SABABU 8 ZINAZOTUFANYA TUULINDE MOYO KULIKO VYOTE TULINDAVYO.



 
BWANA YESU asifiwe!
Karibu tule chakula cha uzima.
ROHO MTAKATIFU amefunua vitu hivi adimu ili tujifunze na kuijua kweli inayoweka huru.
Mithali 4:23 ‘’Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. ‘’
Kwanini kila mtu analazimika kuulinda moyo kuliko yote ayalindayo?
Ni kwasababu tabia ya mtu hutoka moyoni na sio rohoni.
SABABU 8 ZINAZOTUFANYA TUULINDE MOYO KULIKO VYOTE TULINDAVYO.
     1.  Kwa sababu kwa moyo mtu huamini hata kupata uzima. Warumi 10:10 ‘’ Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. ‘’

           2.  Moyo unalindwa ili usitoe mabaya. Yeremia 4:14 '' ... jioshe moyo wako usiwe na uovu, upate kuokoka. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako hata lini? ''  pia  Mathayo 15:19 ‘’Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano; ‘’
       3.Moyo ni shamba la kupandwa Neno la MUNGU. Mathayo 13:15 ‘’Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. ‘’
        4.  Moyo hutoa Chemichemi za uzima. Mathayo 5:8 ‘’Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona MUNGU.  ‘’
     5.  Moyoni  hukaa KRISTO.Waefeso 3:17 ‘’ KRISTO akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ‘’
      6.  Moyoni  ni mahali pa amani ya MUNGU. Wakolosai 3:15  ‘’ Na amani ya KRISTO iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. ‘’
      7.  Moyoni ni makao ya ROHO MTAKATIFU. 2 Kor 1:22 ‘’ naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya ROHO mioyoni mwetu. ‘’
     8.   Moyoni ni mahali pa upendo wa MUNGU . Warumi 5:5 ‘’ na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la MUNGU limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na ROHO MTAKATIFU tuliyepewa sisi. ‘’

Ni namna gani nitaulinda moyo wangu?
Kuna njia za kuulinda moyo wako? Njia hizo ni muhimu sana kwako na zinakuhitaji wewe ili moyo wako ukae salama daima na moyo wako usikupeleke motoni. Zingatia njia hizo 8 hapo chini.
                     NJIA 8 ZA KUULINDA MOYO..
1.  Weka Neno la MUNGU kwa wingi moyoni mwako. Zaburi 119:11 ‘’ Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. ‘’
2.  Epuka vikundi vibaya. 1 Kor 15:33 ‘’Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. ‘’
3.  Sahau yaliyopita.Isaya 43:18 ‘’ Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. ‘’
4.  Usifikiri mambo ya mwilini.I Kor 3:3 ''kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? ''
5.  Ridhika na ulichonacho. Mithali 15:16’’Kuwa na mali chache pamoja na kumcha BWANA; Ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu. ‘’
6.  Jitahidi sana kuomba mara kwa mara. 1 Thesalonike  5:16  ‘’ ombeni bila kukoma;‘’
7.  Usikubali mawazo mabaya yakutawale. Zacharia 8:17 ''wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema BWANA. ''
8.  Mtafute BWANA YESU kila wakati. Zaburi 34:4 ‘’ Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote. ‘’
Naamini umekula chakula hiki cha uzima na umeshiba.
Naamini utatendea kazi hiki ulichojifunza leo.
Unaweza hata uka-Print ili kuwasaidia na maelfu wengine.
Usiache ku-share ujumbe huu ili uwe umehubiri pamoja na mimi na watu wengi zaidi watajua njia za kuwasaidia ili walinde mioyo yao kuliko vyote.
BWANA YESU anakupenda sana na nakuombea Baraka za BWANA YESU siku zote.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292
 
              mabula1986@gmail.com
  MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
  MUNGU Akubariki.



Comments