MUNGU HANA USAHAULIFU.

MUNGU Hana Usahaulifu.
Neno Usahaulifu Linatokana Na Neno Kusahau. 
Kusahau Ni Kitendo Cha Mtu Kuacha Kufanya Jambo Fulani Ambalo Lilikuwa Limepangwa Au Umepanga Mwenyewe. 

Wewe Mteule Wa BWANA YESU Ni Muhimu Kujua Jambo Hili Kwamba MUNGU Hana Usahaulifu. 

Katika Biblia MUNGU Mwenyewe Anasema Neno Hili Isaya 49:14-16 " Bali Sayuni Alisema, YEHOVA Ameniacha, BWANA Amenisahau. Je Mwanamke Aweza Kumsahau Mtoto Wake Anyonyaye, Hata Asimhurumie Mwana Wa Tumbo Lake? Naam, Hawa Waweza Kusahau, Lakini Mimi Sitakusahau Wewe. Tazama, Nimekuchora Katika Vitanga Vya Mikono Yangu; Kuta Zako Zi Mbele Daima.".

  -Ndugu Yangu Ahadi Ya MUNGU Maishani Mwako Ni Kweli Na Ndiyo. 
-Usikate Tamaa Binti Unayeona Umri Unakwenda Na Hakuna Kijana Wa Kukuoa, Ongeza Maombi Na Acha Manung'uniko Na Kujilinganisha Na Wengine. 

-Usiseme MUNGU Amekusahau Kijana Kwa Maana Umeomba Muda Mrefu Ili Upate Kazi, Songa Mbele Na YESU Na BWANA Anaandaa Jambo Jema Mbele Yako, Ongeza Maombi Na Usitegemee Wanadamu. 

 Watu wengi sana hupishana na baraka zao maana wanaomba na MUNGU anawaambia kwamba atawapa kile walichoomba lakini baada muda kidogo imani yao inapungua na kurudi nyuma na kipindi wakirudi nyuma na majibu ya MUNGU yanakuwa yanakuja lakini MUNGU anaghairi baada ya kuwakuta wamerudi nyuma.

Zaburi 62:8. Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; MUNGU ndiye kimbilio letu. 
-Wanaomtumaini MUNGU hawakati tamaa.
-Wanoamwamini MUNGU wana uhakika na MUNGU wao wala hawawezi kumdhania kwamba MUNGU kasahau ahadi zake kwako.
Biblia hapo juu imesema kwamba ''Ifunueni mioyo yenu'' yaani semeni mnahitaji nini kwa BWANA , Kwa lugha nyingine unaweza kusema kwamba ''Ombeni kwa MUNGU''

Yohana 15:7 . Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. 
Hakikisha neno la MUNGU linakaa kwa wingi moyoni mwako.
 Waebrania 4:16 "Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji." 
Ndugu uliyempokea BWANA YESU tambua kwamba maombi ni haki yako, yaani MUNGU atakusikia na kukujibu hata bila kupitia kuombewa na wengine. 
 Je MUNGU yuko tayari kusikia maombi yetu na kutujibu.

Mathayo 7:11 "Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema je! si zaidi BABA yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?". 
MUNGU hajakusahau ndugu yangu.
 Anakuandalia jambo jema. 
Endelea tu kusubiri kwa maombi. 
na tambua jambo hili kwamba ''ILI MUNGU AWE MUNGU NI LAZIMA YEYE NDIYO AAMUE NA SIO SISI WANADAMU TUMUAMLIE'' 
Anatujua vyema ndio maana hutuandalia mema katika muda sahihi. tusiache kuomba na wala imani yetu isipungue na kudhani kwamba MUNGU ametusahau.
MUNGU hana usahaulifu hata kidogo.
 ''MUNGU si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?-Hesabu 23:19''
MUNGU sio Mwanadamu hata aseme uongo
 MUNGU anajibu maombi.
Ndugu omba siku zote.  
MUNGU Akubariki Na BWANA YESU Anakupenda Sana.
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           +255714252292

             mabula1986@gmail.com
  MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

 

Comments