Shalom, neno changamoto linaweza kuwa na maana kadhaa, katika
somo hili nimefafanua changamoto kama ushindani au mashindano baina ya
pande mbili au zaidi, kila upande ukidai uhalali wa kile unachokiamini
na hivyo kushawishi upande wa pili ukubaliane na kukifuata kile
unachokiamini. Kutoka kwenye dhana ya vita vya kiroho (Waefeso 6:10),
Shetani kama mfalme wa giza ndiye mwenye kuzileta changamoto mbalimbali
dhidi ya wana wa Mungu kwa nia ya kuwaondoa kwenye nafasi zao za
ki-Mungu na hivyo kuwatumia kufanikisha makusudi yake ya ufalme wa giza
na mwishowe kuwaharibu kabisa. Zifuatazo ni sehemu ya changamoto kubwa
zenye kuwakabili vijana;
- Kuipenda dunia (1Yohana 2:15 -16).
Ule mstari wa 15 unasema ‘Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia, Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake’.
Sisi sote leo tu mashahidi juu ya nama ambavyo vijana wengi,
wanavyovutwa na nguvu ya dhambi inayotenda kazi duniani kupitia taama ya
mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima. Shetani kwa kutumia mambo
hayo amewafanya wengi sana kuipenda na kuifuatisha namna ya dunia hii,
wasijue kwamba nia ya mwili ni mauti na wale waufutao mwili hawawezi
kumpendeza Mungu (Warumi 8:5-6)
- Kufanya maamuzi muhimu yahusuyo maisha
Vijana wengi wapo katika rika ambalo wanahaja ya kuoa au kuolewa na
wengine bado wanasoma katika nagzi mbalimbali. Katika nyakati za sasa
imeakuwa ni changamoto kubwa sana kwa kijana kumpata mwenza shaihi wa
maisha sambamba na kujua nini asome ambacho kina uhusiano mkubwa na wito
wa kusudi la Mungu katika maisha yake. Tambau kwamba (a) Mungu
anapokupa fursa ya kusoma, si suala la kusoma bali kusoma kitu ambacho
kipo connected na future ambayo Mungu amakuandalia (b) si kila
mwanamume/mwanamke anafaa kuwa mwenza wako wa maisha. Naam ile kwamba
wako wengi ambao wangetamani kuishi na wewe kama mke au mume ni ishara
kwamba wengi wao si wenza sahihi wa kuishi na wewe. Katika kutafuta na
kupata mwenza wa maisha vijana wengi leo wanatumia akili zao bila
kumshirikisha Mungu ipasavyo, wasijue kwamba ndoa isiyounganishwa na
Mungu, ni kikwazo kikubwa katika kulitumikia shauri la BWANA Mungu wao.
- Kuishi kwa amani katika ndoa
Hii inahusu wale ambao walishaoana. Kwa zaidi ya miaka saba katika
kufundisha na kuandika masuala yahusuyo mahusiano ya wanandoa
nimejifunza na kuthibitisha kwamba ndoa nyingi za vijana zina matatizo
makubwa kuliko wengi wanavyofikiri juu ya ndoa hizo ambazo wanaamini ni
changa. Binafsi nimeshuhudia ndoa nyingi ambazo ni chini ya miaka mitano
lakini wanandoa husika hawalali kitanda kimoja tena, hawaaminiani tena,
hawapeani unyumba tena nk. Naam kuishi vema na mwenza limekuwa gumu
sana kwa wanandoa wengi ambao ni vijana na baadhi yao wanajuta kwa nini
walioa au kuolewa.
- Matumizi ya teknolojia (mtandao)
Kijana mwenzetu Danieli alionyeshwa kwamba katika siku za mwisho
maarifa yataongezeka sana, jambo ambalo ni dhahiri katika kizazi chetu
bila shaka. Sote tu mashahidi juu ya namna vijana wanavyotumikishwa na
nguvu ya matumizi mabaya ya mitandao mbalimbali ya kijamii. Sote tunaona
namna vijana wengi wanavyotumia muda mwingi kusoma na kuangalia vitu
visivyofaa kwenye mtandao na mbaya zaidi tunaona ni kawaida. Kadri
kijana anavyaongalia vitu vichafu ndivyo anavyoyachochea nguvu ya dhambi
na kutenda mabaya ndani yake, naam ndivyo anavyoingiza roho chafu za
kila namna ndani yake.
Hali ngumu ya kiuchumi inaleta ushawishi kwa vijana kujiingiza kwenye
mambo ambayo yanaharibu mahusiano yake na Mungu. Naam wapo ambao
imefika mahala wameamua kuingia kwenye biashara haramu za madawa ya
kulevya, zinaa, uasherati, kutamani kuishi maisha ya kuiga, na mbaya
zaidi hata wale ambao wanakiri kumpokea Yesu nao wanaishi maisha ambayo
hayana ushuhuda makazini mwao, mtaani mwao nk hususani linapokuja suala
zima la uaminifu, mahusiano na fedha.
Pengine zipo changamoto nyingine, lakini hizi tano nilizoziandika
ndizo ambazo nimeona umuhimu wake zaidi kuzifundisha kwa kuwa zina
athari kubwa sana sit u kwa vijana wenyewe bali zaidi kwenye ufalme wa
Mungu wetu. Katika sehemu ya pili nitaanza kwa kukuonyesha ni kwa namna
gani kijana anaweza kuazikabili changamo husika.
Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA!
Na: Patrick Sanga
Comments