SABABU ISHIRINI (20) ZILIZOTUFANYA TUMPOKEE YESU KRISTO KAMA BWANA NA MWOKOZI ETU.

BWANA YESU asifiwe ndugu zangu wote.
Leo ninakuletea ujumbe mzuri sana, ujumbe wa kuwapeleka watu uzimani, ujumbe ambao utaongeza imani yako.
Leo tunajifunza SABABU 20 ZLIZOTUFANYA TUMPOKEE BWANA YESU.  Sio kwamba zipo sababu 20 tu bali zipo sababu nyingi sana za kumfanya mwanadamu kumpokea BWANA YESU.
Hakika ni muhimu kwa kila mmoja duniani kumpokea YESU KRISTO kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yake maana nje na yeye hakuna uzima wa milele.
Sababu hizo ni hizi hapa;

1.  YESU KRISTO ndiye  Mwokozi wetu(Warumi 10:13'' kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka.'' )

2.  YESU KRISTO ndiye  aliyetuweka huru mbali na uonevu wa shetani(Yohana 8:36 ''
Basi Mwana(YESU) akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. '' )

3.  YESU KRISTO ndiye aliyetupa uzima wa milele (1 Yohana 5:11-12 ''
Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba MUNGU alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa MUNGU hana huo uzima.'' )

4.  YESU KRISTO ndiye aliyetuchagua sisi (Yohana 15:16 ''
Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo BABA kwa jina langu awapeni. '')
5.  YESU KRISTO ndiye mkombozi wetu pekee (Matendo 4:12 ''
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. '')

6.  YESU KRISTO ndiye aliyetufanya kuwa watoto wa MUNGU (Yohana 1:12-13 '' 
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. '')

7.  YESU KRISTO ni  MUNGU  wetu(Tito 2:13-14 '' 
tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema. '', Yohana 1:1-3  '' Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa MUNGU, naye Neno alikuwa MUNGU.  Huyo mwanzo alikuwako kwa MUNGU.  Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Soma pia Matendo 20:28,Waebrania 1:8.

Katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu MUNGU tu(ufunuo  19: 10). Mara nyingi YESU katika maandiko aliabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. 
Kama YESU asingekuwa  MUNGU, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba YESU ni MUNGU. YESU ni MUNGU katika mwili.'')

8.  YESU KRISTO ndiye aliyetukomboa kutoka kwenye uharibifu kuja kwenye Nuru (1 Petro  1:18-19 ''
Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya KRISTO. '')

9.  YESU KRISTO ndiye  aliyetupa haki yote na ukombozi(Warumi 3:24-25 '' 
wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika KRISTO YESU; ambaye MUNGU amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa. apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye YESU. '')

10.  YESU KRISTO ndiye aliyekufa msalabani kwa ajili ya uzima wa milele wetu(Warumi 5:8-9 ''
Bali MUNGU aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa KRISTO alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.   '')

11.  YESU KRISTO ndiye aliyetuokoa(Waefeso 2;8-9 ''
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu  '')

12.  YESU KRISTO ndiye ambaye manabii wote wa kweli humshuhudia kwamba ni MWOKOZI wetu(Matendo 10:43 ''
Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi. '')

13.  YESU KRISTO ndiye mpatanishi kati yetu na MUNGU BABA (1 Timotheo 2:5-6 '' 
Kwa sababu MUNGU ni mmoja, na mpatanishi kati ya MUNGU na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu KRISTO YESU; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake. '')

14.  YESU KRISTO ndiye aliyetusamehe dhambi (Wakolosai 1:14-15 ''
14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;  naye ni mfano wa MUNGU asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. '')

15.  YESU KRISTO ndye anayetushindia yote (1 Kor 15:55-57 ''
Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.
  Lakini MUNGU na ashukuriwe atupaye kushinda kwa BWANA wetu YESU KRISTO.
'')


16.  YESU KRISTO ndiye  tuliyemkiri na yeye akatupa uzima (Warumi 10:9-11 ''
Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.   '')

17.  YESU KRISTO ndiye yeye aliyetufundisha kumjua MUNGU wa kweli( Yohana 14:6-7,23 ''
YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. YESU akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na BABA yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. '')

18.  YESU KRISTO ndiye atakayetufufua siku ya mwisho (Yohana 11:25-26 ''
YESU akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. '', 1 Kor 15:21-23  '' Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika KRISTO wote watahuishwa.
  Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni KRISTO; baadaye walio wake KRISTO, atakapokuja.
'')



19.  YESU KRISTO ndiye mhukumu wa wanadamu wote( 2 Kor 5:10 ''
Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha KRISTO, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya. '')
20.  YESU KRISTO ndiye aliyetuumba upya  sisi wateule wake.(Waefeso 2:10 ''
Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika KRISTO YESU , tutende matendo mema, ambayo tokea awali MUNGU aliyatengeneza ili tuenende nayo. '')

MUNGU akubariki sana na YESU KRISTO anakupenda sana.



 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.

                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                           0714252292

             mabula1986@gmail.com
  MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments