.
-Ndugu
unaishi kwa sababu MUNGU anataka ubadilike na kumrudia yeye.
- MUNGU
amekuhifadhi hai ili umtumikie. Ndiposa Mtume Paulo anasema katika nyaraka zake
kwamba ‘’ Kuishi ni KRISTO na kufa ni faida’’ Yaani kama ataendelea kuishi basi
atamhubiri KRISTO kwa mataifa na kama akifa basi ataenda kupumzika mbinguni
ambapo huenda watakatifu baada ya kumaliza kazi yao ambayo MUNGU aliwapa
duniani. Huyu alikuwa ni mtakatifu, Vipi kwa upande wako ndugu?
Kwanini uko
hai leo? Tafakari na tambua kwamba uko hai kwa sababu kuna sababu ya MUNGU kukuweka
hai yawezekana MUNGU anakuvumilia kwamba labda utapata ufahamu na kuacha
dhambi, anakuvumilia japokuwa ni kwa kitambo tu.
3.
Kwanini
MUNGU aliniumba?
Ndugu MUNGU alikuumba kwa kusudi maalumu na kwa ajili ya
kumwabudu. Ona jinsi MUNGU alivyomwambia Yeremia Katika Yeremia 1:5 ‘’ Kabla
sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa;
nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.’’
Yeremia wa
leo ni wewe, umeumbwa kwa kusudi jema la MUNGU.
Ndugu yangu
nakuomba liishi kusudi la MUNGU la kukuumba na sio kuishi kwa kulitumikia
kusudi la shetani. Maana wengi wamejitenga na MUNGU aliyewaumba na
kujiungamanisha na shetani, ni mbaya sana kumsahamu aliyekuumba na kuanza
kumtukuza adui yako.
Shetani ni
adaui wa kila wanadamu, ndiye aliyesababisha kifo, ndiye aliyeleta dhambi,
ndiye aliyesababisha laana na hata ukimtumikia hana shukrani na kama ukifa
katika dhambi ataanza kukutesa kuzimu. Ndugu zangu tumkimbilie BWANA YESU ili
tuokoke na moto wa milele.
-Ndugu
umeumbwa kwa kusudi jema la MUNGU.
-Litumikie
kusudi la MUNGU.
-Kataa dhambi,
ogopa dhambi, ikimbie dhambi na usitende dhambi.
4.
Dunia
imejaa dhambi, je nitaponaje?
Warumi 5:6-8 ‘’Kwa maana hapo
tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, KRISTO alikufa kwa ajili ya waovu.
Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu
kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Bali MUNGU aonyesha pendo lake yeye
mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa KRISTO alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali
wenye dhambi.’’
Ndugu yangu
japokuwa dunia imejaa dhambi lakini yupo Simba wa kabila la Yuda YESU KRISTO
anayeokoa.
-Huu ni
upendo wa MUNGU wa ajabu sana kwetu. MUNGU ameandaa uzima wa milele ambao umo
ndani ya Mwanaye pekee YESU KRISTO.
-Kama
tunataka kuliishi kusudi la MUNGU basi tumpe YESU maisha yetu.
-MUNGU
hataki hata mmoja apotee ndio maana anatualika bure kabisa kushiriki uzima wa
milele kupitia Mwanaye YESU KRISTO.
Kuna watu
wengine hudhani kwamba MUNGU ameandaa njia nyingi za kuwapeleka uzimani
wanadamu lakini kumbe njia ni moja tu yaani YESU KRISTO. Yohana 14:6 ‘’ YESU
akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji ila kwa
njia ya mimi. ‘’ Matendo 4:12 ‘’ Wala hakunakwa BABA, wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana
hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi
kuokolewa kwalo. ‘’ Ila
ni jina la YESU KRISTO tu , Warumi 10:13 ‘’ kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina
la BWANA ataokoka. ‘’
5.
Je
natakiwa kufanya nini muda ambao niko hai?
Mathayo 28:19-20 ‘’ Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote
kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU; na
kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja
nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.’’
Ndugu zangu huu ni wakati
wa kumtumikia MUNGU. Huu ni wakati wa kuwaambia wanadamu kwamba YESU KRISTO
anaokoa. Ni wakati wa Mama kuihubiri familia yako ili ijisalimishe kwa YESU, ni
wakati wa mtoto kuwaombea wazazi wako na kuwashauri kuokoka maana hizi ni
nyakati mbaya.
Wafilipi 2:13 ‘’ Kwa
maana ndiye MUNGU atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa
kulitimiza kusudi lake jema. ‘’
MUNGU analo kusudi kwa
wanadamu wote ndio maana anataka kukutumia wewe ili watu wote waokoke. Wewe
utajiona kama unatumika / unahubiri/ unafundisha/ unawaonya watu ili wakimbilie
kwa YESU na kupona kumbe ni MUNGU anayetenda kazi ndani yako ili tu kulitimiza
kusudi lake jema.
Muda huu ukiwa hai ndio
muda wa kumtumikia MUNGU, hakuna wakati mwingine wowote.
6.
Nikiondoka
duniani nitaenda wapi?
Warumi
14:8-9 ‘’Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa BWANA, au kama tukifa, twafa kwa
BWANA. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya BWANA. Maana KRISTO alikufa akawa hai tena kwa sababu hii,
awamiliki waliokufa na walio hai pia.''
Kuna
wanaokufa kwa BWANA YESU na kuna
wanaokufa kwa shetani. BWANA YESU yuko mbinguni hivyo na wanaokufa katika yeye
huenda mbinguni. Na shetani yuko kuzimu hivyo wanaokufa katika shetani/ dhambi
huenda kuzimu. Unaweza kutazama mfano wa Lazaro na Yule tajiri, Lazaro
alipokufa alienda mbinguni kuungana na akina Ibrahimu na tajiri alipokufa
alienda kuungana na majini kuzimu.
7.
Nitakuwa wapi milele ijayo?
1
Thesalonike 4:16-17 ‘’Kwa sababu BWANA mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na
mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya MUNGU; nao waliokufa katika
KRISTO watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia,
tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki BWANA hewani; na hivyo
tutakuwa pamoja na BWANA milele.’’
Ni heri kufa
katika KRISTO.
Ni heri
kumpokea BWANA YESU leo.
Ni heri
kumwishia BWANA YESU.
Ufunuo
20:12-13 ‘’Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti
cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni
cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile
vitabu, sawasawa na matendo yao. Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Waka Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani
yake; na Mauti nahukumiwa
kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.’’
Kuna
watakaoishi uzimani milele na kuna watakaoishi motoni milele.
BWANA YESU
atuokoe.
BWANA YESU
atusaidie maana hakuna njia nyingine ya uzimani nje na BWANA YESU.
Yakobo 5:8 ‘’ Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa
maana kuja kwake BWANA kunakaribia. ‘’
Kwa sasa naishia hapo,
MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea
BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu
kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana
makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani
aliko KRISTO BWANA.
Comments