![]() |
Watu wakiangalia uokoaji baada ya jengo mojawapo la kanisa la SCOAN kuanguka. |

Karibu watu 15 wamekufa na mamia wengine bado wamefukiwa baada ya Jengo mojawapo la Kanisa la mhubiri TB Joshua kuporomoka jana Ijumaa.
Kanisa hilo
- Synagogue Church of All Nations (SCOAN) lililoko Ikotun, Lagos lenye
ghorofa sita - lilibomoka jana majira ya saa 7 mchana (saa 10 kwa Saa za
Afrika Mashariki).
Msemaji wa
Mamlaka ya Huduma ya Dharura katika Jimbo la Lagos, Friday Adeboayo,
alithibitisha kwamba miili ya watu 15 iliopolewa kwenye kifusi.
TB Joshua ni miongoni mwa wahubiri maarufu wa Nigeria akiwa
na maelfu ya wafuasi ulimwenguni kutokana na miujiza yake anayoifanya
pamoja na utabiri.
“Watu wanatoka kila sehemu duniani kushuhudia na kupokea miujiza ya Mungu kupitia maisha ya Nabii TB Joshua,” ndio ujumbe ulioandikwa kanisani hapo.
Katika maendeleo mengine, Wakala wa Taifa wa Huduma za Dharura (NEMA) umetoa taarifa kuhusiana na jengo hilo lililoporomoka.
Msemaji wa NEMA, Ibrahim Farinloye, alisema kwamba jengo hilo awali lilipewa kibali cha kujenga ghorofa mbili, lakini katika mshangao wa wengi, zikajengwa ghorofa tano.
“Hizo nyingine tatu zilikuwa zinaendelea kujengwa wakati jengo lilipoporomoka saa 7 mchana (Saa 10 alasiri) wa Ijumaa.
“Kabla ya kuwasili kwa waokoaji hao, karibu watu 15 walikuwa wameopolewa wakiwa hai na watatu wakiwa wamekufa. Waokoaji wameokoa watu watatu wakiwa hai na maiti tatu, lakini kuna watu wengi ndani,” alisema Farinloye kupitia kwenye ujumbe wa sms.
POLENI SANA SCOAN KWA TUKIO HILI LA BAHATI MBAYA, NA HONGERENI SANA KWA HUDUMA NJEMA YA KUMTUKUZA MUNGU ALIYE HAI.
![]() |
Kanisa la Tb Joshua |
Comments