PAG CITY CENTRE ZANZIBAR WAJIFUNZA UJUMBE KUHUSU MALANGO YA KUZIMU

  Waimbaji wakiwa wana mwabudu BWANA kabla  ya kuanza ibada.
        Ujumbe uliofundishwa unaitwa MALANGO  YA  KUZIMU.
Pata machache kuhusu somo hilo.

Katika  somo  hili  la  malango  ya kuzimu  tutapata  kujua  kazi  za  MAJINI  na MAPEPO.

MAPEPO:  Ni jeshi  dogo  la  kuzimu linaliofanya  uharibifu,lakini  linaaribu  na  kuangamiza  mambo  mengi  sana.


Mtu mwenye  mapepo  mara  nyingi  hauwezi  kumuona  kwa macho  ya  kawahida  ni  mpaka  uwe  katika  macho  ya  Rohoni  ndo  unaweza  kumgundua.

Zifuatazo  ni  dalili  za  mtu  mwenye   mapepo:


  1. Macho  yenye kiburi,
  2. Ulimi  wa  uongo,
  3. majigambo mengi  na kujifanya mjuaji wa  kila  kitu.
  4. Miguu  yake  ni  mwepesi  kukimbilia  maovu.
5:Ni  mtu  ambaye  anapenda  sana  kukaa  kwenye vikao   vya  masengenyo n,k. 
           JESHI  LA  KUZIMU   
Mapepo  ni  ajent  wadogo  sana  wa  kishetani  wanaofanya  kazi  kwa kiele  ele kuliko  majini.

Efeso 6:11-12.

Vaeni  silaha  zote  za  Mungu,mpate  kuweza  kuzipinga hila  za  shetani.Kwa  maana  kushindana  kwetu  sisi si  juu ya damu  na  nyama; bali  juu  ya  falme  na  mamlaka,juu  ya  wakuu  wa  giza  hili, juu  ya  majeshi ya mapepo  wabaya katika ulimwengu  wa  roho.        

  Mapepo  wabaya katika  ulimwengu wa roho ni  hawa ambao  wanakuwa  ajent  wadogo  sana  kwa  ajili  ya uharibifu.

MAJINI:
            
Ni shetani  aliyepewa  ruhusa  kutoka  kwa  mmiliki  wake  ili  atawale kwa jambo  fulani

 Yanamilikiwa  na yanafugwa,yana  nguvu  kuliko   mizimu,  yana  uwezo   mkubwa wa  kuangusha  ata ndege ,meli magari  kwa  kutaka  damu  za  watu.

Mapepo  yenyewe  hayatumii  damu,bali  yenyewe  unyonga  na  kutesa  tuu,na  usababisha  maradhi makubwa makubwa  kama  KISUKARI, H.I.V, KANSA, UVIMBE TUMBONI,BP nk.


MUNGU akubariki na zifuatazo ni Habari picha katika ibada hiyo.



 Waimbaji wakiwa wana mwabudu BWANA kabla  ya kuanza ibada.

 Ibada hiyo ilifunikwa na nguvu za BWANA

Kulia ni mtumishi wa Mungu ELIUDI ambaye Mungu anamtumia  katika kiwango kikubwa mno.

 Mwimbaji wa nyimbo za injili akimtukuza  MUNGU.


 Mtumishi wa MUNGU ELIUDI MJWAUZI akifundisha kuhusu tofauti ya MAJINI na MAPEPO.
 Mtumishi wa Mungu ELIUDI MJWAUZI akiwaombea  wagonjwa  waliokuwa wanasumbuliwa  na nguvu  za  giza.
 Mtumishi wa Mungu ELIUDI MJWAUZI akimwombea mama  aliyekuwa na nguvu  za giza.

Watumishi wa Mungu wakimwombea dada  aliyekuwa na ngome  za  Majini  na kumtesa  lakini alipata  kufunguliwa  na  kwa  sasa  yuko  huru akimtukuza  Mungu.


Barikiwa  sana  mtu  wa Mungu 
Ni  mimi ndugu  yako 
Baraka  Audax
0717  461006
Injili   ya Kristo  Zanzibar.

Comments