MWALIMU WA SUNDAY SCHOOL ALIYEPIGILIWA KWENYE MTI AZUNGUMZIA MASAIBU YAKE

Mwalimu wa Kanisa katoliki Peter Asutsa akielezea mkasa uliomfika.
(Picha:  NATION MEDIA GROUP)

Mwalimu mmoja kanisa katoliki nchini Kenya, ambaye aliibiwa fedha zake na yeye mwenyewe kupigiliwa msumari kwenye mti, amezungumzia mkasa huo.

 Wezi hao walimuibia dola ishirini na nne Peter Asutsa Alhamisi iliyopita, kabla ya kuupigilia kwa msumari mkono wake kwenye mti katika msitu mmoja uliopo Eldoret, magharibi mwa Kenya. 

Mwalimu huyo wa mafunzo ya Jumapili (Sunday School) alikaa kwa saa kumi na sita akiwa katika maumivu makali kabla ya kuokolewa na polisi.

Amesema aliweza kuwasiliana na mke wake kwa kutumia simu yake aliyokuwa ameificha kwenye nguo yake ya ndani. 


Comments