PAPA FRANCIS AFUNGISHA NDOA 20 KWA SIKU MOJA.

Jumapili ya tarehe 14, familia zaidi ya 20 zimekuwa zenye shangwe jijini Roma huko Vatican, baada ya papa Francis kufungisha ndoa kwa umati huo wa watu. 

Waume 20 kwa wake 20. na hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Papa kufanya hivyo tokea aapishwe kuwa kiongozi wa kanisa hilo lenye takribani zaidi ya wafuasi bilioni 1.3 ulimwenguni kote. 

 Ibada hiyo ya ndoa hiyo ambayo iliambatana na usia wa papa kwa kanisa kuhusu kusamehe, ilikuwa na mwanamama mmoja ambaye tayari likuwa na mtoto kwenye ndoa yake iliyopita, huku pia wengine wakiwa wanaishi pamoja kabla ya kukata shauri na kufuata taratibu husika kwa mujibu wa kanisa katoliki. 
 
 Tukio hilo ambalo lilivutia maelfu ya watu, limekumbushia enzi ambayo Papa John paull II alifungisha ndoa huko Roma, ikiwa ni mwaka 2000, miaka 14 tokea kipindi hicho, hadi kuona 'mnuso' kwa mara nyingine tena. "Kanisa lazima liache kukazania kuhudu kufundisha (kukemea) kuhusu utoaji mimba, vidonge vya uzazi na mahusiano ya jinsi moja, na badala yake liwe lenye kurehemu, vinginevyo liwe hatarini kuanguka mithili ya kadi zilipangwa kwa kusimama juu ya nyingine. Amenukuliwa Papa na kunogea kuwa ndoa ni maisha halisi, na si maigizo kama kwenye runinga. 

Kwenye ibada hiyo, Papa Francis, ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Roma, aliwaita wanandoa kwa majina yao mmoja mmoja ili kuitikia kiapo cha kuishi na wenza wao kwa uaminifu maisha yao yote.

Comments